Hujuma za wakata tiketi za mabasi dhidi yangu

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,796
8,771
Amani ya bwana iwe nanyi. Mungu atuepushe na maradhi ya Corona..waislam muwe na mfungo mwema.

Nimekuwa mhanga wa kutotendewa haki kila ninaposafiri iwe kwenye ndege ama boti.

Nadhani nafanyiwa hujuma kabisa na hawa wakata tiketi za mabasi si kwenda popote pale nimejikuta nakuwa mnyonge safarini hata kama nitakuwa nimewahi seat na kuchagua sehemu nzuri.

Sijawahi kusafiri nikiwa na mwanamke mzuri ama mwanadada mzuri tukiwa katika seat moja zaidi ya kukutana na kero tupu. Mfano kuna moja nilitoka Mwanza kwenda Tabora nikajikuta nipo na mama na watoto wawili ikabidi nitoe msaada.

Kuna safari nyingine Dar Dom kituko kuingia kwenye basi nikutana na jibaba nene halafu likagomea upande niliochagua dirishani nikaona isiwe tabu sababu safari ni moja nikakaa sehemu yake shida ikawa kupanua miguu utadhani amepakata furushi.

Ebu jamani wakata tiketi mjaribu kutupangia sisi wawindaji wadada ama wanawake wa maana kumbuka safari ya Dar Songea halafu unapangwa na kitu cha hatari hii kwangu ni hujuma. Najitayarisha ninunue gari langu ili nami nichague pin za kusafiri nazo.
 
Back
Top Bottom