Kutokana na ushahidi uliotolewa mbele ya mahakama hii, mahakama hii imepigiwa simu na Bi Kidude na imepitia kwa umakini wa hali ya juu ushahidi wote uliotolewa mbele yake na imejiridhisha bila mashaka kwamba;

1) Watuhumiwa wote hawana hatia ya kutenda hayo makosa.

2) Waachiliwe huru mara moja ili mshtakiwa namba moja awahi Kilimanjaro Bus la alfajiri kwenda kutoa ushahidi dhidi ya gaidi kule dar es salaam.

CCM Hoye, CCM hoyeeeee.

Kumbuka ana kesi nyingine huko Moshi, mchezo bado sana huu....
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imehitimisha usikilizwaji wa kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021, inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, hukumu ya Kesi hiyo sasa ni Oktoba 01, 2021.
Hukumu inaeleweka tayari. 7baya ajiandae kuja kumtolea ushahidi Mbowe Kisutu

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imehitimisha usikilizwaji wa kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021, inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, hukumu ya Kesi hiyo sasa ni Oktoba 01, 2021.
ajiandae kulipa faini - ila next time awe makini sana, nafikiri msemo wa "Cheo ni dhamana" atakuwa ameuelewa vilivyo.
 
Ishu ya Sabaya ilikua kutuhadaa kwamba sheria Ni msumeno na Mama n mpenda haki but nothing at all!

Kingine spidi ya kesi, Ni kumtengenezea mazingira sabaya kumezeshwa sumu atakayoenda kuimwaga kwenye inshu ya Mbowe!!

#muda Ni msema kweli'!
Asante kwa ramli
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imehitimisha usikilizwaji wa kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021, inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, hukumu ya Kesi hiyo sasa ni Oktoba 01, 2021.
Kesi zote zingekuwa zinaendeshwa faster hivi, magereza yangekuwa tupu na rushwa ingekupungua sn
 
Kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha namba 105/2021 iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai ole Sabaya na wenzake Silvester Nyegu na Daniel Mbura imekamilka Leo na mahakama imepanga kutoa hukumu Oktoba

1,mwaka huu
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo ,Odira Amworo alisema mara baada ya mawakili wa utetezi kufunga ushahidi wao aliwataka mawakili wa pande zote kuhakikisha ifikapo Septembe mosi mwaka huu wawe wamewasilisha majumisho ya mwenendo wa kesi ili mahakama ifanye maamuzi haraka.

Wakili wa Serikali Mkuu Tumaini Kweka aliiomba mahakama hiyo kufanya majumisho Kwa njia ya maandishi ndani ya wiki moja.

"Tunaomba siku Saba kwa ajili ya kuwasilisha majumisho kuanzia Leo Hadi tarehe moja mwezi wa Tisa tuwe tumekamioisha "alisema Kweka.

Naye wakili kiongozi upande wa utetezi ,Dancan Oola alisema watahakikisha wanaleta maelezo yao kwa tarehe pangwa 1/9/2021 na wapo tayari kupokea tarehe ya hukumu.

Baada ya maelezo hayo wakili Amworo alisema hukumu itakuwa Oktoba 1,2021.

Awali washitakiwa Lengai Ole Sabaya , Silvester Nyegu na Daniel Mbura Kwa pamoja walisomewa mashtaka matatu yakiwemo ya unyang'anyi wa kutumia silaha na Kumpora Mali na fedha ,julai 16 mwaka na baadaye kesi hiyo kuanza kusikilizwa julai 19 mwaka huu.

Kabla ya kukamilika kwa kesi hiyo mshtakiwa wa tatu , Daniel Laurent Mbura (38), aliieleza mahakama kuwa hamtambui mshitakiwa wa kwanza wala wa pili katika shauri hilo na alifahamiana nao walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Juni 4.

Akijitetea mbele ya Hakimu Amworo shahidi huyo pia amekanusha majina yaliyopo kwenye hati ya mashitaka ambayo yanasomeka kama Daniel Gabriel Mbura wakati yeye jina lake ni Daniel Laurent Mbura.

Shahidi huyo aliiomba mahakama kupokea vyeti vyake viwili kuthibitisha majina yake na mahakama ilivipokea.

Akiongozwa kutoa ushahidi wake na Wakili anayemtetea, Fridolin Gwemelo, mshitakiwa wa tatu katika shauri hilo alisema Februari 9 mwaka huu alikuwa nyumbani na hakutoka siku nzima.

Yafuatayo ni mahojiano baina ya wakili wa Serikali Tumaini Kweka na Shahidi Daniel Mbura.

Wakili:katika Kesi hii washtakiwa mpo wangapi.

Shahidi:Tumeshtakiwa watatu,Lengai ola Sabaya, Silvester Nyegu na Daniel Mbura.

Wakili :kuanzia tarehe 16/7/2021 Hadi Leo tarehe 24/7/2021 kitu gani kinachokuwwka mahakamani wewe, Silvester Nyegu na Daniel Mbura?

Shahidi;Ni Mashtaka yanayohusu Unyang'anyi wa kutumia silaha.

Wakili ;Tangia uape hapa mahakamani ulishawahi kuapa kuwa wewe ni Daniel Lawrent?

Shahidi;Hapana

Wakili; Kwa hiyo utakubaliana na mimimkwamba Daniel Mbura na Daniel Lawrent ni watu wawili tofauti?

Shahidi; Ndio

Wakili:ulisema kazi yako ni ufugaji unafuga Nini.

Shahidi;nafuga Kuku,Mbuzi na Ng'ombe

Wakili unamda gani unafuga

Shahidi;Miaka minne

Wakili ;Ng'ombe anachukua muda gani kuzaa?

Shahidi; Miezi Tisa.

Wakili; na Mbuzi

Shahidi;Miezi mitatu

Wakili ; na kuku

Shahidi ;inategemea na aina ya kuku .

Nje ya mahakama wakili wa Serikali Mkuu Tumaini Kweka alisema kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa julai 16 mwaka huu na imechuku takribani siku 35 kumalizika na wao kama waendesha mashtaka wamekamilisha vema na wanaiachia mahakama iweze kutoa hukumu.

Naye wakili kiongozi upande wa utetezi, Dancan Oola alisema kuwa wakao kama mawakili walikuwa sita wakiwatete washtakiwa watatu ambapo mshtakiwa wa kwanza Lengai Ole Sabaya alikuwa alitetewa na Dancan Oola na Mosses Mahuna .

Alisema mshtakiwa wa pili Silvester Nyegu alikuwa alitetewa na mawakili Edmond Ngemela na Silvester Kahunduka huku mshtakiwa wa tatu alikuwa alitetewa na wakili Fridorin Gwemelo na Justine Juston na kwamba wamejipanga ndani ya wiki moja kuwasilisha majumisho ya mwenendo wa kesi na kusubiri uamuzi wa mahakama.

Ends..

View attachment 1906195View attachment 1906196
Utashangaa mahakama inamhukumu kifungo cha miaka mitano jela, au kulipa faini ya shilingi laki mbili na nusu!!

Maajabu ya mahakama zetu hayo.
 
Huu utata majina mnh...
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom