PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,203
- 8,720
Jana nililazimika kumtembelea huyu rafiki yangu, amelazwa pale Hospitali kuu ya Rufaa ya KCMC.
Yuko ICU.
Yuko hoi bin taaban. Mtu mwoga hutamtazama kwa sekunde 10!
Mipira kadha imeingizwa mwilini kupitia puani.
Haongei, hasogezi kiungo, hatazami.
Ngozi yote ya asili ya mwili wake imeumuka, imetoka, kama vile amemwagiwa uji wa moto, au kama mnyama aliyechunwa ngozi, tayari kwa kitoweo!
Kwa ufupi, ni kwamba hawezi, anasikitisha!
Ni mwajiriwa wa TANAPA, ni dereva.
Jumatano iliyopita23/2/2010 ilikuwa asafiri kuwapeleka wakuu wake kwenda Mkoa wa Pwani kwaajili ya vikao, lakini jumanne yake ghafla alianza kuumwa sana.
Akakimbizwa Seliani Hospitali, ambapo walipomwangalia, moja kwa moja walimpa rufaa ya KCMC baada ya kuona ugonjwa wake si wa kawaida, na anabadilika kwa kasi ya ajabu kila sekunde zinapoongezeka, anakuwa critical!
Kwa mujibu wa ndugu zake, madaktari hawajagundua ugonjwa, zaidi ya kususpect allergy!
Tukiwa hapo Hospitali, kama kawaida kila anayeingia kumwona akitoka anasema lake!..Lakini kilichonivuta ni kauli za wengi wakisema :
-Safari iliyokuwa afanye huyu ndugu, kuwapeleka wakuu wake Pwani ndiyo inayomponza!
-Wengine wakisema, ni gari jipya alilokabidhiwa aliendeshe, ndo linalommaliza!
Mimi si muumini wa uSHIRIKINA, lakini kauli na simulizi za watu hawa zinatisha!
Wadau niambieni, kuna ukweli gani katika dhana nzima ya kauli kama hizi?