Hujuma viongozi kuwahadaa wakuu wa nchi

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Nimesimuliwa kioja hiki na kiongozi mwandamizi wa huko nilipokuwa nafuatilia yaliyojilia ziara ya Naibu Waziri Mwanri wilayani Ludewa, hujuma zimezoeleka kwa miongo na awamu kadhaa za uongozi katika nchi hii, ni donda ndugu.

Asante Mfuatiliaji, na haya mambo ya watendaji kuwadanganya viongozi hayajaanza leo;​

Mwaka 1988 kule Manda - Ludewa idara ya maji hao hao walimdanganya Rais Mwinyi, wakachotelea maji kwa ndoo, wakayajaza kwenye tenki, Rais Mwinyi akanawa maji bombani na alivyoondoka maji hayakutoka tena mpaka leo.
 
Idara ya usalama wa taifa inafanya kazi gani hadi uozo kiwango hiki kuifunika nchi? Ni aibu kubwa usalama wa taifa kutokuwa makini na utendaji wao na kabisa kufanya hadaa ya hali ya juu kumdanganya kiongozi wa nchi uwepo wa huduma sehemu husika na anapokagua kubaki chenga ya macho. Hawa usalama wa taifa huwa hawahakiki shughuli zinazohitimishwa na ratiba ya mkuu wa nchi hadi kuingia kwenye kashfa zinazofukiwafukiwa?
 
Nimefunguka akili, kumbe ndio njia wanayofanya hawa viranja wa idara ya maji, maana wakuu wanapokuja kufungua miradi ya maji hutoka pale tu wanapojaribia, na wakishaondoka hakuna kinachoendelea, jamani kwa nini hawafuatiliwi?
 
Mbona Rais Kikwete licha ya kuchezewa mchezo huo mara nyingi na hata vyombo vya habari kuanika ukweli hajachukulia hatua wahusika? Mi naona ni mpango mzima kutoka ngazi za juu.
 
Nimesimuliwa kioja hiki na kiongozi mwandamizi wa huko nilipokuwa nafuatilia yaliyojilia ziara ya Naibu Waziri Mwanri wilayani Ludewa, hujuma zimezoeleka kwa miongo na awamu kadhaa za uongozi katika nchi hii, ni donda ndugu.

Asante Mfuatiliaji, na haya mambo ya watendaji kuwadanganya viongozi hayajaanza leo;​

Mwaka 1988 kule Manda - Ludewa idara ya maji hao hao walimdanganya Rais Mwinyi, wakachotelea maji kwa ndoo, wakayajaza kwenye tenki, Rais Mwinyi akanawa maji bombani na alivyoondoka maji hayakutoka tena mpaka leo.

Nao walitokea huko huko na walizoea kufanya hivyo hivyo, kwa hiyo hawashangai kwa vile ni mazoea yao.
 
Back
Top Bottom