Huko nje Watanzania tunadhauraulika sana siku hizi

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Wale wanaosafiri safiri kidogo ninaamini wananielewa.

Enzi za Mwalimu (RIP baba/babu yetu), huko ubeberuni huyu mzee ingawa walikuwa hawampendi kwa misimamo yake lakini walikuwa wakimwogopa na kumheshimu mno.

Why? Ni kwa vile alikuwa ana uwezo wa kuitetea misimamo yake scientifically (aka kisomi) na IQ yake ilikuwa ipo njema sana. Halafu ukichanganya na ile tabia yake ya kutokupenda ubinafsi (selflessness) ndiyo haswa ilimwongezea legitimacy zaidi ya kusimamia proudly yale aliyokuwa akiyapigania. Akaheshimika!

Sasa hivi tumekuwa nchi kituko. Hata Wamalawi na Wakomoro hapa jirani wanatuona ni kama ma-Zinjanthropus fulani hivi. Ni nyakati mbaya sana hizi za kutambulika kama raia wa Tanzania. Haijawahi tokea!
 
Kha watuache. Juzi huyu Mzee kawa Na 2 Nyuma ya Rais wa Ghana Kama Mwanasiasa Bora wa bara la Afrika kati ya Marais wa Mataifa 54. Umeshindwa hata kuwauliza Marais wao kwenye hiyo Orodha wanashika nafasi ya ngapi!?
Tuanzie hapo kwanza. Vinginevyo ni wivu tu.
 
Acha maongezi ya kicheni party. Huku nje Kuna muda kweli wa kuwaza hayo. Labda Ukiwa unatoka Nigeria ndo askari wanaweza kukutilia Shaka mana jamaa kwa kuforge Ni hatari. Najivunia Utanzania Wangu. Wewe mwenye chuki za kijinga endelea. Afu Malawi napo unaita nchi za nje.
Ni aibu kutambulika kama Mtanzania siku hizi.

But misukule haina sense (mshipa wa) ya aibu kwa hiyo sitashangaa kusikia kuna watu hawaoni aibu!
 
Poleni sana Watanzania wenzetu mlioko huko Ughaibuni maana lazima tu kama masalia pekee ya Zinjanthropus toka Olduvai Gorge. Wakati wa Nyerere Watanzania walikuwa wanaheshimika zaidi kuliko hata hapa nyumbani kuwa sababu ulimwengu ulipenda msimamo na uwezo wa Mwalimu ingawa hakuwa na PhD.

Mtanzania alikuwa akijitambulisha mtaani Ughaibuni kuwa anatoka Tanzania alikuwa anakumbatiwa kama ndo Nyerere mwenyewe ingawa Mwalimu hakuwahi kufika nchi hizo. Naamini wenzetu walioko huko leo wakijulikana wanatoka Tanzania wanatemewa mate usoni na kukimbiwa kama Wakoma.

Enzi za Mwalimu hata wanachama wa CCM walikuwa wanaonekana mitaani wanatamba kwenye sare zao za kijani wakisalimiana "Kudumu Chama cha Mapinduzi" au "Zidumu Fikra za Mwenyekiti" lakini leo labda hayo yote yanatokea kwenye kumbi zao za mikutano. Manachama yanaona aibu kuwa manachama ya Chama hilo!
 
Back
Top Bottom