Huku ndiko tulikofika, TBC chombo cha UMMA hakirushi hotuba za mgombea Urais, Mh. Tundu Antiphas Lissu lakini kinatumika kurusha matusi ya Polepole!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Huko ndiko CCM imetufikisha kama taifa. TBC chombo kikubwa cha UMMA kinatumika kuwatukana Watanzania wanaopinga utawala wa kibabe usiozingatia sheria wala Katiba.

Badala yake TBC chombo kinachowafikia wananchi walio wengi kinatumika kusifia uvunjaji wa wazi wa kanuni na sheria tulizojiwekea na kuwatukana wapinzani.

Kwa hakika inashangaza, inasikitisha, inaudhi na inakasirisha.
 
Kiufupi wanaita matumizi mabaya ya madaraka,
Mimi natarajia kesho polepole aitwe kwa mroto kwa kuendesha uchochezi
Na si hivyo tu, katika hii kampeni ya kugombea Urais, Polepole anapewa nafasi ya kuongea TBC kama nani? Kuna mambo mengine tunayapuuzia sisi kama wananchi lakini yana athari kubwa kwa taifa. Kesho na kesho kutwa unaweza kukuta na UVCCM nayo ikipewa nafasi TBC kuwatukana wapinzani wa CCM na sisi wananchi tukachukukia poa tu...hivi Watanzania tukoje?
 
Huko ndiko CCM imetufikisha kama taifa. TBC chombo kikubwa cha UMMA kinatumika kuwatukana Watanzania wanaopinga utawala wa kibabe usiozingatia sheria wala Katiba. Badala yake TBC chombo kinachowafikia wananchi walio wengi kinatumika kusifia uvunjaji wa wazi wa kanuni na sheria tulizojiwekea na kuwatukana wapinzani...kwa hakika inashangaza, inasikitisha, inaudhi na inakasirisha.
Una memory nzuri sana sio Chadema waliowafukuza TBC siku ya kwanza ya kampeni na kupewa muda wa dakika 10? Aibu ya mwaka kujisahaulisha.
 
Elewa sababu ya kufukuzwa, na ndo maana TBC walirudi wakaomba msamaha
 
Una memory nzuri sana sio Chadema waliowafukuza TBC siku ya kwanza ya kampeni na kupewa muda wa dakika 10? Aibu ya mwaka kujisahaulisha.
Kwa hiyo TBC inajibu mapigo kwa kutoa nafasi kwa Polepole amtukane mgombea wa Urais Mh. Tundu Antiphas Lissu? TBC inayoendeshwa kwa kodi za wananchi wote bila kujali ni wa chama gani inatii maagizo ya mgombea wa CCM aliyeapa kutopeleka maendeleo kwa wananchi wanaochagua upinzani ingawa kodi wanalipa? Na wewe Ole unaona sawa tu.
 
Huo usemi una maana kwamba wasimamizi wa kweli wa maendeleo yao ni wale wa chama chake kwa sababu hao wengine hata kwenye bajeti ya mwaka huu wa pesa walikimbia Bungeni. Sasa sijui hata huu uchaguzi ungefanyikaje. Think ouside of the box.
 
Ole, Ole, Ole ...je unajua kwa nini CCM kwa sasa inazidi kuchukiwa? Ni kwa sababu ya majibu ya kifedhuli na ya kipumbavu kama hili ulilolitoa hapa...hebu msikilize na huyu hapa chini;

Unawakejeli na kuwafokea wananchi wako waliokumbwa na matatizo ukiyaita natural disaster wakati huo huo uko tayari kuwapa msaada raia wa taifa jingine kwa matatizo hayo hayo uliyoyaita natural disaster, je upo?
 
  • Dislike
Reactions: Ole
Huko ndiko CCM imetufikisha kama taifa. TBC chombo kikubwa cha UMMA kinatumika kuwatukana Watanzania wanaopinga utawala wa kibabe usiozingatia sheria wala Katiba. Badala yake TBC chombo kinachowafikia wananchi walio wengi kinatumika kusifia uvunjaji wa wazi wa kanuni na sheria tulizojiwekea na kuwatukana wapinzani...kwa hakika inashangaza, inasikitisha, inaudhi na inakasirisha.
Kwani CCM iliwafukuza kwenye kampeni zao?. Mkarushe kwenye Tanzania daima, gazeti la mwenyekiti wenu mwenye chama chake. Ruzuku zote mnazobeba mnapeleka kwa saccos, mtakula wa chuya safari hii.
 
Ole, Ole, Ole ...je unajua kwa nini CCM kwa sasa inazidi kuchukiwa? Ni kwa sababu ya majibu ya kifedhuli na ya kipumbavu kama hili ulilolitoa hapa...hebu msikilize na huyu hapa chini;

View attachment 1582888
Unawakejeli na kuwatukana wananchi wako waliokumbwa na matatizo ukiyaita natural disaster wakati huoo huo unawapa msaada raia wa taifa jingine kwa matatizo hayo hayo unayoyaita natural disaster, je upo?
Kwani kuna ubaya gani kwenye maneno hayo? Vile vile Serikali ilitoa msaada baada ya hapo . Hizi propaganda hazitawasaidia kupata kura ndio uongo ambao tunasema hauna tija.

Nchi zote za soutern afrika tumezisaidia sana hasa wakati wa mwlimu Nyerere itakuwa sasa. hata wao huwa wanatusaidia kama una kumbukubu nzuri wakati rais alikuwa mwinyi alpewa forex na Zimbabwe vile vile South Afrika. Wewe kwa sababu hujui unapayuka tu. mchango wa Tanzania kusini mwa afrika unatambuliwa duniani kote sisi ndio kama baba.
 
Huko ndiko CCM imetufikisha kama taifa. TBC chombo kikubwa cha UMMA kinatumika kuwatukana Watanzania wanaopinga utawala wa kibabe usiozingatia sheria wala Katiba. Badala yake TBC chombo kinachowafikia wananchi walio wengi kinatumika kusifia uvunjaji wa wazi wa kanuni na sheria tulizojiwekea na kuwatukana wapinzani...kwa hakika inashangaza, inasikitisha, inaudhi na inakasirisha.
Si mliwafukuza kwenye mkutano wenu Mbagala au mmesahau tena?
 
Kilichorushwa na TBC hata sheria za vyombo vya habari vinakatazwa. TBC imetia aibu sana kwa kweli.
 
Huko ndiko CCM imetufikisha kama taifa. TBC chombo kikubwa cha UMMA kinatumika kuwatukana Watanzania wanaopinga utawala wa kibabe usiozingatia sheria wala Katiba. Badala yake TBC chombo kinachowafikia wananchi walio wengi kinatumika kusifia uvunjaji wa wazi wa kanuni na sheria tulizojiwekea na kuwatukana wapinzani...kwa hakika inashangaza, inasikitisha, inaudhi na inakasirisha.
TBC ina weledi wa kutosha.
TBC wako smart, sawa ni chombo Cha Taifa lakini sio kwa ajili ya matusi na kukejeli maendeleo yaliyopo.
Ni upuuzi na uzandiki.
 
Kwani kuna ubaya gani kwenye maneno hayo? Vile vile Serikali ilitoa msaada baada ya hapo . Hizi propaganda hazitawasaidia kupata kura ndio uongo ambao tunasema hauna tija.
Serikali ilikula rambi rambi zilizotolewa kwa wahusika na hii si mara ya kwanza serikali hii kuwadhulumu raia wake haki zao. Serikali ya Magufuli inaishi kwa dhuluma na ndio maana safari hii wananchi wanakataa na kusema, hapana, imetosha.
Wewe kwa sababu hujui unapayuka tu. mchango wa Tanzania kusini mwa afrika unatambuliwa duniani kote sisi ndio kama baba.
Ohoo, unajua unaongea na kijana au sio? Mimi naamini naweza kukupa somo la uhuru wa Tanganyika kabla na baada ya uhuru. Usimhusishe baba wa Taifa na ujinga unaoendelea kwa sasa ndani ya taifa letu. Misingi ya Umoja wetu kama Watanzania hivi sasa inapitia majaribu ya kutisha kwa sababu ya utawala ulioasi taratibu, kanuni na sheria kama tulivyojiwekea.
 
  • Dislike
Reactions: Ole
Serikali ilikula rambi rambi zilizotolewa kwa wahusika na hii si mara ya kwanza serikali hii kuwadhulumu raia wake haki zao. Serikali ya Magufuli inaishi kwa dhuluma na ndio maana safari hii wananchi wanakataa na kusema, hapana, imetosha.
Ohoo, unajua unaongea na kijana au sio? Mimi naamini naweza kukupa somo la uhuru wa Tanganyika kabla na baada ya uhuru. Usimhusishe baba wa Taifa na ujinga unaoendelea kwa sasa ndani ya taifa letu. Misingi ya Umoja wetu kama Watanzania hivi sasa inapitia majaribu ya kutisha kwa sababu ya utawala ulioasi taratibu, kanuni na sheria kama tulivyojiwekea.

Serikali ile pesa, are you serious? Huna cha kunifundisha au kuniambia kuhusu Uhuru wa Tanzania/Tanganyika. waongopee ndugu zako wa sacos ya mlevi wa konyagi. Chuki yenu kwa Magufuli haitafanikiwa mlifikiri atashindwa kuongoza na sasa mnaanza visingizio. Give credit where is due.

Kama Rais Magufuli ameweza kukuza pato la taifa kutoka sh trilioni 53 alizoacha Kikwete hadi sh trilioni 120, Mungu atupe nini tena?!
 
Back
Top Bottom