Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,272
Ninaishi Kwa Mtogole, nyumba tunayoishi tuko familia tano, wastani kila familia ina watu watano. Wote tunatumia choo kimoja. Mlango wa chooni ni gunia.
Mimi ninafanya kazi za kusafisha mji, mume wangu dereva wa daladala. Anaokutana nao huko anajua mwenyewe na mimi ninaokutana nao nikiwa na fagio langu ni wengi.
Jioni mimi na baba chanja tunajitenga na watoto wanalala chumbai kwao. Nyumba nzima tunachota maji kwa mwenyekiti wa mtaa ndoo ni shilingi mia.
Hayo maji ya kutiririka tunayaona kwenye Bongo Movie. Sisi tunanawa kwenye beseni.
Wataalamu wanasema tusafishe vitasa vya milango, chooni kwetu hakuna kitasa. Ukitaka aliyeko ndani ajue kuna mtu, ana kohoa.
Wanasema tutumie maji ya kutiririka. Imebidi ninunue jagi Kariakoo, watoto wanaosha mikono kwa kushikiana jagi kwa zamu.