Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 973
Wakati tukiendelea kuomboleza vifo vya Watanzania wenzetu waliotutoka, ni muda pia wetu sisi wananchi wa Kanda ya Ziwa, ku-revise way back kuangalia namna ambavyo tumekuwa tukisafiri katika Ziwa Victoria. Kampuni ya Huduma za Meli nchini inayomilikiwa na Serikali (MSCL) inamiliki meli kadhaa za abiria katika Ziwa Victoria, zikiwemo: MV Victoria (Bukoba), MV Serengeti (Uzinza), MV Butiama na MV Clarias (Ukerewe).
Tunajua adha ya usalama ilivyo ya muda mrefu. Meli ya mwisho ya abiria kuundwa na Serikali ni MV Serengeti mwaka 1988 na tangu hapo, tumekuwa tukijionea meli ndogo ndogo tu ndizo zikiundwa na watu binafsi licha ya abiria kuongezeka maradufu katika Ziwa Victoria, hali iliyopelekea abiria wanaotumia Meli hizo kubwa kupungua kutoka 903,000 mwaka 2006/2007 hadi 324,000 mwaka 2015/2016.
Hali imekuwa ya kukatisha sana tamaa kipindi cha nyuma. Hata kwa meli hizo chache ambazo MSCL imekuwa ikiziendesha, zimekuwa mbovu na zinazofanyiwa matengenezo ya mara kwa mara, kiasi cha kuleta hisia kuwa zimekuwa zikifanyiwa hujuma na watumishi wa MSCL na hivyo kuzifungulia milango meli za watu binafsi.
Hata hivyo, kwenye tahadhari za kiusalama ni kuwa, mabaharia wa meli za umma na za binafsi wamekuwa wakiwaelekeza abiria wakati wa safari kuwa, usafiri wa meli ni wa salama zaidi na kwamba meli haiwezi kuzama kwa ghafula bali huzama taratibu (husahau kuwa meli pia zinapinduka, kama MV Nyerere). Kwa maelezo yao hayo, huwa wameyafungia maboya (life jackets) kwa makufuli kiasi kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kuyachukua dalili za ajali zikianza mpaka wao watakapoyafungua.
Wenyeji wa Kanda ya Ziwa, wengi wao hujua kuogelea so huwa hawana hofu yoyote kutokana na mazoea ya kusafiri mara kwa mara (japokuwa wanajua kuwa ukizama kwenye maji ya kina kirefu uogeleaji huwa ni mgumu sana kutokana na nguvu ya maji). Shida huwa kwa wageni ambao hata kuangalia ndani ya maji tu pekee huogopa, so wanapoona maboya yamefungwa hukosa amani.
Maboya yakiwa yamefungiwa kwenye lock kwenye MV Nyehunge. Hapa ajali ikitokea, tutatafutana tu.
Vilevile, kutokana na meli za MSCL kuwa mbovu muda mwingi, abiria wanaokwenda Ukerewe hutumia sana meli za watu binafsi hasa Kampuni ya Nyehunge. Hata hivyo, mara nyingine (japo siyo mara zote), meli za Nyehunge zimekuwa zikikatisha tiketi bila kurekodi taarifa za abiria aliyekatiwa tiketi, hali inayoonyesha kuwa, endapo ajali ikitokea, hawawezi kujua akina nani walisafiri zaidi ya kujua idadi ya tiketi walizouza.
Meli mpya ya Nyehunge iliyofunguliwa mwaka 2016. Hii ina maboya mengi. Angalia maboya kule juu.
Wakazi wa Kanda ya Ziwa, wamefurahia sana kitendo cha Serikali kutangaza kuunda meli kubwa ya kwenda Bukoba, pamoja na kukarabati Meli za Victoria (Mwanza-Bukoba)na Butiama (Mwanza-Ukerewe).
Meli inayotajiwa kuundwa na Wakorea kufanya route za Mwanza - Bukoba.
Pamoja na kuishukuru Serikali kwa kuunda meli mpya kubwa na kukarabati MV Victoria na MV Butiama, tunaiomba itengeneze meli nyingine kwa ajili ya Visiwa vidogo vilivyoko Magharibi ya Kisiwa cha Ukerewe katika Tarafa ya Ilangara. Visiwa hivyo, ni: Kamasi, Galinzila, Gana, Bulubi, Izinga na Sizu. Ukerewe ndiyo inayoongoza Tanzania kwa uvuvi wa samaki hasa dagaa, huku zaidi ya nusu ya samani hao wakivuliwa kutoka katika Visiwa hivyo vilivyoko Tarafa ya Ilangara, yenye wakazi wapatao 100,000. Cha ajabu hakuna meli bali boti/mitumbwi tu, wakati ina abiria wengi kama (probably kuzidi) wa Ukara.