Hukumu ndogo kesi ya Sabaya kusomwa Januari 14, 2022

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mahakama ya hakimu mkazi Arusha inatarajiwa kutoa uamuzi mdogo januari 14, mwaka huu wa kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya{34} na wenzake sita kama ana kesi ya kujibu au laa .

Hayo yalisemwa na Hakimu Mkazi wa Mhakama hiyo,Patricia Kisinda baada ya Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa serikali,Janeth Sekule kufunga ushahidi na kueleza kuwa wamefunga ushahidi baada ya kulidhika na ushahidi wa mashahidi 13 na vielelezo 8 vilivyowasilishwa mbele ya mahakama hiyo na upande wa Jamhuri kuwa vinaweza kuwatia hatia watuhumiwa wote saba katika kesi hiyo.

Sekule alidai na kumweleza Hakimu Kisinda kuwa upande wa Jamhuri umefunga ushahidi kwa kuwa wanaamini kuwa ushahidi wa mashahidi 13 na vielelezo nane vinatosha kuwatia hatiani washitakiwa katika kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi,Rushwa na kutumia vibaya madaraka na utakatishaji fedha haramu.

Baada ya kauli hiyo,Hakimu Kisinda alihairisha kesi hiyo hadi Januari 14 mwaka huu ndipo atatoa uamuzi mdogo kama watuhumiwa hao wanakesi ya kujibu au la kwa mujibu wa sheria.

Mbali ya Sabaya washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na Enock Mnkeni{41) ,Watson Mwahomange {27} maarufu kwa jina la Malingumu, John Aweyo(45),Syliverster Nyengu{26} maarufu kwa jina la Kicheche ambaye pia Ni Msaidizi wa Sabaya,Jackson Macha{29} na Nathan Msuya{31}.

Katika kesi hiyo Sabaya alikuwa akitetewa na Mawakili,Mosses Mahuna na Faudhia Mustapher,Mawakili Silvester Kahunduka na Fridolini Bwemelo walikuwa wakiwatetea washitakiwa wa pili Enock Mnkeni na wa tatu Watson Mwahomange wakati mshitakiwa wane John Aweyo,Mshitakiwa wa tano Silvester Nyegu,mshitakiwa wa sita Jackson Macha na Nathan Msuya walikuwa wakitetewa na wakili Edmund Ngemela.

Waendesha Mashitaka wa serikali waliokuwa wakiongoza kesi hiyo ni pamoja na Waendesha Mashitaka Waandamizi Felix Kwetukia,Tasilia Asenga,Othmed Mtenga,Janeth Sekule na Mwendesha Mashitaka Neema Mbwana.

Katika kesi hiyo Sabaya na wenzake wanakabiliwa na Mashitaka matano ikiwemo shitaka la la kwanza la Uhujumu Uchumi linalowakabili washtakiwa wote ilidaiwa kuwa Sabaya akiwa Mtumishi wa Umma yeye na wenzake Januaria 20 mwaka huu ndani ya Jiji la Arusha na Mkoa wa Arusha akiwa na genge lake la Uhalifu alilokuwa akiliongoza katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro akijua wazi kuwa ni Mkuu wa wilaya alitumia vibaya madaraka yake wakati akijua wazi kuifanya hivyo ni kosa kisheria.

Shitaka la pili lililokuwa likimkabili Sabaya mwenyewe ilidaiwa kuwa kuwa Januari 20 mwaka huu ndani ya Jiji la Arusha na Mkoa wa Arusha akiwa Mtumishi wa Umma alishiriki kushawishi Rushwa ya shilingi milioni 90 kutoka kwa Mfanyabiashara Maarufu wa Jijini Arusha,Francis Mrosso mkazi wa kwa Mrombo ili aweze kumsadia katika kesi ya jinai ya ukwepaji kodi iliyokuwa ikimkabili wakati akijua wazi kufanya hivyo ni kosa kisheria akiwa mtumishi wa Umma.

Shitaka la tatu lililokuwa likimkabili Sabaya ilidaiwa kuwa januari 20 mwaka huu ndani ya Jiji la Arusha na Mkoa wa Arusha aliomba Rushwa ya shilingi milioni 90 kutoka kwa Mrosso mkazi wa Kwa Mrombo Jijini Arusha ili aweze kumsaidia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya ukwepaji kodi iliyokuwa ikimkabili Mfanyabiashara huyo wakati akijua wazi kufanya hivyo ni kosa kisheria akiwa mtumishi wa Umma katika Wilaya ya Hai.

Shitaka la nne la Utakatishaji fedha haramu lililokuwa likiwakabili washtakiwa wote saba kuwa januari 20 mwaka huu ndani ya Jiji la Arusha na Mkoa walichukua fedha shilingi milioni 90 za Mrosso na kwenda kuzifanyia matumizi yasiyokuwa halali kinyume na sheria ya utakatishaji fedha.

Mwisho

images%20(17).jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom