Hukumu ya Lema yazua balaa, imetoa doa katika mhimili huo wa dola. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hukumu ya Lema yazua balaa, imetoa doa katika mhimili huo wa dola.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, Apr 7, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  • MAWAKILI WATEMA CHECHE

  Na Mwandishi wetu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  MAWAKILI wawili wa mjini hapa, wamedai kuwa hukumu iliyomua ubunge Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ilikuwa na dosari nyingi za kisheria na kwamba imetoa doa katika mhimili huo wa dola.


  Wakili Method Kimomogoro aliyemtetea Lema katika kesi hiyo, amezidi kutema cheche safari hii, akidai kuwa hukumu iliyotolewa na Jaji Rwakibarila haikuzingatia hoja muhimu zaidi ya 30 alizoainisha kwenye hati yake ya majumuisho.

  Amesema kuwa jaji katika hali ya kushangaza alitumia ushahidi wa wadai na mashahidi waliothibitika kuwa viongozi na wanachama wa CCM huku akipuuza ushahidi wa upande wa utetezi kwa hoja kuwa mashahidi walikuwa viongozi na wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa na maslahi katika kesi hiyo.


  Alisema kuwa hoja nyingine muhimu ambayo Jaji Rwakibarila hakuizungumzia wala kutolea uamuzi ni ile ya wadai kushindwa kutoa ushahidi mwingine zaidi ya ule wa kusikia ambapo awali walidai wangeleta mahakamani hapo nakala za CD zinazomwonyesha Lema akihutubia na kutoa maneno ya kashfa, udhalilishaji na ubaguzi kidini, lakini hawakuzileta wala hawakutoa sababu za kushindwa kufanya hivyo.


  Kimomogoro alisema hoja nyingine ambayo haikufanyiwa kazi ni ile aliyoieleza mahakamani kuwa ni ushahidi wa kimazingira ulioonyesha kuwa Lema asingeweza kutoa maneno kuonyesha kuwa wanawake hawana uwezo wa kuongoza kwa sababu kwenye timu yake ya kampeni alikuwa akiongozana na wagombea udiwani wanawake ambao aliwanadi na kuwaombea kura.


  Aidha CHADEMA ilisimamisha wagombea udiwani wanawake watatu kwenye kata za jimbo la Arusha Mjini na mgombea ubunge mwanamke katika jimbo la Longido ambalo wenyeji wake ni Wamaasai.


  Kimomogoro alisema kuwa hoja nyingine ni ile ya CCM na mgombea wake Dk. Burian aliyedaiwa kukashfiwa kutolalamika kwenye kamati ya maadili ya jimbo licha ya kupewa fursa hiyo kisheria.


  “Jaji aliacha hoja nyingi bila kuzishughulikia na kuzitolea uamuzi ndiyo maana aliweza kusoma na kumaliza hukumu yake ndani ya saa moja licha ya ukweli kwamba mimi niliwasilisha majumuisho ya kurasa 60, mawakili wa walalamikaji walileta majumuisho yenye kurasa 30 pamoja na maelezo ya mashahidi walikuwa 18 na hoja za mawakili wa serikali ambazo kama angepitia zote ninaamini angetumia muda mrefu zaidi kutoa hukumu yake,” alieleza wakili Kimomogoro.


  Hata hivyo wakili huyo alisema kuwa atakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo wiki ijayo baada ya kupata nakala ya hukumu ambayo inachapishwa kabla ya kujiandaa kukata rufaa.


  Alisema kuwa kutokana na kuwa na nakala ya mwenendo ya kesi waliyokuwa wakipewa kila wiki anaweza kuandaa na kuwasilisha rufaa yake mwisho wa mwezi huu na kulingana na taratibu za kimahakama zilivyo kwa sasa mpaka mwezi Juni maamuzi yatakuwa yamepatikana.


  Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kanda ya Arusha, Shilinde Ngalula, alisema Jaji huyo alitoa uamuzi ambao umeacha shaka kubwa, ikiwa una dhamira ya kweli ya kimahakama au ina mikono ya watu kama inavyolalamikiwa.


  Aliongeza kuwa kwa mujibu wa sheria, Jaji hupaswa kutoa hukumu kwa kusema makosa aliyomtia nayo hatiani mshtakiwa sanjari na kutamka adhabu hivyo kama atakuwa ametumia kifungu 114 cha sheria ya uchaguzi.


  Kifungu hicho kinahusu “Illegal Practice” ambacho kinaangukia kwenye makosa yanayohusiana na vitendo vya rushwa kwa wapiga kura, watendaji wa serikali na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), hivyo alipaswa kutamka wazi kuwa Lema hatagombea ubunge kwa kipindi cha miaka mitano.


  “Hukumu ndiyo inayotamka adhabu; huwezi kuhukumiwa halafu uende kwenye vifungu vya sheria kuanza kuangalia nimetiwa hatiani adhabu yangu inakuwaje, mahakama ndiyo yenye jukumu hilo la kutamka vifungu vya adhabu na si kutamka kutengua matokeo ya uchaguzi na kuacha kutamka vifungu vya kanuni ya adhabu,” alisisitiza mwanasheria huyo.


  Hoja nyingine ambayo inalalamikiwa katika uamuzi huo ni juu ya Lema kutiwa hatiani kwa kosa la kumkashfu aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian, akidai kuwa suala la kashfa hufikishwa mahakamani na yule aliyekashfiwa na si vinginevyo na lithibitike.


  “Kesi za kashfa huwa hazirithiwi ndiyo sababu endapo anayedaiwa kukashfiwa akifariki basi na kesi hiyo huishia hapo,” alifafanua.


  “Kama Lema alitamka maneno hayo na kudhihirika kweli kuwa yalikuwa ya kashfa basi, shauri la kukashfiwa lingefunguliwa na Dk. Burian mwenyewe aliyekashfiwa na si mtu mwingine,” alisema.


  Wakili huyo alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, makosa yote mawili yanaangukia kwenye kifungu cha 108 (II)(a) ambayo humruhusu aliyevuliwa ubunge kugombea kwenye uchaguzi mdogo utakaoitishwa.


  Naye, wakili wa wadai kwenye shauri hilo Modest Akida, aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu kuwa Jaji Rwakibarila alitumia kifungu cha 114 kumtia hatiani Lema lakini hakutamka sheria ya kanuni ya adhabu anayopaswa kuitumikia baada ya kutiwa hatiani.


  Jaji Rwakibarila alimtia Lema kwa kudaiwa kutoa kauli kuwa Dk. Burian si mwaminifu kwenye ndoa yake kwani alikuwa na mtoto aliyezaa nje ya ndoa yake na kwamba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Edward Lowassa.

  Hata hivyo Ngalula alisema kuwa kama ni kweli

  kwenye hukumu hiyo kuna mkanganyiko unaoongelewa unaweza kuondolewa kwa Jaji Rwakibarila kuipitia (review ) na kuifanyia marekebisho au kwa Jaji Mkuu au Mahakama ya Rufaa nchini kuipitia na kuifanyia marekebisho (Revision) ili kuondoa mkanganyiko huo.


  CHADEMA kutoa msimamo leo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, leo anatarajiwa kutoa msimamo wa chama kama kitachukua uamuzi wa kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliyomvua ubunge Lema au la.


  Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Arusha, Ephata Nanyaro, alisema kuwa msimamo huo utatolewa kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya NMC.  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sheria za Serikali yetu Zitatumaliza na kumwaga damu Zetu. Jamani Tutakuwa kama Rwanda? au Kenya?
   
 3. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Watanzania tumisha jua ukweli kuhusu serikali yetu, ni ya visasi na ya kukandamiza haki za watu wake wasio upande wake
   
 4. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amedhalilisha akina mbwenu huyo jaji
   
Loading...