Hujuma za uchina afrika

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Ni kweli uchina imesaidia sana katika kuendelea miundombinu na ujenzi wa vitu vingi sana katika afrika hili halina ubishi kabisa , pamoja na kufanya yote haya kuna baadhi ya vitu uchina inavifanya lazima tuvitupie macho japo kidogo tuwaambie hapa mmekosa hatutaki uwekezaji wa aina hii hata kama una maslahi gain kwetu tuangalie maisha ya mbele zaidi .

Ukienda nchini sudan kuna sehemu mbili kusini na kaskazini , kwa waisilamu wengi na wakristo wengi , kweli kwenye serikali uchina imesaidia sana kujenga nchi hiyo miundo mbinu yake na viwanda vyake vingi na kutoa misaada mingi ya kijeshi na silaha , hao ndio wanaouwa ndugu zetu kule darfur siku zote wanachochewa na uchina , hawa ndio ambao hawataki kuelewana na ndugu zao wa kusini ambao wengi ni wakristo na ni weusi .

Wachina wanajua kwamba mwaka 2011 katika kura ya maoni sudani ya kusini inaweza kuamua kuwa nchi huru kwahiyo sasa iko katika mipango mingi sana ya kujenga miundo mbinu ya taifa hilo la sudani ya kusini huku likifanya tafiti nyingi katika maeneo ya mafuta kwa ajili ya nchi yao wakati ujao .

Mwaka huu tu , nchini Ethiopia Kampuni moja ya china imeamua kufungua kiwanda cha kutengeneza simu za mikono , sijapata taarifa kiwanda hicho kitaanza lini haswa uzalishaji , kiukweli Ethiopia haina madini ya kutengeneza simu hizo kwahiyo wanatumia Somalia kama sehemu ya kutoa madini hayo , huku watu wakipigana vita wao wanachukuwa madini na kwenda kuyapeleka Ethiopia kwa ajili ya shuguli hiyo .

Hata jirani yetu Rwanda nae yuko mbioni kuanzisha kiwanda cha kutengeneza simu za mikononi , unaweza kutaharuki Rwanda mbona haina madini hayo , madini yanatoka kongo ambapo Rwanda siku zote inakataa kwamba inashiriki vita huko .

Nchi ya kongo ilivyokuwa kubwa vile na watu wake wameshindwa hata kuzalisha chip mojabadala yake kanchi kwa Rwanda kwa msaada wa china ndio kimekuja kufaidika na swala hili kweli kipofu usimshike mkono .

Mambo haya yanayoendelea nchi jirani lazima iwe funzo kwetu na kwa maendeleo yetu .

Pamoja na kwamba nchi za magharibi zinamsifia sana paul kagame lakini hazitaki kusema ukweli kuhusu mienendo ya watu wake na taifa lake kwa mataifa jirani jinsi wanavyofanya nakupata maendeleo hayo

Hata hivyo hii haishangazi sana Marekani imeshawahi kuvamia mataifa kadhaa katika kudhibiti mataifa hayo kwa ajili ya maslahi yake ya siku zijazo hata vita ya pili ya dunia tatizo hakuwa Hitler , huyu alitumika kama kisingizio tu kuna mataifa yalitaka kutoka kwa kutumia jina la Hitler .

Jioni njema
 
Back
Top Bottom