Hukumu ya kifo kwa waandamanaji watatu nchini Iran imethibitishwa na Mahakama Kuu

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,215
7,906
Hukumu ya kifo dhidi ya vijana watatu kwa ushiriki wao katika maandamano ya Novemba 2019 Iran imethibitishwa. Hukumu dhidi ya Amirhossein Moradi, Saeed Tamjidi na Mohammad Rajabi, ambayo ilisimamishwa na Mahakama Kuu ya Iran mnamo Julai 10, 2020 ikihusishwa na kuzidi kwa matumizi ya adhabu ya kifo katika kesi zinazochochewa kisiasa nchini.

"Pamoja na hukumu hizi za kifo zisizokuwa sawa, ni wazi kwamba vijana hao watatu wanatumiwa kama mfano ili kuwatisha watu wengine wasiandamane," alisema Hadi Ghaemi, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha haki za binadamu nchini Iran.
 
Marekani anaua magaidi, hahukumu waandamanaji kunyongwa ili kutisha watu waogope kuandamana
Hao sio magaidi ni Saudi na us backed militant wenye mrengo wa kisunni..
Achana na hiyo fuatilia idadi ya innocent victims waliouawa na Marekani katika Syria na Iraq kwenye harakati zake zA ovyo
 
Bora watiwe kamba tu kuliko kuishangilia nchi yao kuwa Kama Syria..
Hao wote wakisikia vitisho vya US Dhidi ya Iran hushangilia Sana hasa kweñye maandamano Kama Yale..
Sasa unakaaje na jibu litalosababisha Kansa kuu?
Iran ikishabadilishwa kua Kama Iraq, Afghanistan ama Syria wao watakimbilia Washington kupewa ufalme! Tabu kwa Nani?
 
Bora hata hao wameperekwa mahakamani wakahukumiwa kupitia mifumo ya haki kwa mujibu wa sheria zao.
Ebu jitoe ufahamu uandamane ndani ya nchi yako inayo ongozwa na kiongozi wa malaika mtarajiwa tuone kama hata mahakamani utafika ukiwa mzima.
 
Bora watiwe kamba tu kuliko kuishangilia nchi yao kuwa Kama Syria..
Hao wote wakisikia vitisho vya US Dhidi ya Iran hushangilia Sana hasa kweñye maandamano Kama Yale..
Sasa unakaaje na jibu litalosababisha Kansa kuu?
Iran ikishabadilishwa kua Kama Iraq, Afghanistan ama Syria wao watakimbilia Washington kupewa ufalme! Tabu kwa Nani?
Innocent ni hao waliohukumiwa kuuwawa kule iran
 
Hukumu ya kifo dhidi ya vijana watatu kwa ushiriki wao katika maandamano ya Novemba 2019 Iran imethibitishwa. Hukumu dhidi ya Amirhossein Moradi, Saeed Tamjidi na Mohammad Rajabi, ambayo ilisimamishwa na Mahakama Kuu ya Iran mnamo Julai 10, 2020 ikihusishwa na kuzidi kwa matumizi ya adhabu ya kifo katika kesi zinazochochewa kisiasa nchini.

"Pamoja na hukumu hizi za kifo zisizokuwa sawa, ni wazi kwamba vijana hao watatu wanatumiwa kama mfano ili kuwatisha watu wengine wasiandamane," alisema Hadi Ghaemi, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha haki za binadamu nchini Iran.
kwa nini wanawasamehe? Hao ndio wanapelekea machafuko na pia iran inajua fika ni vibaraka toka west, hawa ndio walipelekea Libya iwe hapo, kama mimi ni rais natundika tu, huo ni usaliti ulio wazi,hakuna anayeweza kuvumilia kuishi na msaliti, marekani wenyewe walisema wangemnyonga Snowden, wasaliti ndio walipelekea afrika tukawa watumwa.
 
Kwa sababu analeta habari hizo za kunyongwa watu watatu wakati kuna mifano ya watu zaidi ya 100 kwa day wanauliwa kinyama but anakua haongei, ndio nimempa mfano ili aache unafki, alaf kwa nini tunapotoa mifano halisi ya kinyama anayofanya gaidi marekani mnakua mnakasirika na hali ya kuwa iko wazi??????
Marekani hapa anaingiaje ? Au mimi kuna sehemu sijaelewa kwenye original post?
 
Kwa sababu analeta habari hizo za kunyongwa watu watatu wakati kuna mifano ya watu zaidi ya 100 wanauliwa kinyama but anakua haongei, ndio nimempa mfano ili aache unafki
Lakini habari aliyoileta ni ya kweli au si kweli?
Ngoja nikushauri. Ushabiki wako kwa Iran na chuki yako kwa US unakupeleka pabaya.
Hautaki kusikia habari unajiandaa kwa kushindana. I mean kufanya comparisons.
Jaribu kupunguza.
 
Eeeeee, acha unafki ww, mnakua mnaumia mnapoletewa ukweli humu, hamtaki kuambiwa ukweli, sisi kawaida yetu ni kusema kile kilichopo sasa ww endelea na maumivu yako

Back
Top Bottom