Huduma za mtandao wa Halotel haziridhishi

numis

Senior Member
May 25, 2017
176
188
Habari wanajamvi,

Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu kuhusiana na mtandao wa Halotel.

Binafsi nimetumia Halotel tangu ilipoanza; kwa bahati mbaya kama wiki tatu nyuma zilizopita nilipata matatizo nikawa nimepoteza laini yao sasa nikawa nimefanikiwa kwenda kwenye ofisi zao; ile nafika majibu ninayoyapata ni kuwa system ya ku-renew laini haifanyi kazi, wakaniambia kesho yake nikarudi tena nikapata majibu yale yale tena nikaacha tena nikasubiri kama siku nne zipite nikaenda tena nikakuta majibu ni hayo hayo bila hofu wala aibu macho makavu kwa kampuni kama Halotel zaidi ya wiki inaisha mtu unashindwa kupata huduma ya kurenew namba yako.

Mbaya zaidi, watoa huduma mliowaeka ni wa hovyo hasa baadhi ya wahudumu wa hapa ofisi kuu ya Arusha wana madharau hawana uweled kweny kazi hawajielewi wana majibu ya kubabaisha yasiokuwa na hatima mm nadhani kama kuna watu wa Halotel huku kwenye hili jukwaa watafanya marekebisho juu ya hili na pia wajitathmini kama mtandao je watoa huduma wao wamekidhi vigezo vya kufanya customer care services.

Au ndo mambo ya kubebana mtoto wa mjomba?

Hasa wa huku Arusha, wa mikoa mingin sijafahamu. Pili, hatupati huduma ya kurejesha namba yapata wiki sasa mpaka nawaza kwenda kusajili laini ya mtandao mwingine.
 
Kwa ofisi za Arusha upo sahihi. Nilishakumbana na hizo "dharau".
Unamuuliza maswali kwa ajili ya huduma, mtu anakuangalia tu bila kukujibu
 
Back
Top Bottom