Huku ni kuzidishiana umasikini-Bidhaa Feki

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,749
Kama kuna kitu ambacho serikali imeshindwa ni hili suala la kuharibu bidhaa au bunduki zinazokusanywa,mpaka sasa sijauona utajiri wa Tanzania kufanya hivyo,hizi ni fedha za mlala hoi aliesafiri na kwenda mbali kununua kitu ambacho ni rahisi na kukileta nyumbani kukiuza,labda kuna watu watasema wanatuletea bidhaa zisizofikia kiwango cha kimataifa,kwa kweli Tanzania sio nchi pekee inayozungukwa na biashara ya bidhaa za aina hii hata huko nchi zilizo ulimwengu wa kwanza bidhaa za aina hii zipo na zinauzwa na kutumiwa na wateja.
Hivi watu wanaohusika katika kuzuia bidhaa hizi ,ukiwauliza Mtanzania mwanakijiji ataweza kuinunua TV SONNY madein Japan,Camera Madein Japan Radio Madein Japan ,maana wanaoishi huko maulaya ukiwauliza au kuwaagizia kitu made in Japan atakuona unamtafutia mambo asiyokuwa na uwezo nayo na mnaweza kutoandikiana barua na ikawa mwisho wa mawasiliano.
Naona iko haja ya kutoa au kuweka mkoa au mtaa ambao utakuwa unauza bidhaa feki ni mtu na hiari yake kununua origino au feki,jamani kila mtu na uwezo wake,kuna nchi fulani ukienda na ukifika airport kuna kijarida kinachohusu Nchi ilivyo humo utaelezwa kila kitu na kuna sehemu imeandikwa ikiwa unataka kununua kifaa original basi ni mitaa ya upande fulani ila upande mwengine utaambiwa huko bidhaa ni mchanganyiko na hata kwenye maduka ya vifaa vya magari utaona umewekewa kibao au maandishi yanayokwambia kwamba hapa tunauza vifaa genuine.
Naamini kabisa haya mambo lazima yatakuwa na mkono wa binadamu mwenye choyo na wanaohujumiwa hawana pa kulalamikia ,huko maulaya unaweza pia kununua kitu Original na ukifungua ndani ukaona vijisehemu vyengine vinatoka nchi mbali mbali na vingi utaviona vinatoka China.
Sasa suali lipo hapa hivi hawa wanaoleta vifaa ambavyo ni USED mfano wa hizo hizo redio ,pc na TV monitors pamoja na LapTop unafikiri hawa wanauza nini kama sio vitu ambavyo vimebakiza muda kidogo tu kutoweza kutmika au kufanyiwa repair na huko nchi vinakotoka wanapata nafuu vitu kama hivi vikisafirishwa na kuletwa kuuzwa Tanzania kwa mtazamo wangu wamelifanya kama jaa na vingi ya vitu hivi vikiharibika ndio mwisho,kuna kama hizi laptop ambazo power ya LCD yake ni miaka mitatu na ikimaliza inaanza kuwa na trail na kupoteza nguvu yake,halikadhalika maredio na matv Chipset zake ni balaa kubwa kushinda mifuko ya rambo ambayo viongozi wasiojua la kufanya na kumletea Mtanzania maendeleo wamepata pa kuegemea kama walivyo kwa maradhi ya ukimwi kiongozi au waziri atajiona ameleta maendeleo makubwa akiusemea ukimwi hawa ni viongozi wasio jua kazi za kuwa kiongozi au wasio jua kazi zao
Kama kuzuia basi wangezuia hizi bidhaa za electronic ambazo ni used na wala sio recondition.
Kwa kweli Mwanakijiji wa Tanzania bado anahitaji matumizi ya bidhaa feki ikiwa tuna viongozi feki sioni sababu ya kuzuia bidhaa za aina hii.
Bidhaa hizi na ufeki wake basi bado zina kiwango sawa na bidhaa original na hutokea zikaishi kwa muda mrefu kuliko hizo za bei mbaya ambazo Mtanzania wa kijini hata auze ngombe kumi bado hajaweza kuinunua.
Pia kuna ule mtindo wa kuchoma silaha zilizosalimishwa naona hapa napo panahitaji elimu ili silaha hizi badala ya kuchomwa moto zinaweza kutumika katika kutoa mafunzo katika kambi za jeshi au mgambo na hata polisi wenyewe wanaweza kuzitumia kuliko kuzichoma moto.
Kuna haja ya kutafuta ni fisadi gani alievalia njuga jambo hili haswa la bidhaa feki,mbona jamani hiki ni kitu cha kawaida hawa bila ya shaka wameona na kulinganisha na wauza software ipo kazi kweli kweli.
Kwa mfano badala ya kuziharibu kwa nini wasitumie akili ya kupeleka kwenye mashule au ofisi za serikali vituo vya polisi ,shule za nasari yaani hata wangeziuza kwa bei poa katika nyanja hizo ,jamani hata mahospitali wanaweza kuweka tv na kideo yake mwanakijiji hatakosa kitu hapo huku anasubiri kuitwa na daktari aliekwenda sokoni au kujiliwaza baada ya kazi ya jembe na kupalilia kuliko kusaga saga na kuchoma moto moto unasababisha umasikini. Tunatupa nguvu za Mtanzania aliekwenda mbali.
103450.jpg
 
Back
Top Bottom