Elections 2010 Hujuma ya ccm kwa maalim seif sharif hamad, alishinda znz ccm walipora ushindi wake

Hapa siwezi kumwita Maalim Seif ni shujaa na kumlinganisha na Mandela. Mandela alikuwa tayari hata kufa ilikuhakikisha waafrika kusini wanaondokana na utawala dhalimu wa kibaguzi. Watu walikuwa tayari kufa kwa kupiginia haki. Sasa kama mtu ananyamaza ili yaishe huyu ni coward leader na hajawatendea haki wapiga kura wake. Basi angewaeleza ukweli kwamba kura za CUF ni hizi hapa na za CCM ni hizi hapa, lakini kwa kuwa CCM hawataki kuondoka madarakani wameamua kujitangaza washindi, then wapiga kura wenyewe wangejua nini cha kufanya.
 
No Chama kilichoshinda ni CUF. Ilani itakayo tekelezwa ni ya CCM!

With all due respect to the readers, I honestly believe that the "All inclusive government of Zanzibar" will work for the interest of all Zanzibaris. What most of us did not seem to notice was tha fact that CCM in Zanzibar were sympathetic to CUF policies only that they could not oppose it openly. Even where the opportunity presented itself, you could see the leverage of the House of Representatives to the CUF agenda. Take for example such things as the Statehood of Zanzibar and Oil exploration.

Over the next 5 years, expect to see the GoZ moving away from the Union and, well, anything can happen.
 
hayo yote kwa zanzibar yalifanyika, kumbuka uchaguzi wa '95, walipokataa nini kilitokea, 2000 ndo vile tena mauaji ya historia na ccm ikaendelea kubaki madarakani, 2005 unajua kilichotokea unafikiri hata wangekataa 2010 kingetokea nini?

Sawa.
haya maisha ndo mpaka lini?
maamuzi ya wananchi wengi yataheshimiwa lini?
ndugu zangu kwa mtindo huu CCm itatawala milele.
tusijidangnye eti CCM itaachia madaraka kwa hiari,:sad:
 
Mimi sielewi hii lugha kuwa CCM imemhujumu Maalim Seif wakati huo huo tunaambiwa wamekubaliana, nafikiri tungesema Maalim Seif amewahujumu wana CUF kuuza ushindi waliompa kwenye sanduku la kura. Na hapa pia tukubaliane kuwa huu ndiyo mwisho wa CUF, kwani sidhani kama uchaguzi ujao kuna mwana CUF atapoteza muda wake kwenda kupiga kura. Kwaheri CUF kwaheri UPINZANI VISIWANI.
 
Hujuma zilikuwepo na iko siku zitasikika tu ,hilo halina mjadala ,tatizo hapa TZ bado hawa viongozi wanaoondoka na kumaliza muda wao huwa hawana la kufanya kwa ufupi huwa hawana tena kazi ,na wengi wao hawajui wafanye nini ,si watu wa biashara au wenye kumiliki viwanda ,yaani wanakuwa hawawezi kujiajiri na wanabaki katika uongozi wa nchi wakati wao si wahusika tena ,kwa ufupi huwa wanaingilia uongozi uliokuwepo na kufikia hata kuuteka nguvu au kuweza hata kuanzisha makundi.

Angalia alipoondoka Mwinyi,alipoondoka Mkapa viongozi hawa wamekuwa wakijishirikisha katika shughuli mbalimbali za serikali kikamilifu na kufikia hata kutoa hoja ,ni juzi tu katika ugombea Uraisi walijitwika na hata kuambiwa kuwa mwanzo walisusa kumkampenia Kikwete na baadae wakaibuka na kuanza kufanya kampeni katika baadhi ya sehemu.

Watu wa aina hii ni hatari sana katika nchi maana hawajiamini kuwa uongozi wao umemalizika ,sasa fikiria kama kila baada ya miaka mitano tungekuwa tunapata Raisi mpya hivi tungekuwa na msururu wa watu wangapi ?Tokea Mwiny ingelikuwa tayari wametimia watano (Tunawaita Maraisi wastaafu) Kuna Mawaziri wastaafu ,mambo ambayo watu hawa huwa hawaonekaniki katika nchi zingine ,haswa huko Maulaya ambako tunasema ndio kuna maendeleo ,hapa kwetu iweje watu hawa wawe wameganda kwenye serikali tena wakiwa na nguvu ya msukumo wa kuamrisha au kutaka kusikilizwa.

Hatujamsikia Ronald reagan wala Clinton wala Joji Kichaka na mtoto wake kujihusisha katika siasa za Marekani kwenye level za Kichama zinazoingiliana na Serikali wala ndani ya Chama au vyama vyao huwasikii kutajwa kabisa ,wanasema wakati wao umepita ,wakae wakila mafao na sikujihusisha na mambo ya serikali wala Chama.

Lakini hapa Tz hawa jamaa wanakuwa kama luba hawachezi mbali na Chama wala na serikali kote wapo ,haijulikani kama ni washauri au ni mashawishi ,ndio maana ikawa nchi yetu haiendi mbele ,maana kila mtu anapotaka kufanya ni lazima hawa jamaa wawe wenye kutia miguu ,kwenye vikao wamo,kwenye tume wamo ,hivi tutawakusanya watu wa aina hii mpaka lini ,maana mwisho wake wanaweza kutosha kuunda baraza la mawaziri.

Alichokifanya Seif Sharif ni kitu kikubwa sana na ndio hawa jamaa ndoto zao za kuivuruga Zanzibar na kubakia wao waendelee kuwa washauri wa kuchumia matumbo yao zilipopigwa na chini.

Kilichojiri Zanzibar nionavyo ni kuwa kama mliwahi kusikia kuna makundi yakipinga kuwepo kwa serikali ya umoja wa Kitaifa ,makundi au kundi hili halikuwepo Zanzibar tu hata huku Tanganyika lilikuwepo na likiwa bila ya shaka na nguvu fulani ndani ya vyombo vya dola au serikali.Sasa nia haswa na madhumuni kwa habari za hapa na pale,ilikuwa Maalim Seif akatae matokeo yaliyochakachuliwa ,wakiwa na tamaa kuwa Maalim atakataa na wananchi wataingia mabarabarani kupinga matokeo ,hapo kitatokea kitakachotokea na kutakuwa hakuna tena yale maridhiano ,yaani hata kama pasingetokea fujo ,lakini kama CUF wangeyapinga matokeo inamaama wasingekubali kuingia kwenye serikali ya umoja na wala wasingeweza kutoa makamo ,natumai hio hali mmeiona hapo au sio ?

Na kwa mtazamo wao huo wangefanikiwa kubakia katika serikali wao peke yao ,na wangekuwa na hoja kuwa CUF hivi na vile ,lakini Maalim na wenziwe walikuwa wameshaona au wameshayaona hayo kwa kitambo ,yaani walikwisha weka possibilities zote na majawabu yake na kama kawaida ilipotokea hali iliyotokea waliweza kutoa jawabu na leo hii wamo kwenye serikali na wanashiriki kikamilifu ,lile kundi limenyweaa vibaya sana .bado lipo na linajipanga lakini watu wapo macho na wanakwenda nao.
 
mi nampongeza sana maalim kwa busara zake. kama asingekubali sasa hivi tungekuwa tunaongea story nyingine hapa jf, tena sisi sisi ndo tungekuwa tunalaumu kwamba viongozi kwa uchu wa madaraka wanasababisha damu za watu zimwagike. na ni ukweli usiopingika kwamba damu ingemwagika baada tu ya maalim kuyakataa matokeo, so amepima na kuamua kwa busara sana na ni viongozi wachache sana wangeweza kuamua hivi, nadhani mliona yaliyotokea kenya.

Carmel, talk for yourself not JF. Huwezi kumuita uchu wa madaraka kwa mtu anayedai haki yake. Mwenye uchu wa madaraka ni yule anayekunyima haki yako ili aendelee kuongoza. Mfano mzuri ni CCM na ZANU PF. CCM kila siku wanatumia propaganda za amani na utulivu huku wakiwasingizia wapinzani kuwa wanavunja amani wakati ni wao ndiyo wako busy kuhatalisha amani yetu.

Anyway, to cut the long story short, mimi sidhani kama ni kweli Maalim alishinda. Kama ni kweli alishinda halafu akakubali kama wanavyosema hapo juu basi yeye ni failure wa harakati na kama angekuwa ni kiongozi wetu wakati tunapigania uhuru, nafikiri mpaka leo tungekuwa bado tunatawaliwa.
 
Let me repeat what I said before: CUF is an extension of CCM.

Do not expect CUF to ever win a presidential election.
 
Mwiba,
Mkuu wangu mbona unarudia yale mloyataka toka mwanzo?..Jamani kama kweli mnaweza kumsifia Maalim Sief kwa hili wkaati mwaka 2005 hauna tofauti na mwaka huu ati kwa sababu ya amani wakati mnajua fika hakuna haki nashindwa hata kuelewa mantiki ya sifa hizi.
Labda wewe na wemngine nifahamisheni tofauti iliyopo leo hii huko Zanzibar baada ya kukubali kushindwa na mwaka 2005 ikiwa wananchi bado hawaikubai CCM.

Huyo Maalim anakuwa makamu wa rais ambaye hana nguvu yoyote ya kiutendaji isipookuwa kusubiri kama Dr.Shein atakufa. Haya waziri kiongozi atatoka CCM pia sasa sielewi huu muafaka utaleta mabadiliko gani kwa wananchi zaidi ya viongozi wa CCM na CUF kugawana majukumu ambayo yatafuata sera za CCM.
 
Mr. Zero kwani utawala wa wajerumani tanganyika na huu utawala wa ccm ni bora upi?
 
Huu unafik ndio utakao ashiria kifo cha muafaka. Dunia nzima ilimsikia Maalim akikiri kushindwa na kumpongeza Rais mtarajiwa ! Sasa leo mnataka kuleta za kuleta kuwa alifanya hivyo akijua kuwa ameibiwa? Kama palikuwa na makubaliano kama hayo yangebaki baina yenu na siyo kuyaleta kwenye kadamnasi. Kwa kufanya hivyo, badala ya kujijengea heshima mnajionyesha kuwa ni wanafik na ndumila kuwili. Mshindi wa uchaguzi wa urais Zanziba ni Shein na si mwengine. Sisi wamisheni kabla ya watu kufungishwa ndoa huwa waliokuwepo wanaulizwa kama kuna mwenye pingamizi na kitendo hicho na kukumbushwa kuwa kama hatasema wakati huo basi asije sema wakati mwengine wowote. Nafsi ya kuzungumza mlikuwa nayo, hamkusema basi do us all a favor, mnyamaze. Hii buyer's remorse itawapeleka pabaya.

Amandla.......
 
Ismail Jussa Abdulrahman acha umbea ! Seif Shariff Hamad hakushinda na ulimwengu wote ulimshuhudia akimpongeza Dr. Shein kwa ushindi wake. Hata hivyo nakushukuru kwa kutufunulia makubaliano katika hii ndoa isiyo ya kawaida baina ya CCM na CUF. Angalau sasa tumeweza kujua nani alitoa posa na hivyo kuwa na sauti katika hii nyumba pamoja na uwezo wa kutoa talaka. Hakuna namna yoyote mtu anayekubali haki yake iporwe anaweza kuitwa shujaa, hapo Ismail Jussa Abdulrahman unajaribu kufunika kombe mwanaharamu apite. Msaliti ni msaliti tu hata ukimpaka rangi gani hawezi kuwa shujaa na Seif Shariff Hamad nafsi yake itamsuta kwa maisha yake yote hapa duniani. Endeleeni kujidanganya na huo muafaka, toka lini mafisadi wa CCM wakaheshimu mwafaka na upinzani - CUF mmeliwa !
 
nadhani Cuf walisahau kuwa muoaji huwa ni mume na muolewaji huwa ni mke
sasa ni dhahili kuwa sasa wao wameolewa na ccm na si ccm wawe chini yao hao cuf bali
cuf kazi yao ni kuitika bee kwa ccm
 
Back
Top Bottom