Huenda Joanfaith John Kataraia is best DED of the history, anajituma sana huyu binti

Vugu-Vugu

JF-Expert Member
Feb 24, 2017
1,106
1,265
photo_2022-05-21_06-50-18.jpg


Nawasalimu kwa jina la JMT,

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni,Huyu Mkurugenzi deserves better tuache unafiki,

Wakati Rais Samia Suluhu Hassan anamteua binti huyu mdogo mrembo minong'ono ilikuwa mingi hasa humu mitandaoni,nikiwamo na Mimi,

Majuzi nilifanikiwa kufika Wilaya ya Malinyi kwenye halmashauri ya Malinyi kwaajili ya kununua mifugo,

Awali sikuwa na kumbukumbu ni nani Mkurugenzi wa wilaya ya Malinyi inayoonekana kupiga hatua za kimaendeleo kwa kasi sana nadhani hili wote tuliofika Malinyi mtakubaliana na Mimi,

Nilipodadisi kutaka kumjua,mkurugenzi wa hapa ni nani nikaambiwa anaitwa Joanfaith,

Nilipo -google kutaka kumjua huyo Joanfaith nikakuta kumbe ni yule binti mdogo mrembo uteuzi wake uliyezua mijadala mikali mitandaoni,

Regardless umri wake huyu dada ni kiongozi mahiri sana,na Rais hakukosea kumteua nimeridhika,

Baadhi ya mambo yaliyonifurahisha toka kwa Mkurugenzi huyu ni haya,

1. Nimeshangaa kuona mifugo ya Malinyi inavishwa hereni ( eartags ) bora kabisa kama zile nilizowahi kuziona USA miaka 2016,

Hili limenivutia sana ndio maana nikamwona dada huyu anastahili kuwa juu zaidi ya hapa,

Mkoa mzima ni yeye peke yake na eartags,

Wale tuliofanya biashara ya nyama nje ya nchi tunafahamu huwa tunanunua ng'ombe Tanzania na kuwapeleka Uganda na kuwawekea hizo eartags then tunawauza nje kwa bei ambayo ni maratano zaidi,

Iko hivi, Nikinunua ng'ombe hapa Tanzania kwa shilingi milioni moja asiye na eartag ukimpeleka Uganda na kumuweka eartag unamuuza nje kwa zaidi ya shilingi milioni nne za Tanzania,

Kitendo cha huyu dada kuamua kuweka mifugo yake hereni amenisaidia sana Mimi kama mfanyabiashara wa ng'ombe wa kimataifa,

Sasa nitanunua ng'ombe hapa Malinyi na kuwauza moja kwa moja kwa wateja wangu walioko nje ya nchi, hapa lazima niseme huyu dada ni Mkurugenzi bora kabisa,

Kama kuna mtu wanamalinyi hasa wafugaji wanaweza kumshukuru basi ni huyu dada Joanfaith,

Huenda tukaanza kushuhudia ng'ombe anauzwa hadi milioni tatu hapa hapa Malinyi,

2. Ujenzi wa ghorofa kwaajili ya Halmashauri ya Malinyi, yaani she is doing wonders aise, njooni Malinyi na ninyi mjionee haya ninayoyasema,

3. Kamaliza migogoro ya makulima na wafugaji kabisa hapa,

Natamani halmashauri zingine nao waamke, mkoa mzima wa Morogoro ni huyu binti tu kanifurahisha zaidi hasa kwa Eartags,

Hongera dada mzuri kwa kazi nzuri sana ya kuwasaidia wafugaji na wananchi wako wa Malinyi,
===
Hongera RC,
Hongera RAS,
Hongera DC,
Hongera DAS,
 
Back
Top Bottom