Huku tukiikaribisha miaka 60 ya 'Uhuru' Watanzania tumetakiwa Kusalimiana 'Kijapan' kwa Kukunja Ngumi na Kuinama tu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,466
108,621
Nilidhani Viongozi wetu huku kuelekea Kutimiza Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania wangskuwa wanahimiza zaidi 'Utanzania' wetu ila cha Kushangaza sasa Watanzania tunatakiwa Kuiga 'Tamaduni' za Wengine ambazo sina uhakika kama zitaeleweka vyema.

Kuna Mtanzania Mmoja jana akiwa pande za Morocco, Makumbusho na Mwenge alitutaka Watanzania ili kumuepuka Mgeni 'Omicron Variant' aliyeanzia South Africa na sasa yupo Zimbabwe tuwe 'Wajapan' kwa lazima hasa pale tunaposalimiana na tuwe kila tunapokutana tunakunja Mikono yetu Miwili kisha tunabong'oa ( tunainama ) ndipo Stori zetu zingine ziendelee.

Je, mpaka leo tunaenda kutimiza hii miaka 60 Watanzania kama Watanzania ( Waswahili ) hatuna 'Utamaduni' Wetu wa 'Kusalimiana' mpaka tuanze Kuupenda wa 'Kjjapan' ambao naambiwa kwa 'Kijapan' una maana yake Maalum?

Baada ya kutakiwa kusalimiana 'Kijapan' nami kwa hamu sana nasubiria tarehe 9 Disemba 2021 nione kama 'Utamaduni' huu utatumika pale Uhuru Stadium kuanzia kwa aliyeutoa, Watu wa Meza Kuu, Makomandoo na Wananchi kwa Kukunja Mikono yao na Kubong'oa ndipo wakae Vitini.
 
Tuoneshe basi ,namna bora ya kusalimiana Kitanzania ili tujuwe pa kuanzia.

Lakini usije ukatuletea ile ya Kinyachusa ya kupiga magoti!

Au ya kihaya.
 
Back
Top Bottom