Huku tukijivunia ndege zetu, wanafunzi 52,000 hawana madarasa ya kusomea

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
10,526
13,013
Habari za kutwa wanajamvi,

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zatajwa kila siku kwamba uchumi wake unakua kwa kasi. Inatajwa kupiga hatua za maendeleo ikiwemo kupambana na rushwa.

Wakati nchi yetu kupitia kwa wapiga zumari wa mkuu wakijitapa nchi kupiga hatua za maendeleo ikiwemo kununua mindege, kujenga mireli (SGR), kujenga ukuta, vita ya rushwa na elimu bure, hali imekuwa mbaya zaidi katika sekta ya elimu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Elimu TAMISEMI kuna zaidi ya wanafunzi 52,000 nchini pote wamechaguliwa bila kupangiwa shule za kujiunga nazo.

Amesema kukabiliana na tatizo hilo wanaleta mfumo wa double shift kama njia ya zimamoto ya kuondokana na hilo. Hali ni mbaya zaidi mkoani Kigoma.

Aidha imeripotiwa kwamba Shule ya Msingi Nzasa huko Mbagala ina wanafunzi zaidi ya 500 na ina vyumba vya madarasa 22 tu. Hapa ni Nzasa Dar es Salaam sijui huko Nachingwea hali ipoje?

Huku haya yakiendelea Mkurugenzi yule wa Elimu amesema Halmashauri zijenge madarasa kwa mapato ya ndani, alisahau kwamba vyanzo vya mapato ya Halmashauri vimechukuliwa na mchumi mkuu wa taifa na sasa Halmashauri ni vibogoyo, haziwezi kujiendesha.

Wadau wa elimu wanahoji je kati ya maendeleo ya ndege na madarasa ya watoto wa masikini ambao kila siku wanaimbwa majukwaani na ambao wazazi wao hawajui hata njia za kwenda airport kipi kitangulie?

Je, ni kweli elimu bure tu inatosha bila kuboresha miundombinu yake?

Maendeleo ya kweli huwalenga walio wengi, sio ndege, hata mkoloni alileta ndege lakini wengi waliishi kwenye umasikini uliotopea.

Maendeleo bila uhuru ni utumwa

Chanzo cha habari: Azam TV
 
Waafrika tuna matatizo sana. Tunadhani tukivaa suti wakati ndani hatuna hata chupi, tutakuwa tumefanana na wazungu.

Mwafrika anaweza kwenda kununua range rover kwa hela ya mkopo, wakati hata kodi ya nyumba hajalipa. Na baada ya hapo atatamba kuwa amemzidi jirani yake mwenye vitz. Lakini huyo jirani anaishi kwenye nyumba yake, watoto wake wanasoma shule nzuri, na ana akiba nzuri bank.

Tutambue kuwa viongozi wetu ni sehemu ya jamii zetu. Kile kilichopo kwenye jamii, ndicho wanachoenda nacho kwenye uongozi.

Nadhani mmesikia wachina wamegoma kuondolewa kwenye kundi la nchi maskini LAKINI sisi tuliopo kwenye abject poverty, tunasema siyo masikini bali ni matajiri.
 
wanafunzi.jpg
 
Wewe kama mtanzania(mleta mada) unayeguswa na uhaba huu wa madarasa, umetoa mchango gani wa kuhakikisha tatizo hili linatoweka, zaidi ya kuleta uzi kwa kebei juu ya tatizo hili hapa jamvini!?
Kwa hali ya sasa nini kifanyike kuondoa tatizo hili!? Maana umemaliza post yako ya kwanza ya huu uzi kwa malalamiko tu!
 
Wewe kama mtanzania(mleta mada) unayeguswa na uhaba huu wa madarasa, umetoa mchango gani wa kuhakikisha tatizo hili linatoweka, zaidi ya kuleta uzi kwa kebei juu ya tatizo hili hapa jamvini!?
Kwa hali ya sasa nini kifanyike kuondoa tatizo hili!? Maana umemaliza post yako ya kwanza ya huu kwa malalamiko tu!
Swali duni sana ! kwanini usimuulize mnunua ndege ?
 
Back
Top Bottom