Huku si kudanganya umma???

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,944
703
Watanzania wenzangu, kama mnavyojua Tanzania iliondoa kodi kwa mtu yeyote anayeingiza kompyuta nchini. Lakini hata hivyo kuna sheria zilizowekwa kusimamia uchakavu wa vitu vinavyoingizwa Tanzania ili kuzuia nchi yetu kuwa dampo. Nimejaribu kuangalia hii picha kwa makini nimeshindwa kupata la uhakika, ila kwa mtazamo na maoni yangu niliamini kuwa hapa huyu Mbunge Makalla anatania au kuudanganya umma. Naamini hapa atakuwa anatamba kuwa ametoa msaada wa kompyuta, na printa, lakini inaoneka hivi vifaa ni vya zamani. Angalia hata keyboard.....jamani tuacheni kudanganya umma.
Wadau toeni maoni kuhusu hii picha hapa.

2.JPG
 
Hahahahaa da kweli bongo noma, hizo komputer na printer I guess ilikuwa zikawe destroyed yeye akaona dili kuchukua akafaidishe jimboni kwake y.

Hao makatibu kata au walimu they are happy, pengine ndo ya kwanza kijijini.

Kweli we always remain a damping place of european scrapers....more containers are coming stay tuned.
 
Complite hizo zinauzwa elfu hamsi! Cpu,monitor,keyboard,mouse and cables! Nyongeza unapewa printer hp deskjet
 
wizi mtupu...akawadanganye wa vijijini......
Hizi computer kwanza hazizalishwi tena... Keyboard ndo baaasi kabisa ni afadhali angewapa typewriters
 
Prof. Maghembe ameshawah kupeleka Laptop mbili mbovu shule flan ya Kata jimboni kwake. Shule yenyewe ilikuwa haina umeme. Aliitisha mkutano wa kata, akagawa laptop. Wazazi walifurahi sana. Nadhani alziokota.
 
buy a Hp monitor and CPU @ 75,000 Tsh get a printer for free..... nadhani muhishiwa (mh) kaiutilize offer ya maduka ya used computers kariakoo,
 
Ukipiga hesabu ya huo msaada hata laki moja na nusu ni wasi wasi kufika thamani yake.

Lakini posho za waandishi wa habari bahasha ni nyingi kuliko msaada wenyewe.

Jamaa ana tafuta umaarufu kwa kila dizaini
 
Watanzania wenzangu, kama mnavyojua Tanzania iliondoa kodi kwa mtu yeyote anayeingiza kompyuta nchini. Lakini hata hivyo kuna sheria zilizowekwa kusimamia uchakavu wa vitu vinavyoingizwa Tanzania ili kuzuia nchi yetu kuwa dampo. Nimejaribu kuangalia hii picha kwa makini nimeshindwa kupata la uhakika, ila kwa mtazamo na maoni yangu niliamini kuwa hapa huyu Mbunge Makalla anatania au kuudanganya umma. Naamini hapa atakuwa anatamba kuwa ametoa msaada wa kompyuta, na printa, lakini inaoneka hivi vifaa ni vya zamani. Angalia hata keyboard.....jamani tuacheni kudanganya umma.
Wadau toeni maoni kuhusu hii picha hapa.

2.JPG
[/QUOTEMbona singewaachia hilo VX??
 
Gharama ya kuchoma mafuta kwa hilo VX kutoka maduka ya wasomali wauzaji wa kompyuta chakavu pale kariakoo mpaka jimboni kwake mvomero ni kubwa kuliko gharama ya msaada aliotoa...kwa kutaka publicity akawaita na wana habari kabisa...ni kweli msaaada hauna udogo lakini vitu vingine bora usaidie mkono wa kulia na mkono wa kushoto usijue,vinginevyo ni kama utapeli na udanganyifu tu.
 
Sometimes ni vizuri kuliangalia jambo kama lilivo na usiende beyond.... Umeona Mazingira ilipopelekwa ni dhahiri kua hio comp labda ndo mwanzo... Hata wakipeleka Mackintosh hapo inakua haina maana, bora nyiingi kwa bei nafuu... Mradi ziwe na ubora...
 
Kitendo cha kutoa kompyuta inabidi kipongezwe na kwa hapa sasa tunaanza kuhoji PC iliyotolewa ni ya namna gani? picha inatuonesha kuwa hili ni toleo la zamani sana na tena si mpya/ ni chakavu sana. Wabunge wa aina hii hutumia ujinga wetu kujipatia umaarufu
 
Ni bora huyu aliyekumbuka jimboni kwao kuliko wale hata kuja kuwatembelea wapiga kura wao ni issu ila next time aangalie vitu vinavyokwenda na wakati
 
Gharama ya kuchoma mafuta kwa hilo VX kutoka maduka ya wasomali wauzaji wa kompyuta chakavu pale kariakoo mpaka jimboni kwake mvomero ni kubwa kuliko gharama ya msaada aliotoa...kwa kutaka publicity akawaita na wana habari kabisa...ni kweli msaaada hauna udogo lakini vitu vingine bora usaidie mkono wa kulia na mkono wa kushoto usijue,vinginevyo ni kama utapeli na udanganyifu tu.

Ilikuwa na ulazima kuita waandishi wa habari?
 
Sisi wa Sikonge, kijana Said "Hitler" Nkumba aligawa pesa ili MSONDO NGOMA wanunue Kinanda.

Wakati huo kwa sasa hapa Sikonge, mwaka huu njaa kali sana na watu hawana chakula.

Heri huyo walau kapeleka hilo kopo kuliko sisi kumpa Msondo hiyo pesa ambayo sijui waligawana saa ngapi.

Mbunge Wa Jimbo la Sikonge Tabora Saidi Mkumba akimkabidhi Kiongozi wa Bendi ya Msondo ngoma Saidi Mabera Kitata cha Shilingi Laki Tatu kwa ajili ya bendi.
 
Duh nashindwa kupata uhalisia na gharama z akuandaa hicho kitu
Ila tusilaumu sana huenda ni ya kwanza hapo alipoenda kugawa tusilaumu sana
 
Angalia hilo jengo lenyewe linaonekana hata umeme hakuna.Sasa sijui Computer itatumika kama kuonyesha mfano iliwanafunzi wajue computer inavyofanana au ni mapambo katika ofisi ya mwl.Mkuu?KAZI KWELI KWELI KWA HAWA WANASIASA WETU.Si ajabu shule hiyo kuna watu bado wanakaa chini.Kwa nini asiwape madawati?
 
Mkuu hizo alizonunulia hizo used comp hazitoshi hata nadawati mawili sasa ya nini ajipe stress bure
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom