Hukumu ya Babu Seya & Sons hii hapa.

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Nimelazimika kutafuta nakala ya hukumu ya Babu Seya na Wanae iliyotolewa leo hii na mahakama ya rufaa, naomba wanaJF wote tuisome between the lines ili tuelewe kilichopelekea wengine kuachiwa na wengine kutoka na from there sasa labda ndio tuanze mjadala kuliko kufanya speculations zisizo na majibu..

Karibuni..
 
Hapa nimeweka maaamzi ambayo ni likely kukutana nayo mahakamani
 

Attachments

  • This is what is likely to happen when you go to court.doc
    35 KB · Views: 121
Nilishasema mimi niko upande wa watoto waliharibiwa na huyu mshenzi wa tabia ...ningekuwa mimi "hastahili" kuishi hata dakika moja damn
 
Hapa nimeweka maaamzi ambayo ni likely kukutana nayo mahakamani
Asante kwa mchango mzuri Ray B...ila sijakupata vema uchambuzi wako umetulia ila nimeshindwa ku-link na hukumu ya kina babu Seya...niweke sawa mkuu!
 
Asante kwa mchango mzuri Ray B...ila sijakupata vema uchambuzi wako umetulia ila nimeshindwa ku-link na hukumu ya kina babu Seya...niweke sawa mkuu!

Kwanza nashukuru kwa appreciation. Well, nilichomaabisha ni kuwa mfumo wa mahakama ni mfumo ambao sisi Binadamu tukiwa na tawala zetu tunaamini ni sehemu ambayo hali inatendeka lakini ukweli unabaki pale pale katika yoyote ile mwenye ukweli ni mshtakiwa mwenyewe.

Nasema hivi kwa sababu kama umeshawahi kuhudhuri mahakamani au kushiriki katika udadavuzi wa kesi yoyote utagundua kuwa kinachofanyika ni mawakili kuoyesha uwezo wao kisheria na namna wanavoweza kuchezea maneno na kupindisha/kukwamisha hoja ya upande pinzani.

Hapo ndipo unapopata kuna wanaoadhibiwa kihalali na kimakosa. Na kuachiwa huru vile vile iko kwa mtindo huu. Kwahiyo kama wanasheria wanavokwambia (burden of proof lies to the defendant) wakimaanisha jukumu la kujikwamua analo mshtakiwa. Hii ni kusema kuwa kama wewe una makosa kweli lakini ukawa ni mjuvi au ukawa na wajuvi wa sheria, kufikiri na utaalamu wa kupindisha hoja za mashtaka basi unaweza ukatoka bila kupewa adhabu ya aina yoyote ile au wakikosea kidgo ukapewa adhabu ambayo hukulingana nayo (yaani ni ndogo kuliko uliyostahiki). Na vivyo hivyo kama huna makosa unaweza kupewa adhabu kwa kukosa hizi qualities na mbinu za kimahakama/Sheria.

Lakini bila ya kusahau mwisho wa yote, katika utawala ambao mahakama inaweza ikaendeshwa na wenye nguvu kisiasa au kifedha napo tegemea maamuzi mengi ambayo ni tofauti na ule Ukweli niliousema Awali Ambao Aliyenao ni Mshtakiwa
.
 
Back
Top Bottom