Hukumu ya Kibaka!

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,358
4,304
Kibaka amekamatwa na wananchi wenye hasira, wanampa kisago cha nguvu.

Si unajuwa adhabu ya kibaka mtaani ni kifo ?

Akatokeo Mzito mmoja anayeheshimika mtaani, akaamrisha, "jamani nipeni mimi huyo kijana!"

Wananchi wanalalama , aah,mzeee ! ohh,muheshimiwa, huyu ameiba kuku.

Mzito akasema kwa ukali, nimesema munipe huyo kijana, huku anatoa noti ya elfu kumi ,anasema hii apewe aliyeibiwa kuku wake.
Kijana akanusurika, akaepuka kifo.

Mzito akaingia na kijana kwenye gari yake, akamuuliza kijana anaishi wapi ili ampeleke huko salama , njiani akamwambia

" wewe kijana ,nenda shule, chapa kitabu, ukitoka na elimu yako, utawaibia wale wote, mamilioni na watakuheshimu, watakuita, mzee, mheshimiwa, mkuu."

Mzee akaendelea kumpa shule kijana, si unaona mimi hapa, kazi yangu ni kuzichota tu, wenyewe wamelala, ninawakamatisha elfu,elfu, au tano tano si umeona mwenyewe,

« Adhabu ya kibaka ni kifo/mauti. Adhabu ya mwizi wa mamilioni ni kuitwa , mheshimiwa. »

Alipoona kijana yupo sehemu salama , akampatia elfu 10 , akamwambia asirudie kuiba kuku ila aende shule .

Kijana akatikisa kichwa, hakuamini alichokisikia.

Unaweza kuelewa wapi mambo hayo siyo simulizi za vitabuni, ila ni uhalisia wa maisha ulivyo.

Have a nice day, guys !
 
Message from this? cjaelewa mwenzio.

Mkuu umeingia jukwaa la jokes!

Kuna sehemu duniani, kibaka, au mwizi wa karanga na kuku, hawapelekwi mahakamani, adhabu yao ni kifo, instantly

Lakini kinyume chake ni kuwa kuna watu wanaiba mamilioni,mabilioni . Hawa adhabu yao ni kuitwa waheshimiwa na kuonekana kuwa ni "mungu mtu".

Maajabu ya Bongo hayo.
 
Mkuu umeingia jukwaa la jokes!

Kuna sehemu duniani, kibaka, au mwizi wa karanga na kuku, hawapelekwi mahakamani, adhabu yao ni kifo, instantly

Lakini kinyume chake ni kuwa kuna watu wanaiba mamilioni,mabilioni . Hawa adhabu yao ni kuitwa waheshimiwa na kuonekana kuwa ni "mungu mtu".

Maajabu ya Bongo hayo.

Huyo jamaa sio mtanzania nini? Mbona ni kama anamshangaa docta kuvaa koti jeupe?
 
Back
Top Bottom