Huko Duniani Rais anapimwa hivi na taasisi zao

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,219
Africa tuna safari ndefu sana mithili ya safari ya kwenda Mars.

Ni hivi huko duniani kuwa Rais wa Taifa sio lelemama yani baba unapimwa uwezo wako yani utapigwa maswali wewe na wazee waliopiga kitabu wakatoka moshi kichwani.

Yani utafuwatiliwa maisha yako je unasoma vitabu? Unaijuwa nchi yako umetengeneza Bills ngapi zikaleta impact kwenye jamii?
Je unasoma mambo muhimu yakitaifa? Au wewe unapenda udaku.

Je, unasoma taarifa muhimu za siri na unaweza toa comment?

Your level of IQ hapa utakoma yani unatoa mada watu wanakuchambua mwanzo mwisho.

Jamaa wanaenda mbali sana nakuangalia uwezo wako wakusoma vitabu na kutunga vitabu yani hawana habari zetu za Africa hawa jamaa wapo serius na taasisi yao ya Urais.

Ndio maana Bill Clinton kamchepuko tu kangemuondoa ikulu.

Mke wake kosa dogo tu lakuto respond email za CIA na kuvuja kwa email nyeti kule Afghanistan na vifo vya yule agent wa cia ikawe Urais ameukosa. Yani ilikuwa bonge ya issue mpaka mama wa watu akawa mgonjwa.

Hakuna Taifa lenye nguvu dunian wanacheza na hii taasisi kwao hakuna kupokezana vijiti ila kuna kitu kinaitwa performance and integrity.

Unapo ona Baba na mtoto wamekuwa Rais kwa pamoja sio upendeleo ila performance na uzalendo kwa Taifa. Unaambiwa Bush Baba na Mtoto mmoja alikuwa CIA Director Baba na Mtoto Mrusha ndege zakivita na amepona vifo mara kadhaa kwa Taifa lake.

Africa kazi tunayo.
God have a Mercy on us.
 
Sasa Afrika ya Tanzania mgombea hajulikani hadi siku 90 TISINI au pungufu kabla ya uchaguzi. Unahisi muda utapatikana wa kuhoji mambo ya msingi?

Au unahisi huyo aloteuliwa na chama chake atakuwa ana majibu ya papo kwa papo?
Unakumbuka akina wale waliotaka midahalo yao peke yao... Au watumiwe maswali kabla! REALLY!
Kifupi ni kuwa "tunafungashiwa kwenye magunia bila kujua tunachobebeshwa"

NB: Ndiyo maana naunga mkono mabadiliko ya Katiba! Mle viwemo vifungu kuhusu masuala ya uchaguzi huru kwa uwazi!
Mgombea asifichwe fichwe... Sera zipitiwe na kujadiliwa kwa uwazi kwenye mijadala huru!

Tubadililike
 
"... tuachie siasa na taasisi yetu ndiyo uafrika wetu huu, hao wenyewe wana matatizo yao sisi tuna yetu."

Hii ndiyo kauli ya waafrika pale wanapoona wameshindwa jambo na wanatafuta wa kumtupia lawama, hapa tulipo bado tunahitajk hao wakoloni watusaidie unategemea nini la ajabu kutoka kwake?.
 
Kama Trump nae alipimwa kwa hivi vigezo basi US kazi wanayo
Trump alipimwa kwa udhubutu wa kufanya mambo ambayo hakuna mtu mwingine angeweza kufanya. Tutarukaruka lakini Trump aliweza kukanyaga moto kwa miguu, tena pekupeku. Angepata nafasi, angeiba uchaguzi wa US kwa mara ya kwanza.

Mfano kutangaza vita ya uchumi na China. Marekani ilikuwa inamezwa na China kama chatu anavyomeza mbwa. Trump akawasaidia angalau kurusha miguu na kujinasua. Labda by 2030 China atakuwa anaongoza kiuchumi lakini siyo kijeshi.

Pili, tulishuhudia Trump alivyojaribu kuiba uchaguzi uliokamilika. Aliwaaminisha wafuasi wake kuwa atapindua matokeo. Alichofanya dakika za mwisho, ilikuwa uhaini wa wazi. Angekuwa Africa damu zingemwagika kama Rwanda. Tumwache mzungu aitwe mzungu.

Mwisho, Trump anaendeleza mapambano. Hakubali kushindwa kamwe. Hata umpake matope, anaogelea humo humo kwenye tope. Jamaa walimuibulia kashfa kama zote, za wauza k aliokuwa anajitwalia, lakini wapi. Mwisho wakaamua kummaliza kwa kumwibia kura kwa njia za kisayansi.

Mzungu siyo wa kushindana naye.
 
"... tuachie siasa na taasisi yetu ndiyo uafrika wetu huu, hao wenyewe wana matatizo yao sisi tuna yetu."

Hii ndiyo kauli ya waafrika pale wanapoona wameshindwa jambo na wanatafuta wa kumtupia lawama, hapa tulipo bado tunahitajk hao wakoloni watusaidie unategemea nini la ajabu kutoka kwake?.
Utasikia wengine wakichagiza... "sisi ni taifa huru, wasitubabaishe! Tunataratibu zetu..."

Ila kwenye madawa, elimu, magari na simu tupo front mbele kabisa tunademka na vitu vyao bila kujihoji!
 
Kama Trump nae alipimwa kwa hivi vigezo basi US kazi wanayo
Umenichekesha sana. Trump hakupimwa kwa uwezo wake, bali alikuwa ni alternative yao kwa Hillary hasa wale waliokuwa wanachukia kutawaliwa na Obama mweusi, hawakupenda kutawalia na mwanamke! Kwa hiyo wakaangukia yoyte aliyekuwa mwanaume mweupe bila kujali alikuwa na uwezo gani.

Trump ni mtu mzima sana, zaid ya miaka 75 sasa; ila jamaa ana akili za kitoto sana. Ni afdahali angebaki kuendesha biashara ya majumba aliyoachiwa na baba yake ambako alikuwa anaboronga boronga lakini hakuna aliyekuwa anajali; alikuwa akikwama tu, basi anatangaza bankruptcy, sasa hivi alijiexpose mpaka familia yake imekuwa kwenye msukosuko.
 
Trump alipimwa kwa udhubutu wa kufanya mambo ambayo hakuna mtu mwingine angeweza kufanya. Tutarukaruka lakini Trump aliweza kukanyaga moto kwa miguu, tena pekupeku. Angepata nafasi, angeiba uchaguzi wa US kwa mara ya kwanza...
Trump alishinda kwa sababu ya mambo matatu kama si manne...
1. Mfumo dume
2. Mapungufu ya Bill na Hilary
3. Ubaguzi wa rangi
4. Fedha

Yote ya yote Trump hafai kuongoza nchi tofauti na biashara zake!
Kama ulivojenga hoja awali due diligencde ilifanyika... Awamu ya pili system na watu hawakutaka kurudia makosa!

Kwa hapa Tanzania Trump ni mfanano wa Kibajaji au Chalamila!
 
Africa tuna safari ndefu sana mithili ya safari ya kwenda Mars.
Ni hivi huko duniani kuwa Rais wa Taifa sio lele mama yani baba unapimwa uwezo wako yani utapigwa maswali wewe na wazee waliopiga kitabu wakatoka moshi kichwani...
Mkuu, siyo kwa wote ingawa wapo smart sana kwenye issue ya Uraisi.

Ila kwa Trump sina hakika sana...
 
Serikali za ukoloni mlizikataa, na hizi zenu hamzitaki tena. Zimeshawaboa kabisa. Si mngemuacha mkoloni aendelee kutawala? Yule Turnbull angeendelea tuu kubaki kumwakilisha Malkia wa Uingereza mpaka mtakapokuwa tayari kujitawala. Ndiyo nchi za West Indies zilivyofanya na leo wamejenga taasisi imara na demokrasia ya kweli.
 
Africa tuna safari ndefu sana mithili ya safari ya kwenda Mars.
Ni hivi huko duniani kuwa Rais wa Taifa sio lele mama yani baba unapimwa uwezo wako yani utapigwa maswali wewe na wazee waliopiga kitabu wakatoka moshi kichwani....
Hizi ni porojo mjomba......Huko nje ni America tu tena ya kusini vipi mabara mengine sita ukiondoa Africa n yenyewe yako hivyo au ujuaji ni mwingi kwa habari za magazeti .......je USA ina marais wangapi mpaka sasa unazijua record zao,vipi hao makamu wa Rais waliopata Urais baada ya Rais kuuwawa walipimwa lini.......TUACHE UJUAJI NA POROJO
 
Sasa Afrika ya Tanzania mgombea hajulikani hadi siku 90 TISINI au pungufi kabla ya uchaguzi. Unahisi muda utapatikana wa kuhoji mambo ya msingi??
Au unahisi huyo aloteuliwa na chama chake atakuwa ana majibu ya papo kwa papo?
Unakumbuka akina wale waliotaka midahalo
Ndiyo maana naunga mkono mabadiliko ya Katiba!
Tubadililike
Sasa hata kama angejulikana mwaka mmoja kabla kwa africa itasaidia nini?
 
Serikali za ukoloni mlizikataa, na hizi zenu hamzitaki tena. Zimeshawaboa kabisa. Si mngemuacha mkoloni aendelee kutawala? Yule Turnbull angeendelea tuu kubaki kumwakilisha Malkia wa Uingereza mpaka mtakapokuwa tayari kujitawala. Ndiyo nchi za West Indies zilivyofanya na leo wamejenga taasisi imara na demokrasia ya kweli.
Mungu mbariki Mzungu
 
Trump alishinda kwa sababu ya mambo matatu kama si manne...
1. Mfumo dume....
Usisahau Russian intrusion kwenye mifumo ya computer.

Putin hakumtaka kabisa Hillary kwa namna ambavyo alikuwa akiwasaidia wapinzani wa Putin wakati Hillary akiwa waziri wa mambo ya nje.
Hivyo pamoja na udhaifu wa Trump, Putin alimtumia Gen Flyn kama papet wake kupitia Balozi wa Urusi nchini Marekeani Sergey Kislyak

Andiko la mdau lina akili, ila ndio hivyo, at some point hata US na ujanja wao wote, kuna wakati waliingia chaka kwa kuendekeza white supremacy.

Ila lijamaa liliwafaa conservative kwenye mambo ya imani na ndoa. Maana akina Obama, Hillary na Biden ni too liberal mpaka wanakubalina na ndoa za jinsia moja. Kwa sasa kwenye cabinet ya Biden kuna waziri mmoja mwanaume, anapumumliwa na dume jenzake.

Hilo ni moja ya jambo weupe wengi waliona bora nusu shari ya kuwa na mjinga kama Trump ili kulinda maadili ya kiutu, kuliko kuwa na Hillary ambae atasababisha nchi kuwa na major move ya moral decay.

F
 
Uongo mwiiingi,bush alikuaga anambonda mkewe bi. Laura mpk anakimbilia kwenda kulala hotelini.
 
Back
Top Bottom