Hukumu ya kesi kupinga ubunge Sumbawanga mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hukumu ya kesi kupinga ubunge Sumbawanga mjini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ptz, Mar 14, 2012.

 1. P

  Ptz JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 466
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Kesi ya uchaguzi ya kupinga kutangazwa kwa ndg Aeshi Hiraly CCM kuwa mbunge wa Sumbawanga mjini leo mashahidi wa pande zote mbili wamehitimisha kutoa ushahidi wao mbele ya jaji wa mahakama kuu mh Jaji`Bethuel Mpakani Kasefu Mmilla “J.4”(Judge incharge mahakama kuu Mbeya). Kesi hiyo inasikilizwa katika mahakama kuu mjini Sumbawanga, ambapo hoja za msingi zilizokuwa zikisikilizwa ni, moja, mchakato mzima wa uchaguzi kugubikwa na rushwa iliokuwa ukitolewa na mgombea wa CCM na pili ni uchakachuzi wa matokeo uliopelekea kutangazwa kwa bw Aeshi. Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na bw Noberth Yamsebo aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA (mlalamikaji) anayetetewa na wakili mmoja toka mbeya na upande wa washitakiwa unatetewa na mawakili wanne. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa rasmi tangu tarehe 27/03/2012 na leo tarehe 14/03/2012 ndio mashahidi wote wamemaliza kutoa ushahidi wao, upande wa mlalamikaji ulikuwa na mashahidi 25 na upande washitakiwa ulikuwa na mashahidi wanne tu ambao wawili kati yao “ bw Vitusi Silago mchambuzi wa mifumo manispaa ya Sumbawanga na bi Silvia Siriwa aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa na msimamizi mkuu wa uchaguzi wa jimbo la sumbawanga mjini” (kwa sasa yuko halmashauri ya wilaya ya Ileje kama mkurugenzi) ndo wamefunga pazia la mashahidi. Vielelezo mbalimbali vilitolewa upande wa mlalamikaji na mashahidi kama ushahidi kuihakikishia mahakama kutilia manani hoja za msingi za kesi hii, moja kati ya vielelezo hivyo ni fomu mbalimbali zilizotumika kujaza, kujumlishia na kutangazia matokeo ya ubunge ambazo zilitumiwa kuchakachulia matokeo, mashahidi upande wa mlalamikaji walitoa ushahidi wao dhidi ya mgombea wa CCM ukiwepo wa kununuliwa pombe, kununuliwa baiskeli, kupewa fedha cash, ununuzi wa shahada za kupigia kura, ununuzi wa vinanda “keyboard” kwa ajili ya kwaya za makanisa mbalimbali na kuwa vyote hivyo vilitolewa kwa mashariti ya kumpigia kura mgombea wa CCM bw Aeshi. Leo mara baada ya wakili mojawapo toka wa upande washitakiwa kuiambia mahakama kuwa mashahidi toka upande wake wameisha, alisimama wakili upande wa mlalamikaji na kuomba kuwa kwakuwa kesi inaelekea mwisho basi itolewe fursa kuandaliwa majumuisho ya kesi, hoja iliyoungwa mkono na upande wa mshitakiwa, hatimaye katika kuitekeleza hoja hii, upande wa walalamikaji waliihakikishia mahakama kuu kuwasilisha majumuisho yao tarehe 26/03/2012 na washitakiwa wakaahidi kupeleka tarehe 10/04/2012, na mwisho kabisa mh jaji Bethuel Mpakani Kasefu Mmilla akahitimisha mjadala kwa kusema kuwa hukumu ya kesi hii itakuwa tarehe 30/04/2012, na ndo ukawa mwisho wa shughuli za leo kuhusiana na kesi hiyo ya uchaguzi wa Sumbawanga mjini. Katika hatua nyingine, waandishi wa habari walioko Sumbawanga na mkoa wa Rukwa kwa ujumla wamekuwa wakilalamikiwa kwa kutekwa na bw Aesh kwa kutoripoti matukio mbalimbali yanayotokea katika mwendelezo wa kesi hii tangu ianze kwani kwa kiasi kikubwa kumekuwa kukitolewa ushahidi ambao kwa kiasi kikubwa ni udhalilishaji wa bw Aeshi, moja kati ya viongozi waandamizi wa klub ya waandishi wa habari mkoa wa Rukwa alipoulizwa kuhusu hili alijibu kwa madaha kuwa “waandishi tunaangalia matukio yenye maslahi” na kusema kuwa hawajaahidiwa chochote na yeyote na kuwa wao wansubiria hukumu. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI SUMBAWANGA ILI HAKI ITENDEKE. AMINA. Nikiripoti moja kwa moja toka mahakama kuu kanda ya Sumbawanga ni mimi PTZ wa JF.
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Sikukujua hii kitu kabisa kama kuinakesi inaendelea huko.
   
 3. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  asante.
   
 4. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu Ptz, ahsante kwa taarifa, ila unaweza edit tarehe (mwaka) nadhani kuna makosa ya typing
   
 5. P

  PUNJE JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  ..mbona nimeota vibaya kuhusu kesi itakavokwisha? nimeota; majumuisho yatakayotolewa na walalamikaji (26.3.2012; mapema kabla ya walalamikiwa) watapewa washitakiwa iliyatumike kuandaa majumuisho yao; ikiwa walalamikaji wakijua yapo salama katika mikono salama. baada ya walalamikiwa kuwasilisha majumuisho ndipo jaji atatumia majumuisho hayo kuisaidia CCM kushinda kesi. Ni ndoto tuu Lakini.; kwani si ndivy taratibu zinavyosema kisheria?
   
 6. D

  DOMA JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Bravo cdm bravo Yamsebo lakini mtangazaji Joshua joel ndio gamba kwelikweli hivyo hawezi kulipoti
   
 7. m

  muntivukaniki New Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bravo PTZ. tuhabarishe zaidi brother, Je, Majumuisho yameshafanyika? na je upande wa Mlalamikaji ndugu YAMSEBO wameshawasilisha? Tutegemee nini brother? Hao waandishi wa Sumbawanga - Choka mbaya, na wate wamewekwa mfukoni.
   
 8. L

  Lsk Senior Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viva CHADEMA,chama changu.....viva YAMSEBO,mwalimu wangu!!
   
 9. P

  Ptz JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 466
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Yaah! Chadema tayari walisha peleka majunuisho yao kama ilivyoamuliwa na mahakama kwa tar 26 Machi. Imani yangu ni ileile kuwa iwapo judgement itakuwa fair kwa kesi hii Chadema wataibuka kidedea! kinachonishangaza ni kuwa hukumu imepelekwa mbali sana kwani ushahidi ulifungwa tar 13/Machi na hukumu ikatangazwa tar 30/ April. Hafu kuhusu waandishi wa habari, ni kweli wote wamewekwa mfukono, na baadhi yao ni makada wakubwa wa ccm, mfano, Yupo Ndg KISIKA yeye ni reporter wa RFA na afsa uhusiano wa Manispaa ya Sumbawanga na hivyo ile Sumbawanga Tv yeye ndo msimamizi mkuu lakini la kushangaza huwaweka ccm tu kwani ni mjimbe wa UVCCM mkoa wa Rukwa
   
 10. G

  Gibbs Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!!!!
   
 11. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  magamba kwa mbinu sijui,
   
 12. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tuombe mungu haki itendeke na ionekane kama imetendeka katika kesi hii
   
 13. wa tarime tanzania

  wa tarime tanzania Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 13
  Itafahamika tu,mwaka wao magamba ,wamebinywa kidogo arumeru sizani kama watakubari tena
   
 14. J

  Jacob Joachim Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini iwe hivyo? Iweje hao wa CCM waruhusiwe kukaa mda mrefu namna hiyo baada ya majumuisho ya Chadema? Kama Chadema ikishindwa rufani na iwe suluhishwa kwani ni dhahiri kwamba Mahakama kuu upo mchezo mchafu! Viva Chadema.
   
 15. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Tjiandae tena kwa uchaguzi mwingine mdogo hapa, Lusinde andaa matusi mapya kamanda wa chipukizi wa ccm
   
 16. A

  Acidic rain Member

  #16
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ngome nyingine ya CDM ni Swanga mjini naomba viongozi wa chama muwe makini na ngome hii tuichukue rasmi. Enditaaaaa
   
 17. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  summarize bana!
   
 18. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kesi ya uchaguzi ya kupinga kutangazwa kwa ndg Aeshi Hiraly CCM kuwa mbunge wa Sumbawanga mjini leo mashahidi wa pande zote mbili wamehitimisha kutoa ushahidi wao mbele ya jaji wa mahakama kuu mh Jaji`Bethuel Mpakani Kasefu Mmilla "J.4"(Judge incharge mahakama kuu Mbeya).

  Kesi hiyo inasikilizwa katika mahakama kuu mjini Sumbawanga, ambapo hoja za msingi zilizokuwa zikisikilizwa ni, moja, mchakato mzima wa uchaguzi kugubikwa na rushwa iliokuwa ukitolewa na mgombea wa CCM na pili ni uchakachuzi wa matokeo uliopelekea kutangazwa kwa bw Aeshi.


  Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na bw Noberth Yamsebo aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA (mlalamikaji) anayetetewa na wakili mmoja toka mbeya na upande wa washitakiwa unatetewa na mawakili wanne. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa rasmi tangu tarehe 27/03/2012 na leo tarehe 14/03/2012 ndio mashahidi wote wamemaliza kutoa ushahidi wao, upande wa mlalamikaji ulikuwa na mashahidi 25 na upande washitakiwa ulikuwa na mashahidi wanne tu ambao wawili kati yao " bw Vitusi Silago mchambuzi wa mifumo manispaa ya Sumbawanga na bi Silvia Siriwa aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa na msimamizi mkuu wa uchaguzi wa jimbo la sumbawanga mjini" (kwa sasa yuko halmashauri ya wilaya ya Ileje kama mkurugenzi) ndo wamefunga pazia la mashahidi.

  Vielelezo mbalimbali vilitolewa upande wa mlalamikaji na mashahidi kama ushahidi kuihakikishia mahakama kutilia manani hoja za msingi za kesi hii, moja kati ya vielelezo hivyo ni fomu mbalimbali zilizotumika kujaza, kujumlishia na kutangazia matokeo ya ubunge ambazo zilitumiwa kuchakachulia matokeo, mashahidi upande wa mlalamikaji walitoa ushahidi wao dhidi ya mgombea wa CCM ukiwepo wa kununuliwa pombe, kununuliwa baiskeli, kupewa fedha cash, ununuzi wa shahada za kupigia kura, ununuzi wa vinanda "keyboard" kwa ajili ya kwaya za makanisa mbalimbali na kuwa vyote hivyo vilitolewa kwa mashariti ya kumpigia kura mgombea wa CCM bw Aeshi.

  Leo mara baada ya wakili mojawapo toka wa upande washitakiwa kuiambia mahakama kuwa mashahidi toka upande wake wameisha, alisimama wakili upande wa mlalamikaji na kuomba kuwa kwakuwa kesi inaelekea mwisho basi itolewe fursa kuandaliwa majumuisho ya kesi, hoja iliyoungwa mkono na upande wa mshitakiwa, hatimaye katika kuitekeleza hoja hii, upande wa walalamikaji waliihakikishia mahakama kuu kuwasilisha majumuisho yao tarehe 26/03/2012 na washitakiwa wakaahidi kupeleka tarehe 10/04/2012, na mwisho kabisa mh jaji Bethuel Mpakani Kasefu Mmilla akahitimisha mjadala kwa kusema kuwa hukumu ya kesi hii itakuwa tarehe 30/04/2012, na ndo ukawa mwisho wa shughuli za leo kuhusiana na kesi hiyo ya uchaguzi wa Sumbawanga mjini.

  Katika hatua nyingine, waandishi wa habari walioko Sumbawanga na mkoa wa Rukwa kwa ujumla wamekuwa wakilalamikiwa kwa kutekwa na bw Aesh kwa kutoripoti matukio mbalimbali yanayotokea katika mwendelezo wa kesi hii tangu ianze kwani kwa kiasi kikubwa kumekuwa kukitolewa ushahidi ambao kwa kiasi kikubwa ni udhalilishaji wa bw Aeshi, moja kati ya viongozi waandamizi wa klub ya waandishi wa habari mkoa wa Rukwa alipoulizwa kuhusu hili alijibu kwa madaha kuwa "waandishi tunaangalia matukio yenye maslahi" na kusema kuwa hawajaahidiwa chochote na yeyote na kuwa wao wansubiria hukumu.


  MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI SUMBAWANGA ILI HAKI ITENDEKE. AMINA. Nikiripoti moja kwa moja toka mahakama kuu kanda ya Sumbawanga ni mimi PTZ wa JF.​


   
 19. simaye

  simaye JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hapa sumbawanga mjini hakuna waandishi wa habari kabisa na kama wapo basi wanaandika habari za kujitugia nazile wanazopewa na viongozi wa ssm kwa kutpewa posho na kubebwa kwenye magari ya chama. Hawana utamaduni wa kutafuta habari.Yapo matukio mengi ya vipongozi kukandamiza wananchi na kutowajibika vema lakini sijawahi kusikia wanafuatwa na kuhojiwa ili taarifa zifike kwa wananchi na watanzani wenzao wajue wenzao wa Rukwa wanashida zipi. Zaidi sasa hivi kuna sumbawanga tv ambayo Kisika anawachukua ccm na kuweka vipindi vya ovyo badala ya kukusanya wanancihi kueleza kero zao na kuwafikishia viongozi na nafikiri sababu ni u uvccm wa Juma Kisika.Kesi AESHY anaweza kutupwa nje hakimu akiwa fair!
   
 20. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280

  Acha utani bana. Sisiem hawawezi kumtumia tena mtu huyu.
   
Loading...