huduma za tenesco ni mbovu wilaya ya kimara

regam

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
269
51
Wanajamvi. Ninaishi maeneo ya mbezi luis kwenye kakibanda kangu nilikokajenga kwa kujinyima na kufanikiwa kuingiza umeme baada ya kuusubiri kwa takribani miaka minne. Kwenye laini ya umeme niliyovuta kuna tatizo ambalo husababisha kukatika kwa umeme mara kwa mara ikiwa ni kama nyumba nne hivi zinaathirika kwa kukosa umeme. Nilishawahi kuripoti tatizo hili kwenye kitengo cha emergency lakini hawajawahi kufika.
Kutokana na mvua zinazonyesha sasa Dar es Salaam, umeme ndo haujarudi tena jambo lililonifanya niweze kwenda kuripoti na kupewa TB# 11006315 mnamo jumatatu th 19 Dec. Kwa sababu ni emergency niliambiwa watafika ndani ya masaa 24 na hivyo kuniomba niondoke. Lakini cha ajabu hawakuja na kunilazimu kuwafuata siku mbili baadae. Baada ya kufanya hivyo waliniahidi na bado haijazaa matunda na kunilazimu leo th 22 Dec kufuatilia. Niliambiwa niondoke watakuja lakini hadi saa kumi walikuwa bado hawajafika. Nikaamua kuelekea hapo tanesco na kuonana na wahusika. Kama kawaida, waliniomba niondoke lakini nikakataa na ilipofika saa tatu likaja gari na kuniambia ninaondoka nalo. Kwa sababu nilikuwa kwenye kamkoko kangu, wakaniambia niwe mbele na wao wanifuate. Nikafanya hivyo lakini baada ya kufika nyumbani sikuwaona tena na hivyo kupiga simu kuuliza bila majibu ya kuridhisha.
Ilipofika saa tano usiku, nikaamua kuwafuata ofcn kwao na hadi sasa niko hapa. Cha ajabu tangu saa sita hivi nimeahidiwa kwamba gari inakuja lakini hadi sasa haijaja.
Nilichofanya, nikampigia meneja kumweleza yaliyojiri na akanisihi nisubiri. Sasa ni saa saba na nusu usiku, bado nasubiri hii emergency service na niko tayari kukaa hapa hadi asubuhi.
Hivi wadau, nifanyeje ili niweze kufikisha malalamiko yangu kunakohusika ukichukulia kwamba huyu meneja wa hapa anaonekena kutokuwa na msaada wowote?
Naombeni ushauri wenu!
 
Pole mkuu ..kimara nafikiri ni kata iko ndani ya wilaya kinondoni ,jimbo la Ubungo hao inabidi watishwe kama unanamba ya Mnyika mpigie awastue au jikusanyeni kama mpo wengi pelekeni tatizo hapo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom