Wanabodi hukumu inayowakabili viongozi wa CHADEMA mkoa wa Dodoma itasomwa kesho katika mahakama kuu kanda ya Dodoma kuanzia saa mbili asubuhi.Kesi hiyo inawahusu katibu wa CHADEMA mkoa wa DODOMA mh.Masawe,Mratibu wa wanawake wa CHADEMA mkoa wa Dodoma Mh.Kunti Yusuph na Mjumbe wa baraza la vijana mkoa wa Dodoma ndugu Edward.Watu hawa kwa pamoja wanatuhumiwa kwa kosa la kufanya mkutano wa hadhara katika wilaya ya bahi pasipo kuwa na kibali cha polisi.Nitawajuza kitakachotokea kesho mahakamani.Kwa wafuasi wote wa CHADEMA walioko Dodoma mnaombwa kuhudhuria mahakamani kwa ajili ya kusikiliza hukumu hiyo.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI CHADEMA.