Huduma zisizorizishwa na Benki yetu ya makabwela NMB | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huduma zisizorizishwa na Benki yetu ya makabwela NMB

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by nema manyanya, Mar 9, 2012.

 1. n

  nema manyanya New Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wana JF, leo nina dukuduku kubwa kuhusiana na huduma zinazotolewa na benki yetu ya makabwela NMB hapa tanzania, hasa katika kipindi hiki cha karne ya 21, dukuduku langu ni kama ifuatavyo.

  1. Usafirishaji wa fedha toka benki yetu ya makabwela NMB inachukua zaidi ya wiki 1 mpaka mwezi mmoja toka matawi ya nmb kwenda mabenki mengine kama NBC, Azania, crdb n.k hata kama hela hiyo inatumwa kwa TISS

  2. Wateja hasa vyama vya ushirika vinavyoshirikiana na mabenki mengine kama nbc, crdb,TIB n.k wanawekewa zengwe sana katika kusafirisha pesa zao toka katika matawi ya nmb kwenda mabenki mengine bila sababu, na wakati mwingine pesa hizo zinacheleweshwa bila hata sababu.

  3. Wateja ambao wanakopeshwa na mabenki mengine na mikopo hiyo kutumwa katika matawi ya nmb wanachajiwa Tshs. 5,000/= kwa kila muamala, hiyokweli ni haki??? Mfano NMB Ngara

  4. Wateja wengi wanalalamikia sana benki ya NMB kwa kuibiwa katika akaunti zao, na wanapotaka maelezo toka kwa wafanyakazi hawapewa majibu ya kuridhisha, na inatokea mteja kunyimwa hata benk statement ili ajiridhishe.

  Tuanomba uongozi wa nmb makao makuu na matawi wafanyie kazi mapungufu haya ili kurudisha imani kwa wateja wenu. Uwingi wa matawi isiwe tatizo la kunyanyasa wateja na kutoa huduma mbofu.
   
Loading...