Huduma za fedha za mitandao ya simu zinakwaza sana

Afisa Mteule Drj 2

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
3,135
3,170
Hizi huduma ni za muhimu sana ila mara nyingine zinaweza kukusababishia usumbufu ambao unaweza kujutia kuzitumia

Mara kwa mara nimekuwa nikituma hela kutoka Airtel kwenda TTCL. Kama mara 3 hivi kwa siku tofauti baada ya kutuma pesa unaletewa meseji na Airtel kwamba hela imeenda na unaona kabisa salio limepungua lakini baada ya sekunde chache inakuja meseji nyingine inasema internal system error.

Ikitokea hiyo meseji ujue hiyo hela hautajua iko wapi maana huku imeondoka na kule haijafika.Ukiwapigia TTCL wanakuambia uwapigie Airtel kwamba Airtel ndio wana tatizo.

Ukiwapigia Airtel wanakuambia tatizo ni TTCL. Hapa wanatuchanganya watuamiaji wa hizi huduma mpaka tunaziona za ovyo.Pamoja na hayo nina suspect TTCL ndio anaweza kuwa toto baya. TTCL
 
'KODi Kwanza'

Itakuwa TTCL wanakukata Kodi kimya kimya.

Unacheki jina la mpokeaji kama ni sahihi kabla ya kutuma?
 
Mmi huwa nawapigia TTCL nawakomalia. Nawapa nunber ya muamala waangalie hela ipo wapi. Mara nyingi ukiwapigia Airtel na ukawapa number ya muamala watakuambia kma hela imefika au laa. TTCL wakizingua unaweza waambia Airtel warudishe hela
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom