Hukumu inasomwa mbele ya DPP, anatoka nje kuzungumza na waandishi na kueleza watuhumiwa walishaanza kutekeleza hukumu kabla haijasomwa

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Yapo mambo kimfumo yanaleta ukakasi hasa namna serikali inavyoendesha mihimili mingine.

Nimeona DPP akitoka mahakamani Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya Ardhi ambayo kwa mujibu wa hukumu hiyo Jamhuri imeshinda.

Nje ya Mahakama DPP anawaeleza waandishi kwamba watuhumiwa walishaanza kukabidhi baadhi ya nyaraka za ardhi iliyokuwa inabishaniwa.

Najiuliza, kwanini DPP ametoka Dodoma kwenda kusikiliza hukumu ya kesi hii? Je alijua Jamhuri itashinda? Alianzaje kufanya mazungumzo na watuhumiwa kabla ya hukumu? Mahakama imejiongoza au imeongozwa?
 
Hata mimi nimeshangaa sana jamaa walishalipa na laki nne kwa DPP na kukabidhi hati miliki kabla ya hukumu, ndio maana suala la nusrat wa cdm liliwezekana kufanyika kama lilivyofanyika.

Hii nchi kweli sasa haifuati utawala wa Sheria ni hili genge la wauni waliojitangaza washindi wa uchaguzi wanaamua wanavyojisikia.
 
Kwani utaratibu kisheria upo vipi? Au unalalamika bila kuwa na knowledge? Utaratibu ni mtu kutiwa hatiani halafu baadae hukumu huwa inafuata. Inawezekana waliambiwa wanahatia ya fulani hivyo kwa uungwana wao wakaanza kurespond.
 
Back
Top Bottom