Hugh Williams: Jina lilioshindikana kufa kwenye ajali za meli

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Menai ni jina la mlango bahari uliopo katika bahari ya nchi ya Wales.Eneo hilo la mlango bahari limewahi kukumbwa na ajali nyingi za meli lakini hizi ajali tatu zimeandika historia ya kipekee.

Ilikuwa hivi:-

Desemba 5, 1664 meli ilizama katika mlango wa bahari wa Menai ikiwa na watu 81,karibu watu wote walizama na kufa majini lakini jina la manusura pekee lilikuwa ni Hugh Williams huyu ndio abiria pekee aliyepona kwenye ajali hiyo.

Desemba 5, 1785 ikiwa ni miaka 121 baadae meli nyingine ilizama kwenye mlango wa bahari wa Menai eneo lile like la ajali ya kwanza ikiwa na watu 60 huku kila mtu ndani akifa isipokuwa mtu mmoja tuu aliyeitwa Hugh Williams.

Desemba 5, 1820 tena miaka 35 mbele meli nyingine ilizama kwenye mlango wa Menai eneo lile lile la ajali ya meli ya kwanza na ya pili,ikiwa na watu 25, mtu mmoja tu ndiye aliyeokoka, na aliitwa Hugh Williams.

Historia imeandika kuwa baadaye pia meli nyingine mbili zilizama hapo hapo na mmoja wa watu waliopona jina lake lilikuwa ni hilo hilo Hugh Williams japo hizo hazikuzama tarehe hiyo ya December 5.

Matukio haya yote yamebaki kuandikwa katika vitabu pekee na kuhesabiwa kama ni mojawapo ya matukio ya kushangaza duniani, hakuna aliyewahi kuelezea lolote kuhusu jina hilo la Hugh Williams.

UNAONAJE NA WEWE UKAANZA KUITWA HUGH WILLIAMS?
 
Back
Top Bottom