Hujuma kuwanyima Chadema kuwa Chama kikuu cha Upinzani Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hujuma kuwanyima Chadema kuwa Chama kikuu cha Upinzani Bungeni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gurudumu, Nov 3, 2010.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa najaribu kujiuliza kwanini kuanzia jana mchana mapambano ya kulazimisha ushindi kwa CCM na hasa kuwanyima Chadema ushindi wao hasa katika majimbo ya Segerea, Kigoma Mjini, Karagwe, NGara, n.k

  kumbe sasa hivi Chadema na CUF wana jumla ya viti vya ubunge 24 (CUF wana viti 22 kutoka Zanzibar na 2 kutoka Bara). Iwapo chadema watapata angalau kiti kimoja tu cha ubunge basi wanahakikishiwa kuwa chama kikuu cha upinzani bungeni. Kwa CCM hii ni hatari na hasa ni hatari zaid kwa mafisadi.

  kwa matiki hii, usishangae CCM wakawa tayari kumwaga damu ili kuhakikisha chadema hawapati kiti kingine cha ubunge.
   
 2. c

  chamajani JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wee umerogwa eenh? nani alokwambia lengo ni chama kikuu cha upinzani, lengo ni upinzani kuwa juu! wee unawaza kubomoaaa-toa uchafu wako huu.
   
 3. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mimi nililiona hilo mapema sana mkuu, chadema si wana majimbo 22 sasa? check hesabu zako pls
   
 4. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Pia kuna majimbo ambayo kura za wabunge bado kupigwa. Anaeyafahamu atuorozeshee hapa.
   
 5. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Yaani, watu bado hawaelewi mapinduzi yaliyotokea na yanayoendelea kutokea. Nina furaha sana, no matter what!
   
 6. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  lengo la chadema sio kuwa chama kikuu cha upinzani, bali ni kuwa chama tawala, mbona bado mmelala hivyo jamani???:A S angry:
   
 7. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Polepole watu wanaanza kuyakubali matokeo!
   
 8. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hilo linafahamika mkuu ila tumalize lililpo kwa sasa kwanza, fumbua macho uone ccm wanachotaka, acha kulala unaibiwa huku!!!
   
 9. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,205
  Trophy Points: 280
  Kwa hilo hawawezi hadi sasa hakuna chama kingine zaidi ya CCM kitakachoipiku Chadema wabunge, usisahau idadi ya kura za uraisi nayo itachangia kwenye 30% ya viti maalum kitu ambacho Lipumba ameshamaliza pumzi yeye alitegemea kura za Pemba na Kusini ambazo tayari zimeshatolewa.
   
 10. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mhhh unayosema huenda yakawa na ukweli kiasi fulani. Lakini hebu tujiulize mengi ya mambo mazuri chadema ilyafanya bungeni kipindi kilichopita je ilikuwa ni chama kikuu cha upinzani???? Idadi ya wabunge wa chadema ilikuwaje????(5 tu) lakini walifanya kazi nzuri na kubwa. Hivyo basi, mi nafikiri wasiumize saana kichwa na kujenga uhasama na chuki na wapinzani wenzao, badala yake nashauri wajaribu kujenga mahusiano na wenzao kama itawezekana, maana sidhani kama unaweza afikiana na mtu kama Lyatonga ambaye ameshaomba JK amchague kama waziri wa mambo ya ndani. Vinginevyo Chadema wajipange uzuri, wagawane majukumu na wananchi tunategemea watafanya kazi nzuri zaidi na ya kutukuka ili uchaguzi ujao tulichukue bunge zaidi ya 50%. Ama kwa majimbo ambayo kuna ushahidi ulowazi wa hujuma kama Kibaha Shinyanga mjini na Segerea basi Mabere na Tundu wajipange uzuri wafungue kesi mahakamani kupinga matokeo hayo. Katika hili nawaomba Chadema wawe strategic saana, wafungue zile kesi tu wanazoona kuna ushahidi wa kutosha ili kwanza kusevu gharama za uendeshaji kesi na pia kupunguza matumizi ya muda kwenye kesi badala ya kuutumia muda huo kuwatumikia wananchi. Chadema inabidi mkumbuke kuwa miaka mitano ni michache saana, wanachi wanategemea mengi toka kwenu, mkiweza kuyatenda yakaonekana basi mtakuwa mmejenga misingi ya kurudi bungeni 2015 na kuongeza idadi ya wabunge, lakini mkishindwa kutekeleza basi hamtorudi bungeni 2015 na mtakuwa mmeua kabisa nguvu ya upinzani nchini1
   
 11. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kama ni kweli tunashukuru kwa kutuondolea hofu. Sasa tuendelee kufuatilia majimbo yetu na kura za urais
   
 12. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Majimbo bado kupigwa ni pamoja na Mpanda Kati (chadema -mh arfi)
   
 13. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Lengo la chadema sio kuwa chama kikuu cha upinzani bali ni kuifanya ccm kuwa chama kidogo cha upinzani, toa blanket la usingizi hilo mtz!:A S angry::A S angry:
   
 14. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Pemba pia kuna majimbo ya cuf ambayo bado, ni yapi hayo?
   
 15. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  usimshangae!!! hizo ndio akili zetu hatuwazi mambo makubwa, ndio hao wakipewa elfu 2 na doti ya khanga au t-shirt miaka mitano!!:smile-big:
   
 16. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hero pia umelala usingizi, maliza kwanza jambo lililopo mezani ndo tukadai kura zetu walizoiba za urais
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Soma Raia Mwema ya leo uk wa 2 kuhusu suala hili - paragraph husika inasema:

  Kwa kadri ya mwenendo wa matokeo, chama chenye kupata wabunge wengi ndicho kitakachoweza kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kile kitakachofuata kwa idadi ya wabunge kitaongoza Kambi ya Upinzani Bungeni.

  Mchuano huo ama kuongoza kambi ya upinzani au kuunda serikali sasa ni dhahiri ni kati ya CCM na Chadema

  Kwa mujibu wa mwenendo wa matokeo ya kura za ubunge, Chadema inaelekea kupata wabunge wengi zaidi ya CUF ambacho awali ndicho kilichokuwa kikiongoza Kambi ya Upinzani Bungeni chini ya kiongozi wake Hamad Rashid Mohammed.

  Hata hivyo, katika Bunge la tisa lililovunjwa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, CUF ilikuwa na uwezo wa kuunda kambi ya upinzani bila ya kushirikisha chama kingine cha upinzani na ilifanya hivyo mwanzoni mwa Bunge lakini baadaye chama hicho kilishirikisha wabunge wa vyama vingine ambavyo ni Chadema, UDP, na TLP.

  Katika mazungumzo yake na Raia Mwema kuhusu mazingira hayo, kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni aliyemaliza muda wake Hamad Rashid Mohamed amesema taratibu za sasa zinabainisha chama chochote cha siasa kinaweza kuunda kambi yake kama kitafikisha asilimia 12 ya wabunge wote wa Bunge.

  Wabunge hao wanaopaswa kuunda asilimia hiyo 12 ni wa majimboni pamoja na wa viti maalum ambao idadi yao kutoka katika chama cha siasa inategemea idadi ya kura za urais alizopata mgombea urais wa chama hicho.

  Mgombea urais atakayekuwa na kura nyingi za urais ndiye chama chake kitapata wabunge wengi zaidi wa viti maalum.

  Kwa mwenendo ulivyo, Raia Mwema imebaini kuwa wagombea wa urais wanaotarajiwa kupata kura nyingi zitakazowezesha vyama vyao kupata wabunge wengi wa viti maalum ni Jakaya Kikwete wa CCM, akifuatiwa na Dk Wilbrod Slaa wa Chadema huku Profesa Ibrahim Lipumba akiwa katika nafasi ya tatu….
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ukiwa chama kikuu cha upinzani kunakuwa na faida gani?
   
 19. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kwa hiyo uko tayari kuona ccm wanatimiza lengo lao la kuifanya cuf isimamie hoja za upinzani bungeni??? For your information mimi nafuata nyayo za baregu na marando ambao hawajawahi kuwa wanachama au mashabiki wa ccm maisha yao yote!!! Nachukia sana mafisadi, naichukia sana ccm. CUF hawana msimamo wala hawatishi bungeni
   
 20. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Lyatonga ameingia na lengo la kuharibu upinzani bungeni. lakini kwa vichwa vilivyoingia katk bunge la mwaka huu hataweza! Moto wa mageuzi hauwezi zimwa kirahisi hivyo, chadema kwa sasa ni sawa na moto uliomwagiwa petrol! It is unfortunate uchaguzi umefanyika in unlevel field with all favouring ccm, na watangazaji na waandishi wa habari kuwa biased to ccm!
  Kila kitu kina mwisho!
   
Loading...