Huko WILAYA YA KILOSA Wagonjwa wa KIUME na wa KIKE wanalala wodi moja

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,594
5,568
Wadau,

Kwenye taarifa ya habari ya saa 4 niliskia wakitangaza kuwa huko tarafa ya MIKUMI wilaya ya kilosa mkoani Morogoro kuna hospitali ambayo wagonjwa wa kiume na wa kike wanalala wodi moja.

Kadhia hii imesababishwa na uhaba wa wodi hospitalini hapo,jina la hospitali sikulishika kwakweli.

wagonjwa hao wanadai kuwa hupata shida sana wanapotaka kubadilisha nguo

Chanzo: Redio One

Nimelipata jina la hiyo hospitali,inaitwa hospitali ya Mtakatifu KIZITO AU st Kizito HOSPITAL.

Pia kuna mdau amenitonya kuwa Hospitali kuu ya wilaya ya KILOSA inakabiliwa na upungufu wa chakula na hivyo wagonjwa wanakosa chakula
 
CCM hoyeee!kuna shule ya msingi geita tangu imejengwa ina miaka 47 haina choo mpaka leo!choo ni cha makuti.pamoja na dhahabu iliyopo geita
 
Sasa hapo atakuja DC kukanusha kuwa si kweli
wakati ndiyo hali halisi ya sehemu husika.
 
CCM hoyeee!kuna shule ya msingi geita tangu imejengwa ina miaka 47 haina choo mpaka leo!choo ni cha makuti.pamoja na dhahabu iliyopo geita

Rekebisha mkuu, Hiyo nadhani ni Shule ya Msingi Kibirashi iliyopo Wilaya ya Kilindi na ina miaka 42 toka ifunguliwe sio 47. Au kuna nyingine uliyoona ya huko geita kama unavyonena? Link hii hapa http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari-ya-ndani/Shule-ina-miaka-42-tangu-ijengwe--haina-vyoo/-/1724700/1877800/-/bud2xwz/-/index.html
source: Mwananchi june 10, 2013
 
Nimelipata jina la hiyo hospitali,inaitwa hospitali ya Mtakatifu KIZITO AU st Kizito HOSPITAL.

Pia kuna mdau amenitonya kuwa Hospitali kuu ya wilaya ya KILOSA inakabiliwa na upungufu wa chakula na hivyo wagonjwa wanakosa chakula
 
sasa si bora hao wanalala wodini hta kama wanashea wodi moja kama mume na mke lkn wapo hai.

Huko Muleba kuna outbreak ya malaria ambayo imeshaua watoto wapatao 25 sasa hivi na jopo la madaktari na watafiti wako huko kuangalia kulikoni. imagine wilaya moja ndani ya wiki kupoteza watoto u5 25 sio jambo la kuchezea atiii.
 
Wavute subira, mwaka huu tutatumia 1bn kwa ajili ya makaburi ya viongozi kule Dodoma, mwakani tutaongeza wadi na vitanda.

Zidumu fikra za Lukuvi!!!!!
 
Back
Top Bottom