Huko Spain watu 738 wameaga dunia kwa masaa ishirini na minne. Wakenya na Watanzania tuwe makini ili majanga haya yasitupate

Sisi wenyewe tumejiandaa kivipi kabla kusubiri serikali, nimepiga raundi mtaa kucheck watu walivyojipanga, hali ni kawaida tu watu hawaogopi kukusanyika makundi, subiri tuanguke wachache ndio tutatia akili na kuelewa hiki kitu hakina mzaha.
Mpaka sasa Waafrika hatujafa, hivyo tunasubiri kionyeshe meno na makucha ya kweli kwenye hili bara ndio tutakielewa.
Hehehe!! Nachelea kusema kama rais wa Tanzania, tusitishane, hiki kitu hakina uhatari mkubwa kwa sisi ngozi nyeusi, maana wote walioathirika hadi sasa hakuna aliyekata roho, labda wachache waliokua na mazagazaga yao ya awali, ila omundu strong aliyekula ugali wa Kiafrika bado anapeta tu.
Na wewe leo umeungana na bwana pombe!!??😂😂😂🤣🤣safi sana,binafsi namuelewa bwana Magufuli kitu cha kwanza lazima tuondoe hofu,kisha mapambano yaendelee kimyakimya
 
What about patients with comorbidities, how many patients are on Antiretrovirals, How many are diabetic? Wazee pia, Cancer patients, Those in cardiovascular care, patients with Renal or hepatic impairments,
Mzee hiyo mobu yote wapo kwenye risks kubwa in any case provided their immune system is compromised.
Ukicompare demographic composition ya Africa na Europe .Africa has generally a young population thus deaths will be fewer.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, soma vizuri huo uandishi, kuanzia Vocabulary, ni wazi ni Mbongo kaandika, siasa zetu ni za Hovyo sana, acha Jiwe atawale tu Maisha. Tuna wendawazimu Kibao wanataka uongozi.
Waulize hao wanaojilinganisha na Tanzania badala ya kujilinganisha na hizo nchi ulizotaja. Hivi wanafikiria nini kujisifia Wakati idadi ya maambukizi kwao ni zaidi ya mara mbili ya Tanzania?, huo ndio ujinga ndani ya DNA.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wewe leo umeungana na bwana pombe!!??😂😂😂🤣🤣safi sana,binafsi namuelewa bwana Magufuli kitu cha kwanza lazima tuondoe hofu,kisha mapambano yaendelee kimyakimya

Kwa hili sina budi ila kumkubali kwa hayo maneno yake ya kusema damu ya Yesu tu ndio dawa maana mimi Mkristo, rais wenu amekua sugu hadi Tanzania imefungiwa mipaka na mataifa yote yaliyoizunguka, Kenya, Uganda, DRC, Rwanda na sijui Burundi kwa njaa zake kama naye ana jeuri ya kuwafungia mpaka Watanzania.
Halafu naona Watanzania tisa wamekamatwa wakijaribu kuingia Uganda kinyemela na kufukuzwa, kaeni kwenu kwa sasa acheni kupukutika, kitumbua cha dunia kimeingia mchanga.
Nine Tanzanian businessmen intercepted in Uganda, sent home
 
What about patients with comorbidities, how many patients are on Antiretrovirals, How many are diabetic? Wazee pia, Cancer patients, Those in cardiovascular care, patients with Renal or hepatic impairments,
Mzee hiyo mobu yote wapo kwenye risks kubwa in any case provided their immune system is compromised.

Sent using Jamii Forums mobile app

Dah! Sijazoea kuona ukiandika post inayotumia akili, kumbe kiaina uko sawa upstairs, hili bandiko lako linafaa lisambazwe kwa wote wasome kwanini tusishabikie hiki kitu maana tunao baadhi yetu ambao watakufa sana.
 
Ni jambo gani serikali zetu zinaweza kufanya ili kuzuia mamia ya watu kufa kila siku kwa ajili ya Corona? Jana Italy watu 743 walikufa kwa masaa 24. Leo spain watu 738 wameaga kwa masaa 24. Tutafanya nini ili kuzuia haya majanga kufika kwetu?

Ugonjwa huu si mgeni tena. Unaingia vipi, unasambaa vipi na unadhibitiwa vipi yote hadi leo yanajulikana vizuri.

Hili ni tatizo la nchi moja moja kutanzua. Kenya, Rwanda, Uganda, Tanzania nk, nchi moja moja zaweza kuchagua kuwa salama au kutoweka.

Uzuri ni kuwa Uganda ikichagua kuwa salama haiathiriwi na mwingine yeyote iwe Kenya, Rwanda nk. Mipaka hufungwa.

Kila nchi na uelewa wake.

Ngoma ni ndani ya nchi husika. Limekaa kama mtego wa panya. Litakula wote waliomo na wasiokuwamo.
 
MTU akipona li Corona je anaweza kuambukizwa tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo bado kuna theory ila nilimuuliza jamaa yangu ambaye ni daktari,akasema kuna mambo mawili Kwanza ndiyo anaweza kumbukizwa tena kwa kuwa huu ugonjwa wanavyosema ni mafua kabisa ila kirusi tofauti na jinsi kinavyo athiri mapafu pia ni kitu kipya ila dalili huwa sawa na mafua ila yale chronic.
Kwahivyo mfano ukiambukizwa tena hapo itategemea na mwili wako umetengeneza kinga kiasi gani ili kuweza kupunguza athari za hao virusi ndani ya damu wasikue na kuendelea kukudhuru zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, soma vizuri huo uandishi, kuanzia Vocabulary, ni wazi ni Mbongo kaandika, siasa zetu ni za Hovyo sana, acha Jiwe atawale tu Maisha. Tuna wendawazimu Kibao wanataka uongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe kumbe huwa ni mjinga namna hii? Ati jiwe atawale milele. Hapa Afrika hatutaki marais wanaotawala milele. Kwani yeye tu ndio mwanaume kamili na wengine ni wanawake? Hatutaki mambo ya marais wa Afrika kutawala zaidi ya mihula miwili. Umesikia?
 
Back
Top Bottom