Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Soma Raia Mwema ya leo uk wa 2 kuhusu suala hili - paragraph husika inasema:
Kwa kadri ya mwenendo wa matokeo, chama chenye kupata wabunge wengi ndicho kitakachoweza kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kile kitakachofuata kwa idadi ya wabunge kitaongoza Kambi ya Upinzani Bungeni.
Mchuano huo ama kuongoza kambi ya upinzani au kuunda serikali sasa ni dhahiri ni kati ya CCM na Chadema
Kwa mujibu wa mwenendo wa matokeo ya kura za ubunge, Chadema inaelekea kupata wabunge wengi zaidi ya CUF ambacho awali ndicho kilichokuwa kikiongoza Kambi ya Upinzani Bungeni chini ya kiongozi wake Hamad Rashid Mohammed.
Hata hivyo, katika Bunge la tisa lililovunjwa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, CUF ilikuwa na uwezo wa kuunda kambi ya upinzani bila ya kushirikisha chama kingine cha upinzani na ilifanya hivyo mwanzoni mwa Bunge lakini baadaye chama hicho kilishirikisha wabunge wa vyama vingine ambavyo ni Chadema, UDP, na TLP.
Katika mazungumzo yake na Raia Mwema kuhusu mazingira hayo, kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni aliyemaliza muda wake Hamad Rashid Mohamed amesema taratibu za sasa zinabainisha chama chochote cha siasa kinaweza kuunda kambi yake kama kitafikisha asilimia 12 ya wabunge wote wa Bunge.
Wabunge hao wanaopaswa kuunda asilimia hiyo 12 ni wa majimboni pamoja na wa viti maalum ambao idadi yao kutoka katika chama cha siasa inategemea idadi ya kura za urais alizopata mgombea urais wa chama hicho.
Mgombea urais atakayekuwa na kura nyingi za urais ndiye chama chake kitapata wabunge wengi zaidi wa viti maalum.
Kwa mwenendo ulivyo, Raia Mwema imebaini kuwa wagombea wa urais wanaotarajiwa kupata kura nyingi zitakazowezesha vyama vyao kupata wabunge wengi wa viti maalum ni Jakaya Kikwete wa CCM, akifuatiwa na Dk Wilbrod Slaa wa Chadema huku Profesa Ibrahim Lipumba akiwa katika nafasi ya tatu….
Asante Mkuu Zak.
Kwa hivyo dhahiri Chadema ndicho kitakachoweza kuunda kambi ya upinzani, unless kama serikali ya CCM (yenye kumiliki Tume hii ya uchaguzi) - NEC) itakapoamua kukinyima Chadema haki hiyo kwa kumfanya Lipumba kuwa wa pili kwa JK katika kura za urais ili CUF ipate wabunge wengi wa viti maalum.