Huku ni kuwaumiza wananchi wenye uchumi wa chini, Hayati Magufuli alipambana na matajiri ili wenye hali tete tupumue

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,210
12,913
Mh Rais Samia hichi ulichotuletea cha ada ya ya kizalendo hatuitaki.

Huku ni kuwaumiza wananchi wenye uchumi wa chini maana ndiyo watumiaji wakubwa wa hizi huduma ulizotuongezea! Mwenzio alipambana na matajiri ili wananchi wenye hali tete tupumue lakini wewe unakuja kutubana sisi ili wao wapumue?

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema Serikali iliyofail inapambana na wananchi wa hali chini inalinda matajiri waneemeke zaidi sasa naona nawewe umeenza kufail tena mapema sana.

Sasa hatutapeleka hela zetu bank wala kuweka kwenye mitandao! Tutakaanazo ndani.

20210714_201631.jpg
 
Kwa kweli CCM imeshindwa kuongoza nchi mnakata kodi bila sababu mnang'ang'ania serikali ichangiwe iyo sio sawa.
 

Kila tatizo lina chanzo chake, tatizo lilianzia mbali sana.

Je, mlilikemea? Jibu ni hapana!

CCM ni ile ile..

Hivi MATAGA nao wanaimba acha waisome namba au wao tozo uchwara ya kizalendo wanakubaliana nayo?
 
Dunia ya sasa unapopandisha makodi kwenye mawasiliano na mafuta umeua uchumi kabisa.

Sasa hivi watu wataanza kutembea na hela wakati wao wanatusisitiza tuwe tunafanya electronic transactions ili kupunguza gharama za uchapishaji fedha alafu wapandisha makodi hapohapo kama sio upuuzi ni nini sasa?

Mnataka bidhaa zianze kupanda bei?

Uchumi wa Rais Samia utakuwa mgumu kuwahi kutokea.
 
Serikali siku zote hubebeshwa lawama. Lakini hiyo hiyo huwa haikosi mabavu ya kujilinda.

Kule SA maandamano ni kwa sababu lipo kundi kubwa la wasio na kazi, watu milioni 12 na zaidi na kingine ni aina zao za siasa.

Wamewazoesha dezo raia wao, rand 350 kwa kaya sasa zikikosekana hao hao raia wanaigeuka serikali yao.

Sisi ni waelewa na wastaarabu na uzuri ni kwamba matunda ya kodi huwa tunayaona kila siku.
 
Kama hujipendi au huipendi familia yako sogeza kidevu chako barabarani utanyolewe ndevu zako kwa chupa.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema Serikali iliyofail inapambana na wananchi wa hali chini inalinda matajiri waneemeke zaidi sasa naona nawewe umeenza kufail tena mapema sana.
Walikuwepo na wala hawakumuelewa, isitoshe hawana muda wa kutafakari yanayotokea, ushirikishwaji haupo tena, ni watu kadhaa wenye personal interest wanakaa na maswahiba wao wanapanga wanachotaka kiwe, "who is behind this evil move"
 
Ni hivi, ameamua kucheza kama Barca, anatukabia kwenye eneo letu la goli na akipata mpira anapiga shots on target tu kaanza na nishati ya mafuta ili kufanya movement iwe ngumu, na alivyomaliza hapo kapandisha gharama za mawasiliano na miamala ya simu.

Either way utakapokimbilia lazima akunase tu, kiufupi ni kwamba hajatufokea lakini katufokea.
 
kama hujipendi au huipendi familia yako sogeza kidevu chako barabarani utanyolewe ndevu zako kwa chupa.
Nchi hii bado hakuna wa kuandamana.

Kila mtu bado anapenda ugali kuku, mixer Macoron na soup ya ng'ombe.

Wapi wapinleo kina Azory, Ben Saanane kila mtu ameshasahau na maisha yanaendelea.

Wanasiasa ndio kabisa wako busy na mambo yanayowapa faida wao.
 
Kodi hii imepitishwa na BUNGE letu tukufu, wabunge walio chaguliwa kihalali ambao wamewakilisha mawazo ya watanzania wote kwa manufaa ya watanzania wote, kodi hii lazima tuilipe, wapuuzi wachache wasitusumbue wala wasituharibie malengo yetu kama hawataki waende wakaishi Ubeligiji.
 
kodi hii imepitishwa na BUNGE letu tukufu, wabunge walio chaguliwa kihalali ambao wamewakilisha mawazo ya watanzania wote kwa manufaa ya watanzania wote, kodi hii lazima tuilipe, wapuuzi wachache wasitusumbue wala wasituharibie malengo yetu kama hawataki waende wakaishi ubeligiji.
Hakuna Bunge pale kuna vilaza walioingizwa kwa ajili ya kumuandalia mwendazake utawala wa milele ni vile tu Corona ime intercept hii move haramu na ya kishetani.
 
Mh Rais Samia hichi ulichotuletea cha ada ya ya kizalendo hatuitaki.

Huku ni kuwaumiza wananchi wenye uchumi wa chini maana ndiyo watumiaji wakubwa wa hizi huduma ulizotuongezea! Mwenzio alipambana na matajiri ili wananchi wenye hali tete tupumue lakini wewe unakuja kutubana sisi ili wao wapumue?

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema Serikali iliyofail inapambana na wananchi wa hali chini inalinda matajiri waneemeke zaidi sasa naona nawewe umeenza kufail tena mapema sana.

Sasa hatutapeleka hela zetu bank wala kuweka kwenye mitandao! Tutakaanazo ndani.

View attachment 1854493
Huyo aliye waaminisha kwamba matajiri ndio waendeshe nchi huku nyie mnaonjiita wanyonge mkiendelea kuzaliana kama simbilisi wakati huo huo mnahitaji maji safi, hospitali ma daktari na dawa , walimu na madarasa umeme nk. Barabara nzuri nk. Huyo ndiye aliye watia ujinga vichwani mwenu na ndio maana hao matajiri unao waongelea wewe walianza kuikimbia nchi na kuhamisha biashara zao maana mzigo ulikuwa unawaelemea sasa sijui baada ya hapo kingefuata nini? Bora mungu alitenda.

Msiwe wajinga nyie eti kisa mliaminishwa na mtu aliye kuwa na mawazo finyu kuhusu utajiri, matajiri sio wakosaji wala maadui wa nchi bali ni wananchi kama wewe walio pambana kutafuta pesa, na hawakutajirika ili wawahudumie nyie mlio itwa wanyonge enzio hizo hivyo acheni ujinga.
 
Back
Top Bottom