Huduma Za Afya Nazo Utata!

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,473
2,000
Nilienda eneo moja linaitwa Ipinda kutembelea ndugu jamaa na marafiki nikakutana na kero moja ya huduma za afya.
Wakati DSM na maeneo mengi TZ kumuona Mganga ni 500 lakini kule ni 1500 ambayo to me ni kiasi kikubwa mno kwa watu walio vijijini.Mbaya zaidi naambiwa maeneo mengine ni mpaka 5000 kumwona tuu Dk kwa hospitali za serikali kama Rufaa Mbeya.Wakati juzi tuu nimetoka pale Regend-DSM nikalipia 5000 kumwona Daktari na iyo ni Private hospital.
Hii serikali naona haina ata chembe ya uchungu kwa raia wake gharama za maisha zazidi kwenda juu hasa kwa kuchochewa na vijigarama kama ivyo.
 

NaimaOmari

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
806
195
Njowepo, hapa unampigia mbuzi gitaa ... yani hawajui kabisa wala hayawahusu .. wao ni nje nje na wao kwanzia baba mama na watoto wote wanatibiwa nje.

kwenye mawodi ndiyo usiseme watu wanarundikana watatu mpaka wanne kwenye kitanda kimoja isitoshe wote wanakuwa na maradhi tofauti ...
 

BabaH

JF-Expert Member
Jan 25, 2008
704
225
Ndio hari mpya na kasi mpya hii ndugu
Kwani wao si wanachukua vijisent kibao na kufanya wajuavyo wao, si mnakumbuka makamba alienda juzi tu kucheki afya India, kwahiyo wao hawajali hata kidogo

Na ajabu ni kuwa hospitali za serikali hazitakiwi kuwa na consultation fees jamani, lakini kwa sababu swala la rushwa limechukua nafasi kubwa, basi kila mtu anaambiwa tumia akili yako na nafasi yako kujipatia pesa, sasa ndio haya
tunayapata

This is under CCM, hakuna jipya zaidi ya maumivu makali kila kukicha yanayozidi kuongezeka, na wana CCM wanaona sawa tuuuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom