Huenda CCM ikapoteza jimbo moja kabla ya uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huenda CCM ikapoteza jimbo moja kabla ya uchaguzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Aug 21, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,931
  Likes Received: 12,147
  Trophy Points: 280
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeendelea kupata wakati mgumu baada ya mgombea ubunge wa Jimbo la Nzega mkoani Tabora, aliyedaiwa kuwa si raia wa Tanzania, Dk. Hamisi Andrea Kigwangala kuwekewa pingamizi la kutogombea kiti hicho na vyama vya upinzani.

  Vyama vya upinzani viliwasilisha pingamizi hilo jana, baada ya kutambua kuwa mgombea huyo alitumia jina la Hamisi Andrea likiwa ni la mkazi mmoja wa jimboni hapa.
  Habari zinasema Dk. Kigwangala alikuwa akitumia jina la Said Nasoro tangu akisoma Shule ya Msingi Kitongo.

  Chama kilichoanza kupeleka pingamizi katika ofisi ya Tume ya Uchaguzi wilayani hapa ni pamoja na Chama cha Wananchi (CUF), baada ya mgombea wake, Kizwalo Dominic Clement kuwasilisha barua yenye kumbukumbu namba: CUF /NZG/KM/UCH/17/30 ya Agosti 20, kikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa mgombea wake, John Massanja Mezza.

  Barua ya CHADEMA yenye kumbukumbu namba MJM/CH/I ilisema chanzo cha pingamizi hiyo ni pamoja na kufanya udanganyifu wa jina pamoja na shule aliyosomea.

  Inadaiwa kuwa Kigwangala alikuwa akiitwa Said Nassoro katika Shule ya Msingi Kitongo iliyopo mjini Nzega mwaka 1984 akiwa darasa la kwanza hadi la saba mwaka 1990.

  Barua hiyo inasema: “Mgombea huyu ni wazi kabisa amesoma Shule ya Msingi Kitongo mjini Nzega, kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba 1984-1990 na hakubahatika kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari akiwa anatumia jina la Said Nasoro, hapa hapana ubishi juu ya hili, kwa sababu aliosoma nao wapo na walimu wake wapo, ni ushahidi tosha.”

  Barua hiyo inaeleza aliyesoma shule hiyo yupo kwa jina hilo hilo la Hamisi Andrea na alihitimu masomo yake ya msingi mwaka 1991 na kufaulu na kujiunga na Shule ya Sekondari ya Kigoma.

  Kilichofanyika ni kumdhulumu mwana kijiji huyu, kwani alipofuata masharti ya kujiunga na Idara ya Elimu Nzega, jibu alilopewa ni akasubiri barua nyumbani atatumiwa na idara hiyo, hadi leo hajatumiwa barua hiyo.

  Inadhihirisha kwamba kwa kutopata msaada kutoka shule aliyosomea na kwa kutoelewa kwake, inaonyesha wazi Idara ya Elimu Nzega na Shule ya Msingi Mwanzoli kuna mchezo mchafu ulifanyika. Mgombea wa CCM, Kizwalo Dominic Clement, aliiambia Tanzania Daima kuwa:

  “Hapa kuna ushahidi wa kutosha kabisa ambao unakana kutosomea Mwanzoli Shule ya Msingi Ndugu Hamisi Andrea Kigwangara, kwani Hamisi Andrea halisi yupo, wanafunzi aliosoma nao wapo na walimu wapo hapa, sasa basi kwa hiyo tunaomba atenguliwe, pia ashitakiwe kwa kughushi elimu na kumdhulumu mwanakijiji huyu,’’ alisema Kizwalo.
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  CCM wangelijua hili jambo linavyozidi kuwadhalilisha wangemwachia Bashe tu aendelee kwani inadhihirisha ni chama cha kimafia chenye kufanya jambo pasina ya kujali maslahi ya wananchi. Ngoma nzito hiyo movie linaendelea wacha nikachukue popcorn na soda niendeleee kuangalia haka kamovie tehetehe mwaka huu hata tusiopiga kura tunapiga CCM si mtetezi wa wanyonge sasa inadhihirika!!!
   
 3. P

  Paul S.S Verified User

  #3
  Aug 21, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  haya upinzani tuombe mambo yawe kweli upinzani nao wahesabu jimbo la kwanza kabla ya uchaguzi
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sasa ndio napata stori vizuri..mwanzoni tuhuma zilikuwa nyingi dhidi ya huyu mgombea...mara Mrundi n.k kumbe...

  - Dr Hamis Andrea Kigwangala (tunavyomfahamu sisi) ndiye Said Nasoro aliyesoma Shule ya Msingi Kitongo 1984 - 1990, hakufaulu Stn 7.

  - Hamis Andrea (wa ukweli) aliyesoma Shule ya Msingi Mwanzoli 1985 - 1991 na kuchaguliwa kwenda Kigoma Sekondari (lakini hakwenda).

  Shutuma ni kuwa

  - Dr 'Hamisi Andrea' Kigwangara alikula njama na kutumia matokeo/cheti/jina la Hamis Andrea na kuendelea na masomo.

  Huyu Dr anatakiwa kufikishwa mahakamani kujibu hivi tuhuma; hafai kuwa kiongozi hata wa nyumba kumi.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nyie hamuijui Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC0)? Ni taasisi ya CCM, ngojeni tu muone. NEC hawawezi kukubali 'mabosi' wao waaibike kwa hili.
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  naona presha inazidi kupanda tu aisee.... Hii inanikumbusha ilee sakata ya kufoji umri
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Waache watafunane malipo ya fitna hayo...yanawamaliza wenyewe!
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Tatizo Makamba bado hajapata ufunuo wa madhara yatakayozaliwa na jambo hilo, yeye anajua kupayuka tu!....Anachojua yeye ni kwamba amemfurahisha bosi wake anayempa ajira!
  Kama vyombo vya sheria vitakuwa fair, basi jimbo hili tunalo tayari!
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nasikia juzi trh 19/8 alikwenda mahakamani kuapa kuwa yeye ni Dk. Hamisi Andrea Kigwangala, ndiyo kusema kabla ya hapo kwenye primaries CCM walimchagua Ndugu Said Nasoro au Dr. Hamis Andrew Kigwangala, hapo nachanganyikiwa kidogo.
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama udanganyifu basi ni hatua za kisheria zichukue mkondo wake
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani CCM wanaweza pia kupoteza jimbo jingine tena -- la Singida mjini baada ya Mohd Dewji kuwekea pingamizi na mgombea wa Chadema. Katika pingamizi hilo (nimebahatika kusoma nakala yake) Dewji anatuhumiwa kugawa fulana, khanga, na vyandarua wakati wa zoezi la kura za maoni, baadhi ya vitu vilikamatwa na Takukuru na viko ofisini mwao hadi leo. Naye Dewji alipata kuhojiwa na Takukuru.

  Mfano wa vyandarua -- hivi ni msaada tu kutoka fedha za msaada wa US lakini yeye aliamua kuweka nembo yake, kama vile ni yeye ndiyo alivitoa. Kazi kwenu NEC -- kuhusu hilo pingamizi. By the way Mohd Dewji alichangia CCM bilioni ngapi katika ile fundraiser?
   
Loading...