Huduma za maji, serikali iunde kampuni zitakazofanya kazi kama muundo wa kampuni za simu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Baada ya kusikiliza maoni ya Mheshimiwa Lema aliyoyatoa wiki iliyopita, nimelitafakari sana wazo lake kuhusu huduma ya maji, maji ni muhimu sana kwa maisha ya kila siku ya binadamu. Yakichukuliwa kibiashara biashara ya maji ina faida kubwa.

Tanzania tumebahatika kuwa na vyanzo vingi vya maji, kama kutakuwa na mipango mathubuti ya kuhakikisha miraji mikubwa ya kuchota maji kutoka kwenye boreholes na kujenga reservoirs za kuboresha maji ili yawe salama kwa matumizi ya jamii.

Mfano tu kama kila kaya itawekewa flat rate ya 30,000 na vijijini 20,000. Managing Direrector awe Corporate na apewe nguvu za kufanya maamuzi mradi havunji sheria zilizotungwa na bunge kwa miradi ya jamii.

Kila kanda iwe na kampuni yake inayojitegemea na ikiwezekana serikali itafute share holders. Biashara iwe na msimamo wasiolipia maji wanakatiwa na kama kukitokea mahitaji ya matengenezo taarifa itolewe siku mbili kabla ili watu wahifadhi maji, na matengenezo yafanyike katika masaa 12 ya siku. Kama matengenezo yatakuwa ni zaidi ya masaa 24 magari ya maji yatoe huduma za maji mtaani.
 
Siyo kwenye maji tu ata umeme pia serikali imeshindwa kwenye mambo mengi sana kuitanua sekta binafsi kwanza ingeongeza ajira kama makampuni ya simu yalivyotoa ajira nyingi na pia kodi ingekuwa inalipwa kikamilifu bila mzunguko kuliko Tanesco na idara za. Maji zinavyofanya sasa zinapewa ruzuku lakin hakuna lolote
 
Sijui tunafeli wapi?
Miaka ya nyuma nakumbuka idara ya maji walikuwa wanakuja kusoma meter zetu na watu wanalipa kwa mwezi nyumba nyingi zilikuwa na mabomba ya maji safi
Ooh those old days
 
Sijui tunafeli wapi?
Miaka ya nyuma nakumbuka idara ya maji walikuwa wanakuja kusoma meter zetu na watu wanalipa kwa mwezi nyumba nyingi zilikuwa na mabomba ya maji safi
Ooh those old days
Ile ilikuwa ni system iliyoachwa na wakoloni, idadi ya watu imeongezeka ilhali vyanzo vya maji bado ni vilevile. Mabomba mengi yameoza maana yamekaa ardhini zaidi ya miaka 60.
 
Ile ilikuwa ni system iliyoachwa na wakoloni, idadi ya watu imeongezeka ilhali vyanzo vya maji bado ni vilevile. Mabomba mengi yameoza maana Tameka ardhini zaidi ya miaka 60.

Kweli kabisa nakubaliana na wewe ila kama wangeendeleza tangu wakati huo kungekuwa hakuna tatizo we could catch up with population
Tutafika taratibu
 
Siyo kwenye maji tu ata umeme pia serikali imeshindwa kwenye mambo mengi sana kuitanua sekta binafsi kwanza ingeongeza ajira kama makampuni ya simu yalivyotoa ajira nyingi na pia kodi ingekuwa inalipwa kikamilifu bila mzunguko kuliko Tanesco na idara za. Maji zinavyofanya sasa zinapewa ruzuku lakin hakuna lolote
Hawawezi kukubali maana maji na umeme ni karata kwny mambo yao ya kisiasa,so jibu ni NO
 
Kweli kabisa nakubaliana na wewe ila kama wangeendeleza tangu wakati huo kungekuwa hakuna tatizo we could catch up with population
Tutafika taratibu
Ujamaa uliturudisha nyuma na baada ya hapo Vita ya Kagera ni wakati sasa wa kuacha collectiveness ideology, corporate business zinadeliver.
 
Kama system inakwenda vizuri si credits zinarudi kwao na wananchi wanakosa malalamiko
Si uliona kule kwa Lissu hawakupewa maji sababu jimbo haliko chini yao.

Sasa Private Co's hawawezi wakaziendesha kihiivyo cz zenyewe zina angalia profit tu na zingepeleka maji tu huko na hapo ndipo watagombana na wenye 'inchi'.
 
Mfano tu kama kila kaya itawekewa flat rate ya 30,000 na vijijini 20,000. Managing Direrector awe Corporate na apewe nguvu za kufanya maamuzi mradi havunji sheria zilizotungwa na bunge kwa miradi ya jamii.

Kila kanda iwe na kampuni yake inayojitegemea na ikiwezekana serikali itafute share holders. Biashara iwe na msimamo wasiolipia maji wanakatiwa na kama kukitokea mahitaji ya matengenezo taarifa itolewe siku mbili kabla ili watu wahifadhi maji, na matengenezo yafanyike katika masaa 12 ya siku. Kama matengenezo yatakuwa ni zaidi ya masaa 24 magari ya maji yatoe huduma za maji mtaani.

Auntie, hayo mawazo yako ni ya mtu aliyekulia na kulelewa mjini, ni non applicable katika maisha ya watu wengi wa kawaida ukitilia maanani kwamba watu wengi vipato vyetu ni vidogo.
 
Auntie, hayo mawazo yako ni ya mtu akiyekulia na kulelewa mjini, ni non applicable katika maisha ya watu wengi wa kawaida ukitilia maanani kwamba watu wengi vipato vyetu ni vidogo.
Kama mna kipato mnakuwa na bomba la mtaa mnachangia 5,000 kwa mwezi
 
Si uliona kule kwa Lissu hawakupewa maji sababu jimbo haliko chini yao.

Sasa Private Co's hawawezi wakaziendesha kihiivyo cz zenyewe zina angalia profit tu na zingepeleka maji tu huko na hapo ndipo watagombana na wenye 'inchi'.
Nimekuelewa mkuu
 
Back
Top Bottom