Hukumu ya ICC yamtaja Rostam Aziz mmiliki wa Dowans!

Wana JF,

Kwa hili la DOWANS damu lazima itamwagika na itawakumba na wasio husika kwanini serikali siwaweke wahusika hadharani kwa hili?? Kwanini Dowans iwe kizungumkuti mpaka leo ni miaka mingapi sasa mpaka leo. Dawa ya hawa ni kutowachagua tena na wasitegemee kurudi tena.
 
All these primary impulses, not easily described in words, are the springs of man's actions.
 
Watu mnaandika hapa kwa kumung'unya mung'unya. Watu hao wanaotajwa kuhusika kwa namna yoyote ile na hiyo DOWANS ni Rostam Aziz, Edward Lowassa, Nimrod Mkono na mwingine ni huyo ***** aliyebwagwa kwenye ubunge last year kule Mwanza L. Masha.
Ndiyo nimewataja, sasa kafungueni kesi mahakamani kwa kuchafuliwa majina. Mnanuka UFISADI mtupu.
 
Duh;
Watanzania tunahitaji Uzatiti ktk hili,

ni Lazima tushupae.

Wageni washaifanya Tanzania kama shamba la bibi.

Viva Sitta japo kwa hili.:whoo:
 
Hivi wale akina Shimbo na yule mwingine aliyejitaja kuwa ni Assistant wa usalama wako wapi? Hiki ndicho kipindi cha wao kufanya kazi. Au hizi pesa zimekwenda kwenye uchaguzi? inabidi tujue. Hila halipwi mtu hapa. Rostamu ametajwa saana hivi kwa nini? Je ndiye kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wa Tanzania? Richmond waliiba lakini hapa sidhani.
 
bunge lina uwezo zaidi ya huo.. hata ku-impeach the president, lakini yote hayo yanategemea spika wa wabunge na vichwa vyao

naskia makinda tayari keshaanza kuweka zengwe kuhusu hioja binafsi

Kwa wabunge hawa ambao 2/3 yao wamewekwa kwa nguvu ya mafisadi,hawawezi kuwageuka mabwana wakubwa wao hata iweje..
 
Hivi wale akina Shimbo na yule mwingine aliyejitaja kuwa ni Assistant wa usalama wako wapi? Hiki ndicho kipindi cha wao kufanya kazi. Au hizi pesa zimekwenda kwenye uchaguzi? inabidi tujue. Hila halipwi mtu hapa. Rostamu ametajwa saana hivi kwa nini? Je ndiye kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wa Tanzania? Richmond waliiba lakini hapa sidhani.

Kwani haya malipo yanahusu wapinzani? manake huko ndiko ungewaskia wamesimamia vidole lakini kwakuwa ni wale wale wanapiga kimya..
 
Mimi naposhindwa kuelewa ni kwamba inawezekanaje Dowans kushinda case ambayo mkataba wake kisheria ulikua batili, kwa mimi navyofahamu ni kwamba mkataba wa Richmond (ambayo baadae ikakabidhi kazi kwa Dowans) na Tanesco ulikuwa batili na ni dhahiri Richmond walikiuka vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba huo (kutosambaza umeme kwa wakati) hivyo kisheria hii ni sababu moja ya kuvunja mkataba, sasa swali linakuja je serekali waliingia mkataba mpya na Dowans? kama Dowans walirithi mkataba uleule wa Richmond (ambao ni batili ''null and void'') inawezekanaje wakadai fidia na hatimaye kushinda case?
inamaana wakili wa Tanesco amelipwa pesa zote hizo lakini akashindwa ku-raise issues hizi? na kama alizi-raise issues hizi majibu ni yapi?
 
Utamsumbua tu Pinda alishasema ni bora kumtoa roho kuliko kuzungumzia vitu kama hivyo, yeye hana habari anajiandaa kwenda shambani.

12_10_6jywre.jpg

hata sox havai?
 
please jamani watanzania tuache tabia zakutofuatili mambo kwa usahihi wake,huyu mwandishi anatakiwa kutaja kile hukumu inachozungumza na nani anatajwa katika hukumu hiyo,sio swala la kutuambia mbunge,tuna wabunge wengi sio lazima awe rostam.riport ya richimond inasema mmiliki wa kampuni hizi hajulikani ni kampuni za kitapeli,hivi mpaka kampuni inashinda kesi mahakamani bado mmiliki wake ni jambo la kuendelea kuhisi?tuache tabia za uzandiki wa kutumiwa vibaya na wanasiasa mfilisi.nyie waandishi wa habari andikeni vitu kamili na sahihi,sio kutaka kuuza magazeti yenu tu,nasi jf hoja zisizo na kichwa wala miguu hatuna sababu ya kuzizarau na kuwambia wawasilishaji wale fulldata za habari zao.​
NAMCHUKIA SAAANA rostam aziz, lakini tusisahau KULIKONI ni gazeti linalomilikiwa na REGINALD MENGI. na sote twajua ugomvi kati ya MENGIna ROSTAM AZIZ.
Tusije tukawa twaendeshwa kama magari mabovu kumbe kinachoendelea ni vita vya biashara?????!!!!!!!!!!!!
 
Mbona MwanaHalisi iliwahi kuibandika "list of shame" kama ilivyo wandugu? Tuseme siku hizi "wameshajirudi?"

buchanan....... LIST of shame wallibandika kama ilivyo kwa sababu walikuwa wamenukuu toka mkutano wa hadhara,, kisheria hakuna tatizo
 
Hivi wale akina Shimbo na yule mwingine aliyejitaja kuwa ni Assistant wa usalama wako wapi? Hiki ndicho kipindi cha wao kufanya kazi. Au hizi pesa zimekwenda kwenye uchaguzi? inabidi tujue. Hila halipwi mtu hapa. Rostamu ametajwa saana hivi kwa nini? Je ndiye kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wa Tanzania? Richmond waliiba lakini hapa sidhani.

Hivi unaamini kuwa nchi hii kuna usalama wa taifa? Hapa kuna UFISADI WA TAIFA.
 
watanganyika, ni heri kufa tukiipigania nchi yetu kuliko kukaa kimya huku tukinyanyaswa na mafisadi KWANINI TUSIINGIE VITANI? tena itakua vita nzuri sana. Peoples power vs mafisadi. Natoa hoja

hapa umenena mkuu, bila ya kutwangana hapa tutaendelea kuumizana mpaka tukome, tukipiga kura wanaiba na mafisadi wanaendelea kuiba rasilimali za nchi tu kwa sababu hatuna cha kufanya..tutwangane tuu...leteni vita kudadadeki!!
 
ICC orders Tanesco pay Dowans Tsh185bln
In a landmark judgment, the International Commercial Court of Arbitration in November ordered Tanzania’s Electricity Supply Company (TANESCO) to pay Dowans USD 24,168, 343 equivalents to Tsh 185Bln for breach of contract. The ruling brought a new twist and sparked more controversy to the alleged emergence electricity power supply corruption case which has rocked the country for the past four years.

The case arises from the botched purchase of emergence power supply from Richmond LLC. A parliamentary investigation revealed that the emergence power supply contract was concluded in dubious and scandalous way. Richmond had no capacity to supply power and high ranking government officials were suspiciously involved in flouting tender procedures in favour of Richmond LLC. The parliamentary report recommended government terminates its contract with Richmond and all key government officials (including the Prime Minister Mr Eward Lowassa) to resign from public office. Facing criticism, Richmond LLC sold its assets to Dowans Tanzania Ltd

The government later terminated its contract with Dowans and stopped it from selling its equipment before the matter was resolved. Aggrieved by government’s decision, Dowans filed a case at the International court of Arbitration claiming breach of contract. The ICC ordered TANESCO to pay the money with an additional 7.5% interest amounting to USD 19, 995, 626. Dowans is satisfied with this ruling but the government and the public is not. Some citizens and activists have described the judgment as a mockery of justice and perpetuation of corruption. Some key government officials have called on the government to ignore the ruling while the Attorney General has asked TANESCO to provide it with all the case files for review and possible appeal against the judgment.



Source: Case data as provided by PCCB Headquarters and other sources
 
Mimi naona suala hili limechukua muda mrefu kulitatua kutokana na kusitasita kwa Serikali kwa sababu zisizoeleweka. Hakuna ubishi kwamba Richmond ilitutapeli kwa kuleta mitambo isiyokidhi viwango tilivyolipia. Kampuni yenyewe ime-prove ni feki huko Merikani.

Pili, Dowans imethibitishwa na Mwarabu (Mwana Mfalme = Prince) aliyetajwa kuwa ndiye mwenye hisa kwamba ni feki. Hata huko Costa Rica kunakodaiwa mmiliki mwingine yupo, Serikali ya nchi hiyo imethibitisha taarifa hiyo ni ya uongo. Kwa hiyo hii Dowans ni feki pia.

Kwa hiyo bila hata kuwahusisha hawa vigogo Wabunge na Wanasheria wa hapa kwetu, wanaotajwa na Kubenea na Samwel Sitta, napendekeza Serikali ichukue hatua ya kutaifisha hii kampuni ya Dowans kwa kupitisha Sheria Bungeni kwa tukitumia nguvu yetu ya Sovereignty. Tutamke katika hiyo sheria kwamba hatutalipa fidia kwa atayejitokeza kwamba ni mmiliki wa Dowans. Sababu ya kutolipa fidia ni kwamba TANESCO wameshawalipa vya kutosha hawa mafisadi.








Usalama wetu ni kufanya jitihada ya kukataa juhudi zote za kulipa.
PENDEKEZO;DOWANS IBINAFSISHWE HARAKA.
Atakayejitokeza kuwa ni mmiliki sasa ashitakiwe haraka. Alijificha kipindi cha Richmond! Huyo RA aliwahi kusema kuwa anamfahamu mmiliki wa DOWANs!. Wizi wa kijinga hasa!!!
 
Tanesco ililia na Rostam











Rostam(5).jpg

Rostam Aziz




Taarifa sasa zimevuja juu ya aina ya utetezi ya uliowasilishwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kwenye kesi dhidi ya Dowans Tanzania Limited katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC), ambako imeamriwa kulipa mabilioni ya shilingi kwa kuvunja mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura.
Katika utetezi wake ambao NIPASHE imeuona, Tanesco mbali ya kujenga hoja mbalimbali, iliamua kulia na Mbunge wa Igunga, ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, kuwa ndiye hasa Dowans.
Tanesco katika utetezi wake ilidai kuwa Dowans haijasajiliwa Costa Rica kama ilivyodai, ila mradi ni unaomilikiwa au kuendeshwa au kuhusishwa na Rostam.
Tanesco pia ilishuku barua za utambulisho wa Dowans, moja ikiwa imeandikiwa Desemba 8, 2006 na nyingine Desemba 18, 2006, zikiitambulisha kama kampuni yenye hadhi na ikiwa inatambuliwa na walau benki mbili maarufu duniani, ikiwamo Royal Bank ya Canada na CRDB ya Tanzania.
Utetezi huo wa Tanesco pamoja na mwingine, vilitupiliwa mbali na ICC na hivyo kuipa ushindi Dowans katika shauri hili ambalo liliwasilishwa kwake baada ya kuvunjwa kwa mkataba iliourithi kutoka Richmond Development Corporation.
Katika kesi hiyo, Tanesco imeamrishwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 94.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, juzi aliwaambia waandishi wa habari kuwa kiwango kinachotakiwa kulipwa kwa Dowans ni Dola za Marekani 63,812,630 sawa na Sh. Bilioni 94 na si Sh. Bilioni 185 kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa na vyombo vya habari.
Katika hukumu ya ICC pia utetezi mwingine wa Tanesco ulijiegemeza kwenye ubatili wa kubadili mkataba wa Richmond kwenda Dowans kwamba ulikiuka sheria.

Source: Nipashe Jumapili (IPPMedia) 01-09-2011 Jumapili
 
Back
Top Bottom