Huenda Rais Magufuli akawa ameumaliza rasmi ule ubishi wa Chuo Kikuu gani bora kati ya SAUT na UDSM

Sawa je una maoni gani kuhusu Waheshimiwa na Wasomi Wanazuoni Waandamizi kutoka hapo UDSM akina Kabudi na Mpango kila mara Kuambiwa au Kutukanwa Wapumbavu katika Simu na Mheshimiwa Rais JPM kama alivyosema Yeye mwenyewe?
Sasa wasingesoma wakati huo wanasubiri huu mkumbo wa vyuo vya kata?
 
Katika Utafiti wangu mdogo tu na hasa kwa kumfuatilia Mheshimiwa Rais akiwa anachukizwa na Watendaji wake nikagundua kuwa wengi wao ni Wasomi wakubwa tu kutoka Chuo Kikuu cha UDSM ambacho huwa anapenda Kuwaokota huko mara kwa mara katika Teuzi zake Serikalini.

Na hata Uchunguzi wangu mdogo tu nimegundua kuwa wengi wa wale ambao Mheshimiwa Rais JPM amekuwa akiwatumbua na kuchukizwa nao kwa Utendaji wao mbovu pindi anapowateua ni kutoka hapo hapo UDSM.

Kuna Ubishani ambao nilikuwa nikiuona hapa Jukwaani kutoka kwa Members waliosoma UDSM na wale wa SAUT ila bahati mbaya sana Majina yao hao Members nimeyasahau lakini kuna Mmoja ni Mtetezi mzuri kabisa wa Chuo Kikuu chake cha SAUT ( nikimkumbuka nitamtaja ) alikuwa mara kwa mara akisema kuwa Chuo Kikuu cha UDSM sasa kimebaki tu Jina na wapo ambao walikuwa hawataki Kumuamini au Kukubaliana nae.

Kwa mtazamo wangu nadhani sasa mara baada ya Mheshimiwa Rais JPM kuwaita Mawaziri wake ambao ni Wasomi na Wanazuoni Waandamizi kabisa akina Kabudi na Mpango kuwa ni Wapumbavu katika Simu alizokuwa akiwapigia huenda hapa tayari lile Hitimisho la Chuo Kikuu gani bora kati ya SAUT na UDSM likawa limepatikana. Kwani sijawahi kuona Mheshimiwa Rais akiwatukana Wasomi wa SAUT bali naona kila mara akiwatukana tu wa UDSM.

Tujadili.
Huyu ni popoma
 
Acheni ujinga wa kufananisha takataka na UDSM. UDSM ina udhaufu wake lakini si wa kulinganisha na SAUT. Hata uwe kipofu, huwezi linganisha sisimizi na tembo.
Inawezekana maana UD inatoa ma PhD holder watoto juha kiengereza wakati tangu sec anejifunza masomo yote kwa lugha hiyo hiyo anayo haijui na haipendi
 
Mleta mada hayuko serious anawatania na kuwachangamsha kidogo so kwa niaba yake nawaimba msichulie serious saaanaaaa hiki alichokiandika. SAUT hii ya ma GPA makubwa ya kujiokotea hata wasiojali kusoma? SAUT hii ambayo mtu anaruhusiwa Ku carryover hata course saba na maisha yanasonga tu na mwisho Wa siku anatoboa vema tu?
 
Kiongozi kuna vitu fulani huhitaji nguvu kuvishindanisha. Ni sawa unashindanisha Simba na Liverpool. Ni kujifurahisha tu. Kuna vyuo vimejengwa kwa misingi ya umri, reputation (muulize mwanafunzi yeyote anayetaka kwenda chuo chaguo lake la kwanza ni lipi kati ya UDSM na SAUT, kuna chuo atakikataa hata akiwa usingizini unless pass-marks zake ni ndogo na anajua zitamnyima sifa za kwenda chuo hicho kikongwe), walimu, tafiti, na pia usisahau UDSM ni comprehensive university.

UDSM ni chuo pekee Tanzania kilichopo miongoni mwa vyuo 16 vikongwe na bora barafu Afrika kupitia mwamvuli wa African Research Universities Alliance (ARUA).

SAUT kabla hata haijaingia kujilinganisha tu na UDSM iangalie quality of students and lecturers ilionao. Lakini pia staff:student ratio zinazosababisha college zake kama ya AJUCO Songea ifungwe kwa kukosa walimu na facilities.

Ni upuuzi tu kuanzisha thread zisizo kichwa wala miguu ambazo waanzishaji ni watu waliokosa nafasi ya kusoma vyuo vyenye sifa.

Chuo chenye sifa ila kinazalisha watu wapumbavu.OVER
 
Hivi hiki Chuo cha SAUT kipo Mkoa gani nchini Tanzania kwani nimekuwa nikisikia Watu wengi wakikitaja na wakikisifia kuwa ni Kizuri na kwamba Wanafunzi wengi wanaosoma na kutoka hapo huwa ni Werevu kupita wale wa Vyuo vingine vya Tanzania. Nauliza hivi kwakuwa Mimi sijabahatika kufika hadi Chuo Kikuu Kielimu kama wengi wenu humu au hapa.
Gentamycin una vioja kweli kweli.

Unaiona SAUT kama havard

UD ni UD tu hata wewe mwenyewe unatamani ungesoma UD lakini basi ndo ivo qualifications hazikutosheleza.

Pole sana mzee
 
Katika Utafiti wangu mdogo tu na hasa kwa kumfuatilia Mheshimiwa Rais akiwa anachukizwa na Watendaji wake nikagundua kuwa wengi wao ni Wasomi wakubwa tu kutoka Chuo Kikuu cha UDSM ambacho huwa anapenda Kuwaokota huko mara kwa mara katika Teuzi zake Serikalini.

Na hata Uchunguzi wangu mdogo tu nimegundua kuwa wengi wa wale ambao Mheshimiwa Rais JPM amekuwa akiwatumbua na kuchukizwa nao kwa Utendaji wao mbovu pindi anapowateua ni kutoka hapo hapo UDSM.

Kuna Ubishani ambao nilikuwa nikiuona hapa Jukwaani kutoka kwa Members waliosoma UDSM na wale wa SAUT ila bahati mbaya sana Majina yao hao Members nimeyasahau lakini kuna Mmoja ni Mtetezi mzuri kabisa wa Chuo Kikuu chake cha SAUT ( nikimkumbuka nitamtaja ) alikuwa mara kwa mara akisema kuwa Chuo Kikuu cha UDSM sasa kimebaki tu Jina na wapo ambao walikuwa hawataki Kumuamini au Kukubaliana nae.

Kwa mtazamo wangu nadhani sasa mara baada ya Mheshimiwa Rais JPM kuwaita Mawaziri wake ambao ni Wasomi na Wanazuoni Waandamizi kabisa akina Kabudi na Mpango kuwa ni Wapumbavu katika Simu alizokuwa akiwapigia huenda hapa tayari lile Hitimisho la Chuo Kikuu gani bora kati ya SAUT na UDSM likawa limepatikana. Kwani sijawahi kuona Mheshimiwa Rais akiwatukana Wasomi wa SAUT bali naona kila mara akiwatukana tu wa UDSM.

Tujadili.
Kwa kumuangalia rais mwenyewe na mambo yake, wala huna haja ya kwenda kwa kina Kabudi na Mpango, unapata jibu la elimu yake UD.
 
Back
Top Bottom