Hukumu ya kesi namba 456 ya 2016 inayowakabili Wakurugenzi wa Jamii Media iliyokuwa itolewe leo, imeahirishwa kwa mara ya 5

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
IMG_20200402_122333_464.jpg

Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Mike William) ambapo Kampuni ya Oilcom iliandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar imeahirishwa tena leo Aprili 02, 2020 hadi Aprili 08, 2020.

Hukumu hii awali ilipangwa kutolewa Novemba 26, 2019 ikapangwa tena kutolewa Disemba 06, 2019 na baadae ikapangwa kutolewa Januari 22, 2020 na kisha ikapangwa Februari 19, 2020 kutolewa saa 6 mchana ambapo iliahirishwa hadi leo Aprili 02, 2020

Hakimu Simba alitakiwa kutoa hukumu ya Kesi hiyo leo baada ya Upande wa Utetezi kumaliza kujitetea, lakini uamuzi wa hukumu katika kesi hiyo umeshindikana kutolewa kutokana na Hakimu kuomba muda zaidi ili kupitia ‘submissions’ zilizotolewa

Hakimu Simba amesema Submission zilizotolewa zimenukuu kesi nyingine nyingi ambazo pia na zenyewe zimenukuu kesi nyingine. Hivyo ili kuitendea haki kesi hiyo ameomba muda zaidi

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 08, 2020 ambapo ndio anatarajiwa kuja kutoa hukumu

Katika kesi hiyo iliyoanza tangu Desemba 2016, Washtakiwa wanatuhumiwa kukataa kutoa ushirikiano kwa Polisi kwa kutowasilisha taarifa za aliyeandika katika mtandao wa JamiiForums kuhusu Kampuni ya OilCom ikidaiwa kukwepa kulipa kodi na kuchakachua mafuta kwenye bandari ya Dar

Taarifa walizozitaka za Mtu aliyeandika hayo zilikuwa ni IP Address, Majina yake Halisi, Namba zake za simu na mada nyingine zote alizowahi kuandika katika mtandao huo wa JamiiForums

Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums - JamiiForums
 
Katika kitu kinachonishangaza ni tabia ya wana JF walioko Dar kushindwa kuhamashishana kuhudhuria kwenye kesi hiyo. Hivi mnajua kesi hiyo inahusu kuwalinda na matumizi ya majina bandia na faragha yenu ya kutumia JF kwa uhuru?
 
Back
Top Bottom