Huko Songea kuna maajabu gani mpaka Wasomali wakimbilie huko?

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,255
2,000
Habari wanabodi!

Katika taarifa ya habari ya leo wakati natazama hapa ITV kuna gari kubwa imepata ajari kule Handeni watu wa tatu wamefariki.

Polisi wamefanikiwa kuwakamata wasomalia kama 15 waliokuwa wakisafiri wanaelekea Songea kwenye makaa ya mawe, sasa hapa ndio najiuliza huko Songea kuna nini cha ajabu mpaka watu wavuke mipaka yote waende Songea?

Kama kuna fursa nyingi tuambiane, haiwezekani watu wavuke mipaka yote waje mpaka Bongo wakati wenyewe wabongo hatujui kama kumeila huko.

Kama kuna mgodi umetema tuambiane ,tuwahi na moko zetu huko bombi nyumbi.
 
Dan Zwangendaba

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
2,649
2,000
Wewe haujaelewa nimeuliza kama kumeila sehemu?yaani kama kuna mgodi unatema huko pesa nje nje.?ukisema kumeila wazee wa migodi wanaelewa wakina Ngosha .
On the way to Canada, US and UK through Mozambique then South Africa. Vijana wa kisomali hawajalala hata kidogo linapokuja suala la kutafuta maisha ughaibuni ndugu.
 
road master

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
1,562
2,000
Habari wanabodi!

Katika taarifa ya habari ya leo wakati natazama hapa ITV kuna gari kubwa imepata ajari kule Handeni watu wa tatu wamefariki.

Polisi wamefanikiwa kuwakamata wasomalia kama 15 waliokuwa wakisafiri wanaelekea Songea kwenye makaa ya mawe, sasa hapa ndio najiuliza huko Songea kuna nini cha ajabu mpaka watu wavuke mipaka yote waende Songea?

Kama kuna fursa nyingi tuambiane, haiwezekani watu wavuke mipaka yote waje mpaka Bongo wakati wenyewe wabongo hatujui kama kumeila huko.

Kama kuna mgodi umetema tuambiane ,tuwahi na moko zetu huko bombi nyumbi.
Hao ni wapita njia
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,600
2,000
On the way to Canada, US and UK through Mozambique then South Africa. Vijana wa kisomali hawajalala hata kidogo linapokuja suala la kutafuta maisha ughaibuni ndugu.
Somalia na Ethropua hakuna rasilamali Zinazovuma hapa Afrika hivyo hawana cha kupoteza hivyo vijana wa kitanzania kuiga kijana msomali/muhabeshi ni kujipotezea muda.
Tanzania kuna migodi bubu mingi sana ya kujichimbia tu na kutoka maisha tena bika kodi.
Tanzania kuna maziwa makubwa 3 yanayotoa samaki muda wote ie Tanganyika Viktoria na Rukwa.
Tanzania ina mabonde oevu ya kulima mwaka mzima ambayo ni Rufiji,Kilombero, Ruaha/Usangu, Nyasa kagera, Kilimanjaro,Malagarasi nk
Tanzania kuna ardhi yenye rutuba isiohitaji mbolea mikoa ya Kagera,Kigoma,Songea,Mbeya,Tanga,Morogoro, Pwani, Lindi mtwara Njombe,Iringa Katavi ,Rukwa,Songwe, Kilimanjaro nk Jichagulie mkoa wa kwenda ukaanzishe kilimo.
Tanzania kuna mbuga za wanyama za kutosha.
Tanzania ina mipaka ya kutosha ya kukuwezesha kufanya biashara na nchi jirani.
Tanzania ina Amani tele na watu wakarimu wenye upendo kila mkoa.
Halafu umuige msomali kutapatapa kwenye maroli huku ukiacha rasilimali za kutosha kukufanya uwe tajiri .
Rejea shairi linaitwa Fikiri:
"Fikiri mimi jamani nakufa hapa kwa nini, chakula kingi nyumba, ..nyumbani ashiba..." .
Ulaya kuna rasolimsli gani za kumtajirisha mkimbizi kutoka Afrika, je waweza nitajia watu maarufu waliotajirika kwa kuwa wakimbizi huko ulaya .
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom