Hukumu ya kesi ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums kutolewa tarehe 22 Januari 2020

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
6,453
Points
2,000

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
6,453 2,000
1575636686548.png

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam nchini Tanzania imepanga kutoa hukumu katika kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na mwenzake Micke William Januari 22, 2020.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema leo Ijumaa Desemba 6, 2019 wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa lengo la kupangiwa tarehe ya hukumu.

Awali, Wakili wa Serikali ya Tanzania, Sylvia Mitanto aliieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kusomewa hukumu.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Simba baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashtaka pamoja na ushahidi wa upande wa utetezi uliotolewa na washtakiwa wenyewe.

Melo na Willium wanadaiwa kuzuia Jeshi la Polisi nchini Tanzania kufanya uchunguzi kinyume cha Sheria namba 22 (2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandano Namba 14 ya mwaka 2015.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Aprili Mosi, 2016 na Desemba 13, 2016 katika maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam nchini Tanzania.
 
vipik2

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2011
Messages
1,803
Points
2,000

vipik2

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2011
1,803 2,000
Sasa mbona ilisemwa leo ndio hukumu; hakuna mawasiliano yanayoeleweka? Halafu ikifika Januari 22 itakuwa ni "siku ya kufikiria lini tutoe hukumu"?
Tunaandaliwa kisaikologia kabla ya kutufungia mtandao pendwa, watu watakuwa hawana kosa ila JF itakuwa na makosa ya kufungiwa subiri uone
 
Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
12,709
Points
2,000

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
12,709 2,000
Hakika naamini JF itaibuka kidedea

Kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) inaeleza wazi, nikinukuu "Mtu yeyote yuko huru kutoa maoni yake na kupokea na kutoa habari, kupitia chombo chochote cha habari, bila ya kujali mipaka ya nchi na mawasiliano hayo hayataingiliwa kati na chombo chochote kile" mwisho wa kunukuu

Naamini ingawa mkuu wa malaika aliweka wazi kuwa atawatuma malaika wake waje waifungie JF, lakini kwa uwezo na utukufu wa Mungu hataweza!

Watashindana lakini hawatashinda
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
32,949
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
32,949 2,000
Sasa mbona ilisemwa leo ndio hukumu; hakuna mawasiliano yanayoeleweka? Halafu ikifika Januari 22 itakuwa ni "siku ya kufikiria lini tutoe hukumu"?
It's true, the info given is sketchy, watu tumejitokeza mahakamani Kisutu, kumbe imepangiwa tarehe nyingine. Kwenye mass mobilization, updates should have been within minutes. Unapoacha shughuli zako to join forces kuonyesha solidarity for the just cause, halafu unakuta nothing, unakuwa a bit frustrated.

Let's wait for 22nd January, 2020.
P
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,848
Points
2,000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,848 2,000
Sa
It's true, the info given is sketchy, watu tumejitokeza mahakamani Kisutu, kumbe imepangiwa tarehe nyingine. Kwenye mass mobilization, updates should have been within minutes. Unapoacha shughuli zako to join forces kuonyesha solidarity for the just cause, halafu unakuta nothing, unakuwa a bit frustrated.

Let's wait for 22nd January, 2020.
P
Sasa ni kwamba hawakuwa na taarifa sahihi kuhusu siku ya hukumu au kuna mtu amechanganya mambo; maana wengine tunatumia ushawishi wetu wote to have this case dismissed with prejudice...
 
Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
49,274
Points
2,000

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
49,274 2,000
Mwaka 1956, Senator John Fitzgerald Kennedy wakati huo (baadaye alienda kuwa rais wa Marekani), aliandika kitabu kilichoenda kupata tuzo ya Pulitzer.

Kitabu hicho kinaitwa "Profiles in Courage: Decisive Moments in the Lives of Celebrated Americans".

Kitabu kinaongelea ma Seneta wa Marekani wanane walioonesha ushujaa wa hali ya juu, na kuamua kusimamia kanuni za haki hata pale kusimamia kanuni hizo kulipowaponza kisiasa na kijamii.

Ni kitabu kizuri sana, huwa natamani sana viongozi wetu waweze kuwa na ushujaa kama huu.

Nikifikiria kwetu Tanzania, tukija kuandika historia ya kipindi hiki, haya mambo mengine ambayo wengine tunayaona ya kawaida tu, yanaweza kupewa uzito sana, na kina Max na Mike wakaibuka kuwa "Profiles in Courage" zetu.

One.
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Messages
5,233
Points
2,000

Nanye Go

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2018
5,233 2,000
Sa

Sasa ni kwamba hawakuwa na taarifa sahihi kuhusu siku ya hukumu au kuna mtu amechanganya mambo; maana wengine tunatumia ushawishi wetu wote to have this case dismissed with prejudice...
Hahaha unachekesha ushawishi gani unaoutumia kesi iwe dismissed?!
Kumuhonga akimu Simba ?!
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Messages
5,233
Points
2,000

Nanye Go

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2018
5,233 2,000
Niliuliza, Jamuhuri ikishinda kuna madhara gani kwa JF na wamiliki wake?!

Kufungwa au faini au vyote?!

Je, JF itafungwa au itakosa haki ya privacy ya mamber wake tu?

JF itatoa notice kwa member wake tujitoe au itatuondoa na kuufunga mtandao kwa usalama wetu?!
 
Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Messages
4,316
Points
2,000

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2012
4,316 2,000
It's true, the info given is sketchy, watu tumejitokeza mahakamani Kisutu, kumbe imepangiwa tarehe nyingine. Kwenye mass mobilization, updates should have been within minutes. Unapoacha shughuli zako to join forces kuonyesha solidarity for the just cause, halafu unakuta nothing, unakuwa a bit frustrated.

Let's wait for 22nd January, 2020.
P
P
Kwa utawala huu wa 'homeboy' wako, Mahakama hazina uhuru wa kufanya maamuzi sahihi kulingana na sheria!

Hakimu Thomas Simba ana maelekezo maalumu toka juu ya kuhakikisha JF inafutika na kusahaulika come 2020!
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
32,949
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
32,949 2,000
Mzalendo2015,
Mkuu Mzalendo, kwanza nakubaliana na wewe kuna mazingira fulani, mahakama ziko kama zinapokea maelekezo, ila ni kwenye kasi za wanasiasa, mfano Lema, Sugu, Lijualikali etc, lakini jamiiforums japo hawaitaji lakini wanajua inawasaidia sana serikali kuliko hata inavyowasaidia wananchi. Ni jf pekee ndio inayotoa mrejesho wa jamii kwa serikali. Feedback ni kitu muhimu sana kwa watawala wowote.
P
 
Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Messages
4,316
Points
2,000

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2012
4,316 2,000
It's true, the info given is sketchy, watu tumejitokeza mahakamani Kisutu, kumbe imepangiwa tarehe nyingine. Kwenye mass mobilization, updates should have been within minutes. Unapoacha shughuli zako to join forces kuonyesha solidarity for the just cause, halafu unakuta nothing, unakuwa a bit frustrated.

Let's wait for 22nd January, 2020.
P
P
Kwa utawala huu wa 'homeboy' wako, Mahakama hazina uhuru wa kufanyd maamuzi sahihi kulingana na sheria!

Hakimu Thomas Simba ana maelekezo maalamu toka juu ya kuhakikisha JF inafutika na kusahaulika come 2020
 
Forum statistics

Threads 1,382,133
Members 526,283
Posts 33,820,283
Top