buswelu moja
JF-Expert Member
- Aug 24, 2014
- 226
- 147
MAHAKAMA ya hakimu mkazi Arusha leo imehairisha kusoma hukumu ya kesi iliyofunguliwa na mkuu wa wilaya mstaafu nchini,Dahn Makanga dhidi ya Mathew Mollel ambaye ni mkazi wa jijini Arusha.
Hukumu ya kesi hiyo ilikuwa inatarajiwa kusomwa leo mnamo Novemba 14 mwaka huu na hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Gwantwa Mwankuga baada ya upande wa mashtaka na utetezi kufunga ushahidi wao.
Akitangaza kuharisha kusoma hukumu hiyo hakimu Gantwa alisema kwamba amehairisha kusoma hukumu hiyo kutokana na sababu mbalimbali ambazo hakuzitaja hadharani.
Mara baada ya kutangaza uamuzi huo ndipo aliposema ya kwamba amefanya hairisho fupi kutangaza hukumu hivyo na kupanga kuisoma ifikapo Novemba 24 mwaka huu.
MY TAKE:
Haijajulikana mpaka sasa ni kwanini Hakimu Gantwa amehairisha kutangaza hukumu hiyo kwa kuwa hizo sababu hajaziweka hadharani.
Leo mahakamani watu walikuwa wamefurika hakika wengi wakisubiri kusikia hukumu hiyo kwa hamu kwa kuwa kesi hiyo imejizolea umaarufu na kuvuta hisia za watu hapa Arusha kutokana na kwamba mlalamikaji na mlalamikiwa wana nasaba na wameoa nyumba moja kwani mlalamikaji ameoa dada mtu na mlalamikiwa ameoa mdogo mtu.
Tukutane ijumaa ijayo nitawajuza nini kimejiri mahakamani stay tuned