Hukumu ya Muuaji ni Kifo ni Dhahiri Hata Usipoadhibiwa

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Kuna watu hutenda uovu mwingi, lakini kwa nafasi zao, hawashtakiwi, na wakishtakiwa, hawaadhibiwa. Kushtakiwa kwao huwa ni njia ya kusafishwa ili warejee kufurahia mema ya nchi.

Lakini ukweli ni kwamba:

1) ukiua, damu ya marehemu ndiyo hukumu yako. Umehukumiwa wewe toka siku ulipofanya mauaji.

2) ukidhulumu, umehukumiwa wewe toka ulipodhulumu.

Ni jambo gumu kulielewa ila waliojaaliwa hekima na kuoneshwa siri za kiimani, wanalijua hilo.

Unaweza kuua, lakini usikamatwe kwa sababu una mamlaka, lakini kama hukumu yako bila ya uovu ile ilikuwa ni kifo, itatekelezwa tu. Kama si kwa mikono ya wanadamu wengine, basi hata kwa mkono wako. Mmesikia, huko Mtwara, Mrakibu wa Polisi aliyekuwa miongoni mwa wauaji wa kijana mfanyabiashara, naye amekufa, kwa kujiua mwenyewe.

Ndugai naye alidhulumu sana haki za watu. Mwishowe amejiadhibu mwenyewe. Aliropoka kwa mdomo wake, akajihukumu mwenyewe kwa kujiuzulu, sasa bado kujiadhibu au kuadhibiwa.

Kuna wengine, Mungu huwaadhibu yeye mwenyewe kwa kupitia matukio mbalimbali.

Huwezi kudhulumu mali au uhai wa watu halafu usihukumiwe. Wengi wa waovu, hasa wenye mamlaka, hukumu zao zipo tangu siku ile walipotenda uovu, kilichobakia ni adhabu.

Watanzania wamejaliwa uoga, unyonge na uvumilivu wa ajabu, ambavyo kwa pamoja vinachukuliwa ni ujinga wa wananchi kutopambania haki zao, lakini ukweli ni kwamba wanachukua hatua, na adhabu kwa watesi wao zinaendelea kutolewa siku hadi siku.

Mmoja kajinyonga, waliobakiwa wataadhibiwa kwa mikono ya nani? Tuendelee kusubiria maana Mungu hakawii bali hutenda kwa wakati ufaao.
 
Kuna watu hutenda uovu mwingi, lakini kwa nafasi zao, hawashtakiwi, na wakishtakiwa, hawaadhibiwa. Kushtakiwa kwao huwa ni njia ya kusafishwa ili warejee kufurahia mema ya nchi...
UKIWAONA DITOPILE MZUZURI alitetewa na dola kwa kuua hadharani ila kalma ilimuondoa akiwa hotelini. Alifia hotelini, alidhani yupo huru kumbe anazunguka na hukumu.

Kikwete alimlinda ditopole sijui kwa nini, mbona SSH hajamlinda Sabaya ! Naomba mungu SSH asiwalinde hao mapolisi awaache wapambane na mahakama wavune walichopanda.

Polisi wanakosa hekima sijui kwa nini !!!
 
Back
Top Bottom