Elections 2010 Hujuma:star TV wagoma kurusha habari za Igunga

kipindupindu

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
1,053
170
wakuu nimemaliza kuangalia taarifa ya habari ya saa nne asubuhi katika kituo hiki cha televisheni,nilitegemea habari ya kwanza ihusu uchaguzi wa igunga,lakini hakuna habari yoyote iliyorushwa kuhusu igunga.watanzania tunanyimwa haki ya kuhabarishwa sijui kwa maslahi ya nani?
Jk katika mambo muhimu ya mwisho wa mwezi 9 ameongelea kuhusu uchaguzi wa igunga iweje chombo cha habari kama star t.v isituhabarishe kuhusu uchaguzi huu??TCRA na baraza la habari najua mpo humu jamvini fungia vyombo vya habari feki kama hivi.

nawasilisha.

Updates:kwa sasa wanaleta matangazo kutoka igunga kwa awamu ingawa watangazaji wanaonekana kuhadaa umma kwamba watu hawajajitokeza kwa wingi,wanasahau watu waliofika kwenye vituo vya kupigia kura halafu wakakosa majina yao katika vituo hivyo.
 
si lazima kaka vyombo vya habari vilete habari unazo zitaka wewe, kwani unafikiri kila mtu anataka kusikia habari za siasa, kama mwanasiasa nenda igunga huko.....
 
halafu sas hivi wanajidai kujadili siasa!!naomba t.v za kenya zije tz kufanya live covarage ya matukio ili tuwapige chini hawa vilaza
 
si lazima kaka vyombo vya habari vilete habari unazo zitaka wewe, kwani unafikiri kila mtu anataka kusikia habari za siasa, kama mwanasiasa nenda igunga huko.....
watu wanatakiwa kupewa habari za aina yote matukio,siasa,michezo,biashara,utamaduni n.k
huu ni mfumo wa kawaida katika upashanaji habari na star t,v imekuwa ikifuata mfumo huu siku zote isipokuwa leo.vyombo vya habari vinawajibika kutupa habari halafu sisi tuchague habari tunazopenda!!
 
yahya nashukuru kwa responce yako lakini swali langu la msingi iweje habari ya igunga isionekane muhimu kwenye habari zenu za leo?kuweni makini fuateni maadili sio shinikizo!
 
Kama nimfuatiliaji wa habari za Star TV wa uhakika huwezi kuwa na Malalamiko haya kwa jinsi coverage ya Igunga inavyopewa Umuhimu, Haturudii habari kama wengine kama ulitzama jana saa 2 usiku habari hiyo imeruka na leo saa 12 asubuhi, sasa tunahangaikia zoezi la upigaji kura. Tazama saa 5 mpaka kutakapokucha.
 
wakuu nimemaliza kuangalia taarifa ya habari ya saa nne asubuhi katika kituo hiki cha televisheni,nilitegemea habari ya kwanza ihusu uchaguzi wa igunga,lakini hakuna habari yoyote iliyorushwa kuhusu igunga.watanzania tunanyimwa haki ya kuhabarishwa sijui kwa maslahi ya nani?
Jk katika mambo muhimu ya mwisho wa mwezi 9 ameongelea kuhusu uchaguzi wa igunga iweje chombo cha habari kama star t.v isituhabarishe kuhusu uchaguzi huu??TCRA na baraza la habari najua mpo humu jamvini fungia vyombo vya habari feki kama hivi.

nawasilisha.
Hatuna umeme wa kuangalia TV
 
yahya M,naona saa tano imefika halafu mnatuwekea kibonde na tibaijuka!!!!anyway ngoja niendelee kusubiri labda mnarekebisha mitambo
 
yahya nashukuru kwa responce yako lakini swali langu la msingi iweje habari ya igunga isionekane muhimu kwenye habari zenu za leo?kuweni makini fuateni maadili sio shinikizo!

Maadali gani unayoyazungumzia hapa...kwani kuna sheria inayowabana kutangaza muda unaotaka wewe?
 
kama nimfuatiliaji wa habari za star tv wa uhakika huwezi kuwa na malalamiko haya kwa jinsi coverage ya igunga inavyopewa umuhimu, haturudii habari kama wengine kama ulitzama jana saa 2 usiku habari hiyo imeruka na leo saa 12 asubuhi, sasa tunahangaikia zoezi la upigaji kura. Tazama saa 5 mpaka kutakapokucha.
a bana we mjajna wenzio humu tunaficha undani wetu wewe umeuza hadi sura ...kula tano .mbili mpe isack ndodi
 
Huyu Yahya M ndio yule wa Star TV? Jamaa ana hasira sana anapofanya mahojiano na wapinzani wa CCM, yaani hasira hadi anauma meno na kufinya mdomo

avatar29341_3.gif
 
Back
Top Bottom