Nyamemba
JF-Expert Member
- Nov 3, 2011
- 845
- 447
Kwa miaka kadhaa mkoa wa Mara na hasa wilaya ya Serengeti umekuwa mateka wa mikoa ya kanda ya kaskazini kimkakati na kimalengo. Mapato karibia yote yanayopatikana kutokana na fursa za utalii yamekuwa hayawanufaishi wakazi husika huku Makao Makuu ya mbuga hii kubwa barani Africa ikiendelea kubaki mkoani Arusha. Kwa makusudi watawala kwa maana ya viongozi waandamizi, ma-DC, na wale wa idara nyeti za serikali wamekuwa kwa miaka yote wenyeji wa mikoa ya kaskazini kuletwa kuendeleza hujuma na kufifisha maendeleo ya wilaya/mkoa huo. Kuanzia kwenye uchaguzi mpaka kwenye mipango ya kibajeti kumekuwa na hujuma za waziwazi kuhakikisha kuwa Serengeti inabaki kuwa tegemezi kwa mkoa hasa wa Arusha. Viongozi wa kisiasa na wafanya biashara wa mji huo wamekuwa kwa mara kadhaa mateka wa mikoa hiyo kwa kuahidiwa tender za kusupply mahitaji kwenye hotel zilizopo kwenye mbuga hiyo huku viongozi wa kisiasa wanaoonyesha kutokubaliana na hali hiyo wakihujumiwa waziwazi na kupoteza nafasi zao za uwakilishi.
Katika uchaguzi wa mwaka Jana umeshuhudia hujuma za waziwazi hasa baada ya viongozi wa serikali na CCM kuwa mateka wa mgombea wa Ukawa, na kwa mara ya kwanza jimbo hili liliangukia Chadema huku na halmashauri nayo ikienda Chadema. Inaelezwa kuwa kuanzia mwenyekiti wa CCM wilaya aliyejiuzuru kwenda Chadema na baadae kurudi ili akamilishe mpango wa EL, mjumbe wa NEC, viongozi wa Idara nyeti za serikali walikuwa wana wa support Ukawa na hata pale, mbunge wa jimbo hilo ndg Marwa Ryoba, mwalimu alipotangazwa mshindi kwa mkakati maalum, M-NEC Serengeti alitoa Zawadi ya ng'ombe wawili kuchinjwa kwenye sherehe za kusherekea ushindi huku wao(viongozi) wakienda kujipongeza ndani ya hoteli mojawapo ndani ya mbuga ya Serengeti.
Ikumbukwe kuwa wafanyabiashara hao ambao ni viongozi wa CCM na ndugu zao ndio wenye tender zote ndani ya wilaya hiyo huku miradi yote wakiitekeleza chini ya kiwango. Mfano miradi ya maji iliyofadhiliwa na world Bank ilichukuliwa na mwenyekiti wa zaman wa CCM na mjumbe wa sasa wa NEC ambapo miradi yote ameijenga chini ya Kiwango na hakuna mradi uliokamilika so far na maji hayatoki. Wafanyabiashara hao walijimilikisha viwanja vya wazi huku wakijiuzia mali za umma na wengine wakipanga kwenye majengo ya Chama kwa ujira mdogo mno.
Natoa wito kwa serikali ya awamu ya tano chini ya Dr Magufuli na PM Majaliwa kutambua aina ya viongozi na watendaji wa serikali mliowarithi kabla ya kuanza kutekeleza yale mliowaahidi watanzania Kwani wamejipanga kukwamisha juhudi zenu.