Huenda Rais Magufuli akawa ameumaliza rasmi ule ubishi wa Chuo Kikuu gani bora kati ya SAUT na UDSM

UDSM, Mzumbe, SUA vina level yake.
SAUT, SJUIT, na vingine vyenye majina ya watu navyo level yake.

Eti akina Miyeyusho kujilinganisha na akina Tyson.
 
Usifananishe SAUT na SJUT. SAUT NI sawa na MacMillan Training vollege
SAUT sio cha kulinganishwa na UD bwana embu tuwe na adabu. SAUT kundi lake ni kina SJUT,UoI nk. UD Ilinganishwe na Makerere,Nairobi U,SUA nk......

Pia tukumbuke suala la muhimu UD=Jalalani
 
Mzee Genta katika ID mpya
Katika Utafiti wangu mdogo tu na hasa kwa kumfuatilia Mheshimiwa Rais akiwa anachukizwa na Watendaji wake nikagundua kuwa wengi wao ni Wasomi wakubwa tu kutoka Chuo Kikuu cha UDSM ambacho huwa anapenda Kuwaokota huko mara kwa mara katika Teuzi zake Serikalini.

Na hata Uchunguzi wangu mdogo tu nimegundua kuwa wengi wa wale ambao Mheshimiwa Rais JPM amekuwa akiwatumbua na kuchukizwa nao kwa Utendaji wao mbovu pindi anapowateua ni kutoka hapo hapo UDSM.

Kuna Ubishani ambao nilikuwa nikiuona hapa Jukwaani kutoka kwa Members waliosoma UDSM na wale wa SAUT ila bahati mbaya sana Majina yao hao Members nimeyasahau lakini kuna Mmoja ni Mtetezi mzuri kabisa wa Chuo Kikuu chake cha SAUT ( nikimkumbuka nitamtaja ) alikuwa mara kwa mara akisema kuwa Chuo Kikuu cha UDSM sasa kimebaki tu Jina na wapo ambao walikuwa hawataki Kumuamini au Kukubaliana nae.

Kwa mtazamo wangu nadhani sasa mara baada ya Mheshimiwa Rais JPM kuwaita Mawaziri wake ambao ni Wasomi na Wanazuoni Waandamizi kabisa akina Kabudi na Mpango kuwa ni Wapumbavu katika Simu alizokuwa akiwapigia huenda hapa tayari lile Hitimisho la Chuo Kikuu gani bora kati ya SAUT na UDSM likawa limepatikana. Kwani sijawahi kuona Mheshimiwa Rais akiwatukana Wasomi wa SAUT bali naona kila mara akiwatukana tu wa UDSM.

Tujadili.
 
SAUT hawatukanwi kwa sababu hawajateuliwa katika nafasi hizo kama unavyoamini wewe.

Ni sawa na kuuliza kwanini mtaani kwako tajiri anaheshimiwa kuliko maskini,tajiri ni kwa sababu ni tajiri ana chochote na maskini ni maskini kwa sababu hana chochote.

Lakini siku ya mwisho hakuna cha tajiri wala maskini atakayeepuka umauti na vyote ataviacha juu ya uso wa dunia,hata kabla ya wadudu kuanza kumtafuna wale maskini watakuwa wanagawana mali ya tajiri alichovuna wakati wa uhai wake.

Tuna-discuss petty issues sana.Ile lugha ya Mhe. aliitoa katika mazingira ya kikao kazi.

Pasipokuwa na kazi katika leisure time mbona wana kuwa kama ndugu kabisa.Tuache ku-exagerate issues ndogo kuwa kubwa.

Hivi nyumbani mtoto akikosa hutamwambia pumbavu?Atakuwa sio mwanao tena?
 
Hivi hiki Chuo cha SAUT kipo Mkoa gani nchini Tanzania kwani nimekuwa nikisikia Watu wengi wakikitaja na wakikisifia kuwa ni Kizuri na kwamba Wanafunzi wengi wanaosoma na kutoka hapo huwa ni Werevu kupita wale wa Vyuo vingine vya Tanzania. Nauliza hivi kwakuwa Mimi sijabahatika kufika hadi Chuo Kikuu Kielimu kama wengi wenu humu au hapa.
Kipo karibia mikoa yote
Mfano
Mwanza
Dar
Iringa
Mtwara
Kilimanjaro
Morogoro
Tabora
Ruvuma
Kagera
Na isingekuwa awamu ya 5 basi sa hv kingekuwepo kila wilaya
 
I'd mpya ya Gentamycine
IMG_20190612_195651_785.jpg
 
Kiongozi kuna vitu fulani huhitaji nguvu kuvishindanisha. Ni sawa unashindanisha Simba na Liverpool. Ni kujifurahisha tu. Kuna vyuo vimejengwa kwa misingi ya umri, reputation (muulize mwanafunzi yeyote anayetaka kwenda chuo chaguo lake la kwanza ni lipi kati ya UDSM na SAUT, kuna chuo atakikataa hata akiwa usingizini unless pass-marks zake ni ndogo na anajua zitamnyima sifa za kwenda chuo hicho kikongwe), walimu, tafiti, na pia usisahau UDSM ni comprehensive university.

UDSM ni chuo pekee Tanzania kilichopo miongoni mwa vyuo 16 vikongwe na bora barafu Afrika kupitia mwamvuli wa African Research Universities Alliance (ARUA).

SAUT kabla hata haijaingia kujilinganisha tu na UDSM iangalie quality of students and lecturers ilionao. Lakini pia staff:student ratio zinazosababisha college zake kama ya AJUCO Songea ifungwe kwa kukosa walimu na facilities.

Ni upuuzi tu kuanzisha thread zisizo kichwa wala miguu ambazo waanzishaji ni watu waliokosa nafasi ya kusoma vyuo vyenye sifa.

Mpumbavu mwingine huyoooooo
 
Hivi hiki Chuo cha SAUT kipo Mkoa gani nchini Tanzania kwani nimekuwa nikisikia Watu wengi wakikitaja na wakikisifia kuwa ni Kizuri na kwamba Wanafunzi wengi wanaosoma na kutoka hapo huwa ni Werevu kupita wale wa Vyuo vingine vya Tanzania. Nauliza hivi kwakuwa Mimi sijabahatika kufika hadi Chuo Kikuu Kielimu kama wengi wenu humu au hapa.
Nyegezi, Mwanza
 
Saut ni levo za teku, tumaini, muccobs, st.john....kuna vitu vingine ukivipa kiki kwa kutumia mgongo wa vitu vikubwa mwisho wake huwa ni kutoa uharo..

Narudia Tena hakuna utofauti sana wa teku na saut.
 
Sawa je una maoni gani kuhusu Waheshimiwa na Wasomi Wanazuoni Waandamizi kutoka hapo UDSM akina Kabudi na Mpango kila mara Kuambiwa au Kutukanwa Wapumbavu katika Simu na Mheshimiwa Rais JPM kama alivyosema Yeye mwenyewe?
Tatizo lao hawajiamini, sasa Kabudi na usomi wote anasimama na kumsifu rais tu. Mpango naye kila sekta ya fedha inazorota, hamwambii kilaza wa masuala hayo wapi anaharibu kwa kutaka kila mtu aishi kama shetani, unafikiri ataitwa aje kama sio mpumbavu?
 
Yaan unalinganisha genge la wahuni SAUTI na chuo kikuu cha taifa

Ficha ujinga wakoo mkuu, nilikuwa nakuheshimu sanaa ila kumbe unaujinga kwa ndani wa namna hii
 
Hivi hiki Chuo cha SAUT kipo Mkoa gani nchini Tanzania kwani nimekuwa nikisikia Watu wengi wakikitaja na wakikisifia kuwa ni Kizuri na kwamba Wanafunzi wengi wanaosoma na kutoka hapo huwa ni Werevu kupita wale wa Vyuo vingine vya Tanzania. Nauliza hivi kwakuwa Mimi sijabahatika kufika hadi Chuo Kikuu Kielimu kama wengi wenu humu au hapa.
Yaani hapa Mkuu Genta umeshindwa kabisaa kujificha
 
mi nadhani tatizo ni wasomi wanaotoka udsm kujipendekeza kwa ccm
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom