Huenda huu ukawa ni Ujumbe muhimu wa Marais wapenda Sifa, Kunyenyekewa na Kutukuzwa kama Mungu duniani

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,648
2,000
Kiongozi wa Tajikistan ametaka kukomeshwa kwa nyimbo zinazomsifu, televisheni ya serikali imetangaza leo, katika kipindi ambacho sifa kwa kiongozi huyo zinazidi kuongezeka.

Kiongozi shupavu wa muda mrefu, Emomali Rakhmon ameeleza kutofurahishwa na matangazo yaliyozidi kiasi ya kumsifu kwa kutumia video za muziki, kituo hicho kilisema. " Badala yake, rais ameagiza uongozi wa Kamati ya Televisheni na Matangazo ya Redio kujikita zaidi kutangaza habari za wananchi wanaofanya kazi bila ya kuchoka, mafanikio makubwa ya nchi na uasili wa taifa hilo la kale ".

Shikamoo sana na mno Rais Emomali Rakhmon.

Nawasilisha.
 

KWADWO ABIMBOLA

JF-Expert Member
Jan 8, 2019
763
1,000
Kwanza tupitie kauli zenyewe alizozitoa huyu Mh. Rais.
Ya kwanza ni hii: "The impression is being created that everything is ideal, and we lack for nothing,"
Kisw: "Kuna dhana inajengwa kuwa kila kitu (kipo sawa) au ni bora na hatuna upungufu wowote".

Na ya pili ni hii: "expose the defects of authorities and look for ways to correct mistakes"
Kisw: "Zifichueni kasoro za utawala/watawala na muangalie njia za kusahihisha makosa".
Mwisho wa kunukuu.

Nimeisoma makala kwenye link hapo chini nikagundua kuwa huyu Rais amesema ukweli unaoshabihiana na hali tuliyonayo hapa Tanzania kwa sasa. Lakini pia kauli hiyo ni ya kujikosha tu baada ya kufutilia mbali vyama vya upinzani na kufanya ukatili na utesaji kwa wakosoaji kwa muda mrefu. Pia rais huyu anatuhumiwa kuasisi mfumo wa vyombo vya habari vya kusifia kila kitu, huku akiviandama na kuvifungia vile vinavyotoa habari bila upendeleo.

Hapa kwetu tunaelekea kuvifutia usajili vyama vya upinzani kama huyu rais alivyofanya miaka kadhaa iliyopita. Pia vyombo vyetu vimeshashikishwa adabu, hivyo habari zenye balance zinapatikana kwenye mitandao peke yake. Mfumo tunaoujenga ni mfumo utakaotufanya tujute mbeleni. Watakaojuta sio wananchi peke yao, bali pia wanaouasisi. Ipo siku rais wetu ataanza kuona kama taarifa za kwenye vyombo vya habari ni kejeli kama huyu aivyoona.

SOMA Hiyo
Since Tajikistan's President Asked...
 

kokubella

Member
Jan 7, 2019
86
125
Nampongeza wengi wawasifiaji ni wanafiki hata, mtu akikosea hawezi jua mapungufu ya kurekebisha
 

Njopino

JF-Expert Member
Apr 8, 2014
3,468
2,000
Yaa, kwa hili tupo pamoja, shida ya viongozi wetu ni wapenda sifa, wanapenda kujionesha wanakubarika kwa wananchi, kumbe sivyo, wapo tayari kuwanunua watu na kuwapakia kwenye malori ya mchanga wakajaze mikutano, wapo tayari kununua watu washinde jf. na social media zingine ili kuwasifia tu wakati kiuwalisia hawana chochote kwenye maeneo yao ya uongozi, hawana tofauti na Baba mfuga kitambi wakati watoto wananjaa, hawana tofauti na mtu aliyevaa coat la suit ndani amevaa shati la kuchanika. Ni upumbavu, ni upumbavu kwa kuwa kununua air time kutangaza kuwa tunakwenda mbele, wakati watu wanalalamika njaa na hali ngumu ya maisha, we bado umeng'ang'ania nyimbo yako. Haina maana hata kidogo, na hiyo dhambi haitokuacha salama.
Usitumie njaa zao kama silaha za kuwaadhibia na kuwanunua kwa bei rahisi. Waheshimu.
🙏🙏🙏🙏🙏
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,648
2,000
Yaa, kwa hili tupo pamoja, shida ua viongozi wetu ni wapenda sifa, wanapenda kujionesha wanakubarika kwa hili wananchi, kumbe sivyo wao tayari kuwanunua watu na kuwapakia kwenye malori ya mchanga wakajaze mikutano, wapo tayari kununua watu washinde jf. na social media zingine ili kuwasifia tu wakati kiuwalisia hawana chochote, hawana tofauti na Baba mfuga kitambi wakati watoto wananjaa, hawana tofauti na mtu aliyevaa coat la suit ndani amevaa shati la kuchanika. Ni upumbavu, ni upumbavu kwa kuwa kununua air time kutangaza kuwa tunakwenda mbele, wakati watu wanalalamika njaa, hali ngumu ya maisha, we bado umeng'ang'ania nyimbo yako haina maana hata kidogo, na hiyo dhambi haitokuacha salama.
Usitumie njaa zao kama silaha za kuwaadhibia na kuwanunua kwa bei rahisi. Waheshimu.
Pumba.vu🙏🙏🙏🙏🙏
Mkuu hiki ' Kisununu ' chako si cha nchi hii. Pole sana!
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
24,914
2,000
Mleta mada ni vizuri kuwa mkweli hakuna binadamu usiyependa kusiwa hata wewe mwenyewe mpenda sofa mtu akikwambia Uzi wako safi sana si utajisikia Raha? Huo ni unafiki kujifanya ohh fulani anapenda sifa sana wewe hupendi sifa? Kama hupendi sifa mbona mtu akikwambia wewe bwege mbona unakasirika.Kupenda sifa ni tabia ambayo binadamu tumerithi toka kwa Mungu aliyetuumba.Yeye mwenyewe Mungu ni mpenda sifa na hukaa katika sifa !!!!! Mleta mada acha unafiki na huyo mnafiki mwenzio Raisi wa Tajikistan watu wakimsema vibaya utaona huyo Raisi atakavyofoka mnafiki mkubwa huyo Raisi.Kila binadamu hitaji lake Moja kubwa ni kusifiwa
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,648
2,000
Mleta mada ni vizuri kuwa mkweli hakuna binadamu usiyependa kusiwa hata wewe mwenyewe mpenda sofa mtu akikwambia Uzi wako safi sana si utajisikia Raha? Huo ni unafiki kujifanya ohh fulani anapenda sifa sana wewe hupendi sifa? Kama hupendi sifa mbona mtu akikwambia wewe bwege mbona unakasirika.Kupenda sifa ni tabia ambayo binadamu tumerithi toka kwa Mungu aliyetuumba.Yeye mwenyewe Mungu ni mpenda sifa na hukaa katika sifa !!!!! Mleta mada acha unafiki na huyo mnafiki mwrnzio Raisi wa Tajikistan watu wakimsema vibaya unaona huyo Raisi atakavyofoka mnafiki mkubwa huyo Raisi.Kila binadamu hitaji lake Moja kubwa ni kusifiwa
Kwa hiki ' Kisununu ' chako dhidi yangu na huu ' Uzi ' niliouleta hapa nina uhakika ungeniona au ningekuwa karibu nawe basi haraka sana ungeni Akwilina Akwiline ( namaanisha Ungeniua ) kwa Kunipiga risasi Mkuu.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,648
2,000
Ni somo tosha sana huko duniani .

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hasa hasa kwa Kisiwa changu pendwa kabisa ninachoishi cha Puerto Rico Mkuu manake Rais wetu ukitaka umuweze na mambo yako yanyooke Wewe msifie tu Kinyume cha hapo utajuta Kuzaliwa Kisiwani Puerto Rico. Ndiyo maana naipenda mno nchi yenu hiyo ya Tanzania kwani Marais wake wote si Watu wa Kupenda Sifa bali ni Watu wa Kazi Kazi tupu hadi raha.
 

Bay of pigs

Senior Member
Jan 5, 2014
158
250
jitahidi siku moja utembelee huku nchini Tanzania mkuu...
Na hasa hasa kwa Kisiwa changu pendwa kabisa ninachoishi cha Puerto Rico Mkuu manake Rais wetu ukitaka umuweze na mambo yako yanyooke Wewe msifie tu Kinyume cha hapo utajuta Kuzaliwa Kisiwani Puerto Rico. Ndiyo maana naipenda mno nchi yenu hiyo ya Tanzania kwani Marais wake wote si Watu wa Kupenda Sifa bali ni Watu wa Kazi Kazi tupu hadi raha.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,047
2,000
Haya mambo hayawezi kumfarahisha mungu-mtu kama raisi Jacquese Perico Matinezi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom