Hujuma: Budget ya Serikali inatumika kuimarisha CCM nchi nzima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hujuma: Budget ya Serikali inatumika kuimarisha CCM nchi nzima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Deus F Mallya, Sep 12, 2012.

 1. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Itakumbukwa kuwa vyama vyote vya siasa hupata ruzuku kila mwezi kwa mujibu wa sheria. Ruzuku hizo zitatumika kuimarisha na kuendesha vyama hivyo kwa kadri itakavyoamuliwa na vyama vyenyewe. CCM kama vyama vingine imekuwa ikipata takriban 1.2billion hivi. Chama hiki kimekuwa kikitumia pamoja na mambo mengine kuwalipa mishahara viongozi wake wa kila Wilaya na mikoa lakini pia kulingana na kauli ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwa pia Wakuu wa Wilaya na Mikoa wana ruhusa ya kuimarisha chama hicho popote walipo.

  Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Wilaya/Mkuu wa Mkoa analipwa posho na stahili zote yakiwemo magari ya kifahari kutoka kwenye bajeti iliyotengwa kuendeshea serikali. Pia huyu akistaafu atalipwa mafao kama mtendaji wa serikali. Kiongozi anapozungumza na kuachwa tu hivi ni kuwa tumeridhia kuwa CCM iwe na ruzuku ya zaidi ya 4.8billion kila mwezi (ukiongeza mishahara na marupurupu ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya) ukilinganisha na vyama vingine kama CHADEMA ambacho hupata wastani wa 233Million kwa mwezi na CUF 98Million.

  My Take: Mara nyingi imegundulika kuwa Waziri Mkuu alilidanganya bunge kwenye majibu yake,Ni vyema sasa kupelekwa hoja binafsi kuhoji uhalali wa watendaji wa serikali kufanya kazi za CCM.

  Ahsanteni.
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,159
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Millya,
  Tunahitaji hili suala kulijadili kwa kina na ikibidi liingizwe kwenye katiba. Si hilo la makada wa vyama kuteuliwa kuwa viongozi wa umma kisha wakaendelea kufanya shughuli za kuimarisha chama badala ya kusimamia sera. Tuwe na utaratibu huo.

  Tunahitaji haya yafuatayo yafanyike kwa wakuu wa Wilaya?
  1. Sifa za kielimu kwa wakuu wa Wilaya (Siyo mnapeleka mtu kama Lusinde - Mbunge wa Mtera kuongoza Wilaya)
  2. Uzoefu wake kwenye uongozi (Kama vile ukuu wa Idara, ukurugenzi nk)
  3. Historia ya uadilifu wake (Criminal/Integrity records)
  4. Nk.

  Lakini katika yote hivi vyeo havina tija kwa taifa hili zaidi sana ni kuongeza mzigo wa matumizi kwa wananchi, huku ukiwanufaisha watawala. Mkurugenzi wa Wilaya na Afisa Tawala wanatosha kabisa kusimamia kila kitu wilayani.

  Nawasilisha
   
 3. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu umeongea vyema. Lakini huo mchakato wa katiba kwangu naona ukungu mbele tayari. Ukungu huo ni namna maoni yanavyoendelea kukusanywa na hatima ya muungano ambapo ni kikwazo kikubwa katika kupitishwa kwa katiba mpya (Kwenye referendum) kwa hiyo tusishangae 2015 tukaingia kwenye uchaguzi bila katiba mpya kwa sababu ya ubovu wa sheria iliyoweka utaratibu huu wa kuandikwa kwa hiyo katiba mpya. Katika kipindi hiki ni vyema tufanye lolote kama kuwasilisha hoja binafsi kupitia kwa wabunge wetu ili serikali itoe ufafanuzi wa Majibu ya Waziri Mkuu.
   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  kwanza kabla ya hoja binafsi Zitto aulizwe ile hoja ya kutaka kumwondoa waziri mkuu iliishia wapi? mbona hakutuambia ameiondoa au imekuwaje!?? mana wakati anakusanya saini za wabunge mbwembwe zilikuwa nyingi kwenye mitandao wakati wa kuiondoa kimyakimya!!
   
 5. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Moja ya mambo makubwa ambayo katiba ijayo inatakiwa kuweka bayana ni kufutwa kwa vyeo hivi vya wakuu wa wilaya na mikoa. Katika ngazi ya mkoa:

  1. Kuwe na Gavana wa mkoa ambaye atachaguliwa kwa kura za wananchi wote badala ya kuwa mteule wa rais. Yeye ndiye awe mtendaji mkuu wa mipango ya mkoa.
  2. Kila mkoa uwe na baraza la uongozi (mfano wa bunge) ambalo litakuwa na jukumu la kupanga na kusimamia mipango yote ya maendeleo.
  3. Mkoa uwe na uwezo wa kuajiri wafanyakazi wake wote.
  Katika ngazi ya wilaya/manispaa/jiji:
  1. Shughuli zote za maendeleo zisimamiwe na wenyeviti wa wilaya au mameya.
  2. Madiwani kama ilivyo sasa waendelee kupanga na kusimamia mipango ya maendeleo katika maeneo yao.

  Kuhusu shughuli zenye sura ya kitaifa kama maswala ya ulinzi, mahakama, polisi, magereza, uhamiaji nk kuwe na mabaraza ya ulinzi na usalama ambayo mwenyekiti wake awe na wadhifa wa waziri na ateuliwe na rais wa nchi. Kama muundo huu utawekwa basi idadi ya mikoa itabidi ipunguzwe ili mikoa iwe na uwezo mkubwa wa kiuchumi.
   
 6. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Bado unaota! Mbona uko nje ya mada!
   
 7. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya yote ni vumbi la uchakavu wa katiba ya 77 kwani inatoa loopholes nyingi kwa chama tawala kutumia budget ya watanzani kujijenga kwa kua haitofautishi chama na serikali. Pia kama m1 alivyosema haihoji uadilifu wa watumishi wa serikali kama ni kwa ajiri ya chama tawala au serikali kuu. Kwa mfano Mkuu wa wilaya ni Ceremonial figure wa kujenga chama tawala wilayani kwani mtendaji mkuu ni MKURUGENZI na MAKATIBU wake.

  Hapa ndio integrity inapokosekana kwani hakuna anaehoji umemteua kwa minajiri ipi? Na kwa kufanya kazi za Chama au Serikali? Wao wanadai serikali ya chama tawala hivyo serikali ni chama, La hasha kwa mfumo huu mtumishi hua na ajira zaidi ya moja at a time na wengine ni wachumba wao, mashangazi, shemeji n.k.
   
 8. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jiulize mawaziri walioondolewa ilikua kulinda kibarua cha nani? Zitto alitaka kumuondoa waziri mkuu ili wale waliochini ya mbawa zake pia waondoke. Baada ya maji kufika shingoni hatimae kumbeba Waziri mkuu ilibidi jopo la Mawaziri kuundwa au kufanyiwa mabadiliko yaliyowaondoa wahujumu uchumi madarakani japo si wote.

  Got t?
   
 9. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  I never argue with fools! sorry!!!
   
 10. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  A fool will never understand himself or herself unless cured and found himself or herself naked!

  Take care!
   
 11. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  You need to take that care as you dont know your right from your left!!
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Yaani kiongozi wa serikali nae ni sehemu ya chama ie conflict of interest
   
 13. mauro

  mauro Senior Member

  #13
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hivi ni baadhi ya vyeo vinavyotakiwa kufutwa tungekuwa na magavana kama watano ama sita tu ambao tunawapigia kura kama za urais tungeweza kusave gharama nyingi mno vilevile hawa magavana wangekua ni watu wanaoshughulikia mambo ya maendeleo zaidi kuliko hawa wakuu wa mikoa kushughulikia mambo ya ccm
   
 14. HGYTXK

  HGYTXK Senior Member

  #14
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Habari zenu wadau,kwa muda mrefu sana nimekuwa nikijiuliza hili swali bila kupata majibu.Nimekuwa nikishuhudia viongozi mbalimbali wa serikali wakitoa pesa au ahadi ktk mikutano mbalimbali ya kijamii mathalini baada ya kusomewa lisala kiongozi anatoa tamko kuwa yeye binafsi atachangia kwa mfano milioni 10 au atachangia mifuko 200 ya cement.Hii inachangia ata kwenye sherehe mbalimbali watu kuvutika kuwaalika viongozi wakubwa wa serikali wakiwa na imani kuwa watachangia au kutatua baadhi ya matatizo yao watakayoainisha kwenye risala yao.Hivi ni kweli viongozi wetu ni matajiri kiasi hiki au kuna fungu wanatengewa kwa ajili ya zawadi kama hizi na udhibiti wake ukoje kama ndivyo?.Mfano halisia ni wa PM aka mtoto wa mkulima kuahidi vijana wajikusanye na kuunda kikundi cha kilimo na yeye binafsi atawachangia milioni kumi na hizi zawadi za kila sikukuu zinazotolewa na Mukulu wetu.

  Nawakilisha.
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Fungu lipo kwenye mengineyo au AOB au miscellaneous.
   
 16. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Acheni matusi jamani, mara muwaite wenzenu Fools mara muwaite watumishi wa umma wana digrii za chupi, hivi nani anawapa jeuri hii??
   
 17. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu siyo zitto tu, hiyo ni sera ya chadema, kwani hata mwenyekiti wake mbowe alipokuwa akirudisha gari la mkuu wa upinzani bungeni zilikuwa mbwembwe kweli kweli, lakini alipoenda kulichukua ilikuwaji? kimyakimya. kama kawa.
   
 18. M

  Maga JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 325
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Pinda nafasi ya uwaziri mkuu imemshinda, kwa kauli yake ile inaonyesha jinsi gani alivyo dhaifu kusimamia rasilimali za umma. Hatuna sababu ya kuwa na wakuu wa wilaya futa wote wakalimie huko kwao
   
 19. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Sasa hapa mpumbav.u ni nani? hhahahahahahaha
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,549
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  ...Mkuu na bado wanachota nyingine nyingi toka hazina ili kugharamia ufisadi wao na mambo mengine mbali mbali ndani ya chama chao cha magamba. Ila mie nina wasiwasi na mambo unayoyaandika hapa na utumiaji wa jina lako, nchi yetu imeharibika Mkuu, tafadhali jilinde.

   
Loading...