Mbelwa Germano
JF-Expert Member
- May 7, 2011
- 789
- 289
Ukosefu wa ubunifu katika kuibua vyanzo vya mapato na udhibiti wake katika uendeshaji miradi ya maendeleo umewafanya viongozi na watendaji wa serikali ya CCM wilaya ya Lushoto wajishirikiana na madiwani wao kuendelea kuwanyonga wananchi wakiwamo walimu kwa kuwalazimisha kuchangia Tshs.20,000 kwa ajili ya ujenzi wa maabara za shule za sekondari.Wananchi hawa pamoja na kuchangia pesa taslimu wanalazimishwa kuchangia nguvu kazi.
Pamoja na ukweli kwamba moja ya jukumu la serikali ikiwemo halmashauri za wilaya ni kukusanya kodi na kutoa huduma kwa wananchi jambo hili ni tofauti chini ya utawala wa CCM kwa kuwabambikia migizo ya mateso wananchi wake kutokana na ukosefu wa ubunifu katika kubuni na kudhibiti vyanzo vya mapato.
Serikali hii sikivu ya CCM inatoa misamaha mikubwa ya kodi,inashuhudia ukwepaji mkubwa wa kodi,rushwa na ufisadi na inaruhusu wananchi waliowengi kunyonywa kwa ajili ya utukufu wa watu wachache.
Ieleweke kwamba pamoja na walimu kuwa na makato ya kodi ya mapato,bima ya afya,hifadhi ya mifuko ya jamii n.k. kutoka kwenye mishahara yao bado wanabebeshwa mzigo huu wa mateso pamoja na kufanya kazi katika mazingira magumu.
Hoja hapa si kupinga ujenzi wa maabara bali uchakato na maamuzi yasiyozingatia hali halisi ya maisha ya watanzania masikini,serikali kusahau mantiki ya ukusanyaji kodi kwa ajili ya maendeleo ya watu na mwisho ukosefu wa ubunifu na udhibiti wa mapato na matumizi ya fedha za umma.
Mbelwa Germano
(Lushoto Constituent)